Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Nafikiri kwa yeyote anayejua mishahara ya viongozi wote iwekwe hapa na tunajadili kama kweli iko feasible kutokana na uchumi wetu. Hatuwezi kulipa kuliko FIRST WORLD bana!!! Ala!
 

FMES,

..hebu tujiulize kama Nancy Pelosi anapata marupurupu kama ya Samuel Sitta.

..serikali haishindwi kumtafutia Spika Sitta makazi ambayo ni affordable kuliko kulipa hizo USD 10,000 kwa mwezi.

..there is a lot of WASTAGE in this country. yaani tukianza na kuziba matumizi ya hovyo-hovyo kama haya nchi hii inaweza kufika mbali sana.
 
Kwanini katika kupunguza matumizi na kuleta mantiki tusiamue kupunguza matumizi kwa viongozi wote wa umma kuanzia Rais, Makamu, Majaji, Wakuu wa majeshi, vyombo vya umma, Wabunge n.k Hiyo ndiyo movement ya kuungwa mkono; lakini hii ya kuchagua mtu mmoja tu...

Wakati wanafunzi wa Chuo Kikuu walipoandamana kwenda Ikulu ya Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 70 kupinga kulazimishwa kuingia JKT na wakidai kuwa kama wataenda JKT basi muda watakaokuwa kule walipwa kama watumishi wa umma, Nyerere aliamuru mishahara ya watumishi wote ikatwe kwani inaonekana ni anasa. Na mishahara yote ikakatwa ili kupunguza hisia kuwa kuna watu wanaishi kifahari mno kutokana na mishahara yao.

Kama tunataka kumkatia "Spita" matumizi ili kuonesha kuwa tunajali hali ya maisha ya watu na kuleta nidhamu ya fedha.. tukate matumizi ya serikali nzima. Lakini ili tujue tunachokata ni kiasi gani hatuna budi kujua viongozi wengine wote wanalipwa kiasi gani, mapango, na pecks nyingine.

Hapa tuwaangalie viongozi wafuatao tu na mtu yeyote mwenye data atumwagie hapa:

Rais
Makamu wa Rais
Waziri Mkuu
Rais wa Zanzibar
Spika na Naibu wake
Mawaziri
Manaibu Waziri
Wakuu wa Majeshi (JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa, Magereza n.k)
Wabunge wote
Wakurugenzi wa taasisi za umma wanaoteuliwa


wanalipwa mshahara wa kiasi gani?
Je wanalipwa posho ya kiasi gani kwa safari ya ndani au ya nje?
Je mawaziri wanapopangishwa nyumba huwa wanalipa kiasi gani?
Pecks zao nyingine ni zipi?
 
Mambo haya tumeyaongelea siku nyingi lakini sidhani kama walioko juu wanasikiliza.

- Yes insanity, damn right!, eti Tanzania tuna ofisa wa serikali anayelipwa USD 18,000 a month? nothing but insanity!

Respect.

Kamanda FMEs!

 
Sera nzima ya kuuza nyumba za serikali na namna zilivyouzwa mimi ninapinga. Hao walionunua, wajue wanakaa kwa muda tu kwani ni LAZIMA hizo nyumba zitarudi tu na zile ambazo hazina sababu ya kuwapo ziuzwe kwa utaratibu wa sheria na sio kupeana peana tu!

Thubut yako;toka mmeingiia bungeni si mlinza na kelele za kurudishwa nyumba za serikali mnajua kinachoendelea..tuache kuwadanganya wananchi ati ata kama wanakaa io siku watazirudisha 5yrs now...warudishe lini????????????
 

Sidhani kama wengi wanam single out spika peke yake kwa makusudi. Laiti perks za viongozi na watumishi wengine wa umma pamoja raisi na makamu wake zingewekwa wazi ungeona outrage kama hii au hata zaidi ya hii.

Hakuna mtumishi wa umma Tanzania anayestahili kuishi maisha ya anasa kupita kiasi kwa gharama za walipa kodi. Perks kama za spika wetu ni epitome ya ujinga!! Halafu kila siku tunaimba nyimbo za kutaka maendeleo wakati vikwazo vya maendeleo ni sisi wenyewe.
 
