Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Hapa ndipo tutakapo zikumbuka nyumba za serikali, hiyo Government Agency ya serikali ilitakiwa kuanza mkakati wa kubomoa nyumba za zamani na kujenga Maflay ambayo yangeweza kuweka wafanyakazi wengi zaidi na kutengeneza mazingira ya maeneo hayo, na pale wafanyakazi wa serikali wakiamua kuka katika nyumba zao, basi hizoi nyumba zingepangishwa kwa mtu yoyote, mradi pesa ya muhusika, kuhusu viongozi wanao stahili nyumba za serikali kutokana na nafasi zao basi wangelazimishwa kuka katika nyumba stahili ambazo zinamilikiwa na serikali, kama Mkuu wa jeshi, polisi, Mkuu wa Chuo Kikuu, Spika, Raisi , makamu wa Raisi, Waziri Mkuu etc au wafanye study wa nchi zingine wanavyo wapatia nyumba viongozi husika, au hiyo housing allowance. Na kwa kweli kiongozi atakaye shinda uchaguzi mwaka 2010 itabidi afanye mkakati huo wa kuona njia iliyo bora ya serikali kuwa na nyumba stahili kwa baadhi ya watumishi wake au ndio system ya Chuo kikuu ya Housing allowance ya 1m ni ipi inafaa? kuwapa mtaji zaidi hao government agency au tupeane mkononi kila mtu akajenge nyumba yake kwa kutumia hiyo housing allowance.


August,
Ninakubaliana na Housing Allowance!
Iwe ina vigezo...
Hii itawapa uchaguzi wa maeneo wanayotaka, na nyumba wanazotaka;

Kuhusu Nyumba za Serikali...kama ni Uamuzi wangu basi Raisi na Baraza lake tu ndio watapewa nyumba:- kama subsidies. Watalipa!
 
Mimi nafikiri tatizo si kujijua au kutojijua umasikini wetu - hata watu wasio elimu na upeo wanajua sisi ni masikini- bali ni lack of commitment ya kututoa katika umasikini.

Ni kama vile hawa viongozi wamekata tamaa kabisa kuhusu kututoa katika umasikini na sasa wanasema "to hell with umasikini, ponda mali kufa kwaja".Ni kama vile Speaker anasema ingawa nchi ni masikini, Spika kama muwakilishi anawawakilisha wananchi wengine katika kuishi kitajiri.
 
Haya ndio matunda ya Mkapa kugawia watu nyumba zenye hadhi kwa ajili ya viongozi, watumishi wa serikali yake. Sasa hivi spika hana nyumba rasmi yenye hadhi yake.

Pamoja na kuonekana ni kiasi kikubwa, spika wa bunge kwa Tanzania ana uzito sawa na waziri mkuu, kama kupishana ni kidogo sana. Sasa hebu tujiulize, ukifanya market analysis ya real estate Dar es salaam, lile hekalu lenye himaya kubwa anayokaa waziri mkuu, kama kupangishwa angekua analipa kiasi gani?... Si ajabu dola 30,000 kwa mwezi maana lipo katika prime of the prime areas za Oysterbay, with swiming pools, tennis courts, nyumba za maana kadhaa za wasaidizi na mazagazaga ya kila aina.

Sasa mlitaka spika akakae Tandale kwa mtogole ndio mujue anatumikia watu? Kila kazi inastahili zake. Sisi sote tunapoomba kazi tunajulishwa na stahili zetu. Wa kulaumiwa hapo ni wanaoindinisha hayo matumizi ambaye sio spika mwenyewe.

Turekebisha mfumo si kumshupalia mtu.
 
