Hapa tunazungushana maneno tu. Tunajaribu kufanya ionekane kuwa hili la Spika ndilo limesababisha hali mbaya ya maisha ya wananchi wetu. Tunataka (kwa makosa) kubebesha mzigo wa lawama wa matatizo ya wananchi wetu kwenye mgongo wa nyumba ya Spika wa Jamhuri ya Muungano. Kwamba madawati hayatoshi sababu ni nyumba ya spika, n.k
Mwanakijiji,
Kuna tofauti kubwa kati ya kusema
1. Matumizi ya Spika yamesababisha umasikini wetu,
2. Culture ya matumizi kama ya Spika yanatudumaza katika umaskini wetu,
3. Matumizi kama ya speaker yako insensitive kuhusu umasikini wetu
La kwanza haliwezi kuwa kweli kwa sababu, ingawa matumizi ni extravagant, ukiyaweka katika national perspective si makubwa kiasi cha ku affect uchumi wa nchi nzima.
Hili la pili na lile la tatu yana mantiki. Spika huyu hapa amekuwa kama "poster boy" wa hii graft overspending, ukiangalia karibu kila sehemu matumizi mabaya ya fedha zetu chache ni kama mashindano, na kila mtu anataka ku qualify kwenda kwenye Olympics.Kwa vile hizi resources ziko limited, the more we take away from our coffers to finance these lavishly regal lifestyles, the more we are taking away from teachers salaries, and underfunded rural dispensaries etc etc.Kwa hiyo Spika anavuma lakini wako wengine wengi, na tutaanza na yeyote ambaye data zake ziatapatikana na kuonekana kuwa ana matumizi yaliyo outrageous. Mimi binafsi sijali innuendos za Rostam vs Sitta wala nani vs nani, as far as I am concerned wote wachafu tu na vita vya panzi furaha ya kunguru, wakianikana na kuandamana ndivyo tutakavyojua maovu yao zaidi na zaidi.kwa hiyo tofauti na wewe, sichelei kumuumbua fisadi mmoja eti kwa sababu kumuumbua ni sehemu ya vita kati yake na fisadi mwingine, ningefurahi na kambi ya Sitta nayo imwage data tuwaumbue wote, kama wanavyosema watoto wa mjini "ukimwaga ugali namwaga mboga".
Kuna mwaka alikuja Waziri Mkuu wa Sri Lanka ziarani Tanzania, akashuka kwenye ndege ya commercial airlines, tena alipanda economy, watu wakashangaa Prime Minister kapanda economy, lakini yeye akaeleza nchi yangu masikini sana na mimi nasevu hela nyingi sana kwa mwaka zinazotumika kwenye maendeleo mengine simply kwa kupanda economy.Hapo hata kama unaenda kuomba msaada dodnor country wanakuelewa, sio unaingia na GulfStream za kuwashinda wao, wananza kujiuliza huyu masikini kweli? Au wakija kuongea na Spika kwake wanaona vile vi apartment vyao kama matusi kulinganisha na makasri yetu (mawaziri wa nchi za ki Scandinavia sishangai kusikia wanakaa kwenye vi apartment, na wao ndio donors!).Kwa hiyo Sitta is just an anecdote to punctuate this story.But we have to start somewhere.Na sijui the underlying innuendos zikoje, lakini the simple mathematics za GDP per capita ya mtanzania haziruhusu hii extravagant profligacy.
Kwa hiyo ndiyo maana nikasema huko juu kwamba Spika Sitta yuko responsible twice, kwanza kama kiongozi wa institution ya bunge yeye alitakiwa kuwa mfano wa kupiga vita extravagancy hii katika institutional level.
Lakini pia kama Samuel Sitta alitakiwa kuwa na dhamiri itakayomsuta, akiangalia wakulima wa Urambo na maisha yao na yeye anavyoishi kisultani, ilitakiwa imuume kiasi cha kukataa huu uungu mtu usio na mpaka.Ndiyo maana nikasema point ya tatu hapo juu, matumizi kama ya Speaker yako insensitive kwa umasikini wetu.Anakuwa kama hajali umasikini wetu anasema kila mtu kivyake.This is simply not a good quality of leadership for someone leading in a poor country, no empathy at all, no integrity, we do not need such greedy narcissist.
Kuhusu hizo breakdown za perks zao ingefaa wote wapigiwe hesabu za kufuatana na GDP per capita ya mtanzania, na kuwekewa viwango kwamba wakitaka perks zao zipande, wapandishe GDP Per capita (ambayo sasa hivi ipo about 1,300 by 2007 estimates from CIA Worldbook), labda ingeweza kuwapa incentive ya kufanya kweli.