Mwanakijiji na wengine hapo juu hongereni maana sasa nimeona ule mwamsho wa kuhama kutoka kwa mtu mmoja mmoja na kuivamia serikali kamili,hapa itaeleweka kunazungumzwa lugha gani ,kuliko kumvamia mtu na kufika hadi private yake ,ilhali ni mpangilio unaotokana na serikali.
Hivi ndio hoja inavyojengwa ,katika kutafuta wa kupambana nae na kueweka serikali katika ufisadi ,tunaposema hakuna fisadi mmoja mmoja iwe mnatuelewa ,hawa watu wanalipwa fedha nyingi ili kurubuniwa na serikali na hivyo kukwamisha juhudi zote ,kuanzia juu kupitia mahakamani na kwengineko wameweka donge nono ,ambalo mtu akitishwa tu kuwa kama mshahara haukotushi tutaweka mtu mwengine ,unafikir ni nani atafurukuta ndio tukaona wabunge wengine na waandamizi wengine kama waligandishwa na barafu ,hawafurukuti kuuliza wala kuhoji anaona hapa nikitokeza pua tu ,nitakosa hii feza ,sasa ni bora mtu ajinyamazie ,ndio leo ukaona kila kitu ni lazima ajibu Raisi au Waziri Mkuu wengine wote wameufyata wala hawataki kujihusisha.Ni fedha tu wanayolipwa ndio inawapa jeuri ya kutoweza kuwajibika katika nafasi zao na badala yake wanawaachia walio juu zaidi ambao ndio wanaomiliki uajiri wao.
 

- Mkuu ndio maana nimesema hii ya nyumba ya Spika ni a starting point tu, nothing personal na yeye as Sitta lakini hili la ufujaji wa hela za wananchi kwa kutumia sheria uchwara linajadilika!

Respect.

Kamanda FMEs!
 















Mkuu hapa unaongelea masaki ya msata au masaki ya Dar es salaam peninsular?... Mitaa ile kiwanja kitupu(vichache vilivyobaki) sasa hivi kinauzwa USD 600,0000 na muuzaji hashuki, kununua hekalu la kispika bei ni kati ya 1m -2.5m USD, jiulize kupangisha itakua ngapi


mmhhhhhh nasikia kichefu chefu kwa kweli.,any way swala halisi ni kwamba hakuna mtu alieamua kumjadili....kama sita....,ndio maana hmajaona mambo ya mkewe wala wanawe.....,ila tuwekane wazi nani anatakiwa kujadiiliwa na hatakiwi kujadiliwa.....,
 
huyo ndie mzee wa viwango na kasi. hamkumsikia wakati akijinadi?
 

Zitto: Kwamba na viongozi wengine kama jaji mkuu, etc, wanalipwa kama Sitta, au wanapangishwa nyumba yenye gharama kama Sitta, au wana fanicha kama za Sitta hailalishi au kulifanya tatizo liwe dogo. Yote haya tulikuwa hatuyajui, gazeti la Tanzania Daima likaibua sasa tumeyajua. Sasa na wewe umetusaidia kutufahamisha kwamba hawa jamaa wa BoT na TRA ndivyo wanavyolipana, then actually umekolesha mjadala. Huu ni ufisadi wa kutisha kabisa na mimi ninashangaa sana sisi chadema tunalia na Mkapa kila siku kumbe kuna ufisadi wa kutisha kabisa kama huo ambao tunaujua na tumeukalia kimya!!

In short, hata kama ufisadi au kufuru ya matumizi ya fedha za umma yamehalalishwa kisheria haiondoi ukweli kwamba ni ufisadi. Hizo fedha wanazolipana ni kufuru kwa nchi hii yenye umaskini wa kutupwa. Wewe unajua vizuri sana kwamba hata wenzetu walioendelea sana na ambao ni matajiri wa kutupwa kama UK hawatumii fedha za walipa kodi kulipana kikufuru kama tunavyofanya sisi mapesa kama hayo. To me, this really is dirty, irritating and disgusting!
 
Implies=> Tumseme Raisi tusimseme Kikwete, Tusimseme Lipumba tuseme CUF, Tusimseme Sitta tuseme Bunge (au Spika wa bunge). Mmmm; ati hapo sijui kuna mantiki ipi unataka kutwambia? The president is Mr. Kikwete, what is a difference between critisizing Kikwete and his Presidency? Bunge la Sita na Sita; wapi na wapi?
 

There you are. USD 18,000 and some people dare to defend this, it is simply unbelievably outrageous! Yaani jamani!
 
Masikini yeyote yule hajui thamani ya pesa! Na ndiyo maana maisha yake yote yeye ni masikini!
 

Kitila, umaskini wa Watanzania wengi ambao dalili zake tunaziona katika maisha yao unatokana na ukosefu wa fedha kwenye taifa?
 
Du
Mishahara kama hiyo pamoja imepitishwa kisheria ni kufuru ya hali ya juu.Hapo ndipo utajuwa wanafiki ktk siasa, kwanini hawapigii kelele ni kwa sababu na wao wanapata karibu kiasi hicho ama na wao macho yao yamelenga huko .

Hatuna wana siasa thabiti walio na nia thabiti ya kututoa hapa tulipo, malengo yao ni yaleyale kwa mluzi tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…