Last edited:
kwanini alipwe house allowance wakati analipwa mshahara kila mwezi sasa zile zinakwenda wapi? hili tatizo la viongozi kupewa kila kitu ndilo linalofanya kusahau uswazi watu wanaishi vipi na kushindwa kutetea bungeni, kama wataishi maisha ya kawaida na kulipwa mshahara wake atajuwa kutetea kule Dodoma kwani ugumu wa maisha anayaona

kweli Tanzania tuna tabaka nne za raia, Viongozi, wafanyabiashara, wafanyakazi waofisi na tabaka la chini wakulima ndio wanaobeba wote walio juu, eti tunasema nchii ni ya wakulima na wafanyakazi, kweli ndio wanaobeba ugumu wote wa maisha,

Tulikuwa na matangazo ya CRDB ya kusukuma grudumu la maendeleo kwenye mlima tulikuwa karibu ya juu, sasa lile gurudumu linaelekea chini tena halina muongozaji kazi kwa aliye chini ole wake

Wakati wa kumn'goa Nduli kule Bukoba, Mwalimu alisema NIA TUNAYO, SABABU TUNAYO NA UWEZO WA KUMPIGA TUNAO, kweli tuliweza leo tena vitu vyote hivyo tunavyo kwa mafisadi tunasubiri nini au aje Mwalimu kutueleza tena?

Huko majuu mbona hatuoni watu kulipwa hela yote hiyo? $8000 ni hela nyingi kwa Tanzania,

Hebu mwenye akili kidogo anisaidie kuweka hesabu kamili ya gharama zote tokea kuchaguliwa spika,mshahara, allowance,gari ya mama kwenda saloon, watoto shule, safari za nje ya eneo,house allowance, umeme,simu,vitafunio wakati wa break bungeni,pamoja package wakati wa kumaliza ubunge

Ikiwa malipo yatafikia $250,000. kwa miaka 5, mimi nilekuwa na akili ndogo hakuna haja ya kuwa na bunge wala spika, huo ni utumiaji wa hela ya wananchi
 
Spika Sitta aandamwa

  • Sasa ahusishwa kwa matumizi makubwa
na Mwandishi Wetu



“Spika ana stahili zake kama Spika, hivyo kulipiwa kodi ya pango kwa dola 8,000 kwa mwezi na samani zake za ndani kugharimu zaidi ya sh mil 200 si jambo la ajabu. Ni kiongozi mwenye hadhi hiyo. Rais anajua, ndiye anayeidhinisha stahili zote za Spika. Hivyo hakuna jambo la ajabu hapo,” alisema Shellukindo.

“

Chanzo: Tanzania Daima

Nani amempa Rais authority ya kuidhinisha haya matumizi ? Mimi nilidhani masuala ya appropriation ni lazima yaanzie Bungeni na sio statehouse.Kwa hiyo Shellukindo anadhani kwa kutaja jina la Rais basi watu ndio watakaa kimya , huu ni ujinga wa hali ya juu. Siyo kazi ya Rais ya kuidhinisha matumizi bali ni kazi ya bunge.

Pia najiuliza hizi samani za shilingi milioni 200 ni za aina gani hizo ? Na hiyo nyumba ya $ 8000 kwa mwezi hiko wapi Dar au Dodoma ? Ili jambo linatia kichefuchefu , na mwisho kabisa na conclude kwa kusema hakuna tofauti yoyote kati ya Rostam na Sitta, both of them are Fisadis ; who are enriching themselves by exploiting Tanzanians.
 
wakati tunabishana kuhusus spika hebu tazameni wenzetu wanavyotengeneza bustani na pathways zao

3038899233_d72791b5ea_b.jpg



sioni kwa nini wasifanye hivi Mnazi mmoja badala ya kupafunga kuonyesha how out of touch kama spika 6
 
GT,

Naah,

Waambie hawa kinamama eti $ 8000 kwa mwezi (probably GDP ya kila mmoja hapo kwa about mwaka mmoja na nusu) ni kiasi fair cha kumpa Spika kwa mwezi kama posho ya nyumba, never mind the other perks for furniture, health care etc.

tan-chick-peas1.jpg


Au ziambie familia zinazokaa hapa, umemcheki huyo lil sista na kindoo? the speaker should be ashamed.

