Sijasema ya kuwa nimehuzunika na wewe kama Zitto, bali nimehuzunika na hoja ulizozitoa zaidi nikizingatia ya kuwa wewe ni Mbunge wa jamhuri wa muungano. Umesema ya kuwa kununua fenicha za hizo gharama ni part ya commonwealth tradition , kwa hiyo inaonekana tunafanya vitu kwa sababu ni part ya tradition bila ya kujali uwezo wetu. Kwa hiyo inaonyesha hatuna maamuzi yetu wenyewe , ni kama mchezo wa monkey see monkey do.
Ni lazima nyie wabunge pamoja na Spika mtambue ya kuwa cheo mlichopewa ni dhamana , na Tanzania (Tanganyika, zanzibar) ilikuwepo kabla yenu na itakuwepo even after y'all have long gone! Nyerere, alitumikia taifa kwa miaka zaidi ya ishirini lakini alipostaafu serikali ilibidi imjengee nyumba . Nadhani kwa standard za bunge letu la leo hakuilinda hadhi yake vizuri ! The whole thing is ridiculous , watumishi wa serikali ni lazima mjifunze kuishi katika hali ya umaskini wetu.
Zitto umesema ya kuwa maamuzi ya kuuzwa nyumba hayakupitishwa na bunge, na kwa kuwa ile nyumba ya kwanza ya Spika aliyepewa Msekwa bado ipo , kwa nini hiyo nyumba isirudishwe baada ya kutumia milioni 200 kwa ajili ya nyumba nyingine. Mbona serikali ilirudisha nyumba zilizouzwa kwenye makazi ya polisi , kwa nini tusirudishe nyumba hiyo ; after all, Msekwa ana nyumba nyingine aliyopata thru Mke wake.
Swali langu la mwisho kwako , jee unadhani ni sahihi kwa Spika kutembelea gari lenye thamani ya shilingi milioni 300 ?