Aliyekuwa Spika Bunge la Uganda Annet Among akabiliwa na shinikizo la kushitakiwa kwa ufisadi

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,800
Reaction score
2,871
img_20240306_1923558960004774868090728.jpg

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Anita Annet Among, anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa baadhi ya wabunge kufuatia madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Baadhi ya Wabunge wameanza mchakato wa kukusanya saini za kumtimua yeye na wajumbe wengine wa Kamisheni ya Bunge, lakini mchakato huo haujakamilika.

Hata hivyo, Among mwenyewe aekuwa akikausha madai ya ufisadi akijitetea kuwa madai hayo ni njama za wapinga sheria ya ushoga na kuwa anataka ushahidi halisi uwasilishwe mahakamani.

"Mimi si fisadi. Ninalengwa kwa sababu ya nafasi yangu katika kupitisha Sheria Dhidi ya Ushoga," alisema Among wakati wa mojawapo ya vikao vya Bunge.

Pamoja na Among kukanusha shutuma hizo, hatua yake ya kuonyesha utajiri hadharani iliibua maswali mengi. Katika hafla za hadhara, alikuwa akitoa michango ambayo nyakati nyingine ilikuwa mikubwa kuliko ile ya Rais.

Rais Yoweri Museveni naye aemuwa akimtetea hadharani, akisema ni njama za “wazalendo wanaofanya kazi kwa wageni” wanaotaka kumwangusha kwa sababu ya msimamo wake dhidi ya ushoga.
698445526_1529567359178803_1179855169528407023_n.jpg

Moja ya nyumba zinazodaiwa kumilikiwa na Annet Among.

Madai ufisadi

Madai dhidi ya Among yalianzia Machi 2024 kupitia kampeni ya mtandaoni iliyojulikana kama Parliament Exhibition.

Kampeni hiyo ilitoa nyaraka zinazodai kuwa spika huyo alipokea zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 kama posho za safari za nje ya nchi, huku baadhi ya siku akilipwa hadi dola 4,000 kwa siku. Kiwango rasmi cha posho kwa siku ni dola 990.

Pia alidaiwa kuagiza Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya safari 10 za nje ya nchi ambazo hakusafiri. Among na uongozi wa Bunge walikanusha madai hayo, wakisema nyaraka hizo ni za uongo na zimetengenezwa ili kumchafua baada ya kupitisha Sheria ya Kupinga Ushoga mwaka 2023.

Wabunge waliomshikia bango ni pamoja na Theodore Ssekikubo (Mbunge wa Kaunti ya Lwemiyaga), ambaye amekuwa kinara na sauti kuu bungeni akiongoza harakati za kukusanya saini za wabunge ili kuwang'oa makamishna wa bunge waliohusika katika kashfa ya kujigawia Shilingi bilioni 1.7 za Uganda kama "Service Award."

Ssekikubo alimkabili Anita Among bungeni mara kadhaa akitaka uwajibikaji kufuatia uvujaji wa nyaraka za ufisadi mtandaoni.

Mwingine ni Sarah Opendi (Mbung wa Tororo) naye amekuwa mshirika wa karibu wa Ssekikubo katika kusukuma hoja ya kuwawajibisha viongozi wa bunge na amekuwa akipaza sauti mara kwa mara kupinga matumizi mabaya ya rasilimali za umma chini ya uongozi wa ofisi ya spika.

Mwingine ni Alioni Yorke Odria (Aringa Kusini) ambaye amekuwa akihamasisha kuhakikisha saini zinazohitajika ili kuruhusu mjadala wa ufisadi wa uongozi wa bunge zinapatikana, akipinga vikali vitendo vya vitisho dhidi ya wabunge waliounga mkono hoja hiyo.

Wengine ni Timothy Batuwa (Mbunge wa Jinja City Kusini Magharibi) aliyehoji kwa nguvu zote uchunguzi wa sasa wa jeshi la polisi (CID), ingawa amekuwa akihoji hadharani kwa nini mamlaka zilisubiri hadi Among akomeze muda wake wa uongozi badala ya kumchunguza mapema akiwa bado ofisini ili kuzuia hasara zaidi.

Michael Timuzigu (Aliyekuwa Mbunge wa Kaunti ya Kajara na Richard Lumu (Aliyekuwa Mbunge wa Mityana Kusini wanaotaka uchunguzi kwa kiongozi huyo.

Pamoja na shinikiz lote hilo hakuna mashtaka rasmi yaliyofunguliwa dhidi yake mahakamani nchini Uganda kuhusiana na madai hayo.

Vikwazo vya kimataifa

Mbali na madai ya ufisadi, Spika Among anakabiliwa na vikwazo vya kimataifa.

Aprili 2024, serikali ya Uingereza iliweka vikwazo dhidi ya Among, ikimzuia kuingia nchini humo na kufungia mali zozote alizonazo.

Mwezi uliofuata, Marekani pia ilitangaza vikwazo dhidi yake na mumewe, Moses Magogo, kwa madai ya ufisadi mkubwa na ukiukaji wa haki za binadamu.

Among alitajwa pia katika sakata la mabati ya Karamoja, ambapo alidaiwa kupokea mabati 500 yaliyokusudiwa kwa wananchi maskini. Alisema mabati hayo yalipaswa kwenda shule za Bukedea na akaagiza yarudishwe.
 
View attachment 3591699

View attachment 3591700

Ikithibitika amefisidi mali ya umma wa wananchi wa jamuhuri ya Uganda kwa manufaa yake binafsi na familia yake, basi inafaa na anastahili kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya Uganda.

Hilo ni muhimu zaidi kwa maoni yangu kwa niaba ya wananchi wazalendo Tanzania 🐒
 
Back
Top Bottom