Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,602
- 22,707
Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (Mb), amesema Bunge la Tanzania linaendelea kutekeleza wajibu wake wa msingi wa kuisimamia Serikali na kuhakikisha ustawi wa wananchi, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya maendeleo yanayoshuhudiwa nchini ni matokeo ya ushirikiano wa taasisi mbalimbali za dola.
Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari leo Jumatano katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kuhusu Maadhimisho ya Miaka 100 ya Chimbuko la Bunge la Tanzania na masuala mbalimbali yanayolihusu Bunge, Spika Zungu amesema si sahihi kulitaja Bunge kuwa ni dhaifu kwa sababu kila Bunge hutekeleza majukumu yake kulingana na mazingira ya wakati wake, akisisitiza kuwa jukumu kuu la Bunge ni kutunga sheria, kuisimamia Serikali na kuhakikisha ustawi wa jamii.