Tanzania-192-setting-550W.jpg
 
Putting things in Perspective:


a. Nyumba hiyo aliyopanga amepanga kutoka kwa nani (hapo ndiyo yawezekana kashfa imelala)

b. Ili kuona kama dola 8000 ni kubwa mno, tujiuliza Mawaziri wanalipiwa kiasi gani katika mapango yao?

c. Kipi ni ghali mno, kujenga jumba lenye hadhi ya Spika (whatever that means) au kulipa gharama ya 8000 kwa mwezi for abt 18 months (sijui alihamia lini, nimechukulia muda uliobakia):

Yaani, kama analipiwa dola 8000 kwa miezi 18 iliyobakia na exchange rateya 1200 tsh.. ina maana hadi ikiisha miezi hiyo itakuwa imegharimu 172.8 milioni. Ukiongeza na hizo za samani, ni 372.8.

Je tunaweza kujenga nyumba ya serikali ambayo itatumiwa na maspika wote wa sasa na hao wajao na ikawa na hadhi ya Spika. If we can't.. then we more than screwed!
 
Jamani hivi nani kati yenu keshafika kweli lile lijiofisi la SITTA?

mimi nishafika nikatembezwampaka anakolala mle ofisini kwake...kufuru

kwanza ana reception mbili za wageni wakawaida then kuna ya watu executive, ana conference room mbili na si hivyo tuu ana chumba cha kulala...na bila kusahau kuwa carpet lililetwa from Spain...sasa hivyo vikorombwezo mle ndani ndio usisikie maani siamini kama Bill Gates au Steve Jobs wana madubwana kama ya spika



samani mle ndani si chini ya milioni 100

one thing is for sure..yule mzee ana taste ya vitu expensive

by the way ukisoma vile vimemo na barua za kudai escort na vingora ndio utajua huyu anataka kukufuru na hasira za KUTOPEWA CHEO ALICHOAHIDIWA NA ROSTAM anamaliza kwetu walalahoi
 
Bomba sana, leo nimetembelea bandara ya Mtwara iliyotelekezwa. Hii bandari ingetumika kidogo tu inge-turn around kabisa maisha ya hawa wamakonde hapa, lakini wapi bana!!

Lakini maisha magumu sana hapa, hotel sh 60,000, ugali/chips/wali kuku 8000-Mtwara!!

Anyway achana na hizi habari wewe, mada hapa ni Spika Sitta-sasa mambo ya Mtwara unayaleta ya nini hapa.

Unaambiwa Spika kupangishiwa nyumba ya dola 8,000, thamani za dola 200,000, benzi ya dola 300,000 katika nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya wananchi wake wanapata chini ya dola 1 kwa siku ni UFISADI ULIOTUKUKA, mimi nakubali wewe unasemaji? Changia mada hii usilete longolongo!

Mkuu unatumia kama laki moja kwa siku hapo Mtwara?bado mambo yako ya TOTOZI,si unajua totozi za Mtwara na sindimba mkuu wetu? unaweza kusahau kurudi Dsm.
 
Last edited:
Mbona Adam Sapi Mkwawa alikuwa anakaa nyumba ya kawaida tu relatively speaking pale nyuma ya ubalozi wa Marekani wa zamani (Laibon) na alikuwa Spika mzuri tu?
 
how much does it cost to buy spika's house i thought 100 - 200million u get very classic house tena dodoma. this is how our leaders are very illiterate. why do they simple buy a house for him! wameshatumia zaidi ya million210 but still they dont have spika's house. wanatucheze 2010 we have to show them they way. huyu spika siamatoka tabora hadhi upi apewe mtu watabora huu. ile nyumba ya serikali tena ilipewa bure kwa nini isimtoshe hamna akili kabisa huyu mzee kwani hakukata .......
 
Mbona Adam Sapi Mkwawa alikuwa anakaa nyumba ya kawaida tu relatively speaking pale nyuma ya ubalozi wa Marekani wa zamani (Laibon) na alikuwa Spika mzuri tu?

hivi ushaona escort aliyodemand mpaka kapewa?

utafikiri yeye ndiyo JK
 
how much does it cost to buy spika's house i thought 100 - 200million u get very classic house tena dodoma. this is how our leaders are very illiterate. why do they simple buy a house for him! wameshatumia zaidi ya million210 but still they dont have spika's house. wanatucheze 2010 we have to show them they way. huyu spika siamatoka tabora hadhi upi apewe mtu watabora huu. ile nyumba ya serikali tena ilipewa bure kwa nini isimtoshe hamna akili kabisa huyu mzee kwani hakukata .......

This is a bit more complex than this.

ASerikali iliambiwa na wakubwa (donor countries, the west) ijitoe katika kumiliki nyumba.Hawa watu walisema hivyo kwa kuangalia systems zao na kufikiri kwamba serikali kumiliki nyumba ni mzigo zaidi ya kuwalipa waajiriwa wake posho. Sasa kinachofanyika ni kama vile watu wa serikali wanasema "Si mmetulazimisha tuache kuwa na nyumba za serikali, basi tutahemea hapa hapa"

Hapa kuna mianya kibao ya abuse.Kwanza hamna transparency, pili hamna uwiano wa market rates na rates za hawa miungu watu ($ 8000 kwa mwezi hilo li mansion ni li Neverland fulani au vipi?)

Hawa wazee wameamua kula tu, washachoka hata kujifake kama wanajali kuhusu umasikini wa nchi.
 
kutokana na maelezo ya Sheik-lukindo wao kama institution ndo walioamua Spika aishi kwenye nyumba hiyo kutokana na hadhi ya cheo hicho.this is so strategic hiyo ni janja ya watu wenye nia ya kukikwaa kiti hicho siku za baadae kwani hadhi ya cheo hicho sio jinsi anavyoishi bali jinsi anavyoimarisha demokrasia nchini kupitia bunge.!!!!
 
Tanzania ni nchi masikini hilo linaeleweka wazi. ni jambo la aibu viongozi wetu kuishi maisha ya kitajiri katika nchi masikini. Ilibidi viongozi wawe mstari wa mbele katika kuupiga vita umasikini na kuonesha mfano katika kubana matumizi yasiyo na ulazima.
Haiingii akilini hata kidogo kwa spika kulipiwa dola 8,000 kwa mwezi kama kodi ya nyumba. Nina wasiwasi kidogo kama yeye spika anajua kwamba analipiwa kiasi hicho cha pesa, hapa inawezekana kuna wajanja wanakula kupitia mgongo wake bila ya yeye kujua. Ila kama anajua na amelikubali hilo basi spika anastahili kuitwa fisadi.

Nashindwa kuelewa kwanini waafrica ni wapumbavu kwa kiasi kikubwa. Tunashindwa vipi kulinganisha mapato yetu halali na matumizi?, kwanini tusiishi kulingana na mapato yetu?, kwanini tunashindwa kuwa vipaumbele katika mipango yetu?, kuna sababu gani ya kutaka kuishi kitajiri wakati sisi ni masikini?.

Bado tuna bajeti tegemezi mpaka leo, lakini tulivyo wapumbavu kile kidogo tunachopewa kujazia bajeti yetu tunakitumia katika anasa. Tumelaaniwa na mungu kwa makosa gani ambayo mababu zetu waliyatenda?. Kwa kweli ni kichekesho mtu kuvaa suti kali ya bei mbaya sana lakini ndani umevaa chupi chafu, mbovu iliyojaa viraka na tena ya kitenge.
 
niliposikia yvone chakachaka katoa gari moja ya msaada KAMA AMBULANCE MTWARA CHOZI LILINITOKA mama yule ana uchungu gani nasi?kamuona mama mjamzito kapanda baskeli masaa mawili si mchezo!sasa ona hapa huyo sitta anajifanya ye mtakatifu wakati anaishi kama malaika.kodi dola 8000 kwa mwezi?mwaka je?gari inaenda kuhudumia kimada wana vimada kibao mi namuona tu ni mzee fulani wa kudandia mambo na si tunamsaidia huku kino kupanda basikeli,mi binafsi namkubali sana msekwa mungu amsaidie popote aendapo,huyu jamaa mwingine,ni muuaji,jambazi.gari 2 zinaenda kuhudumia vimada 2 wakati kuna wananchi 100 or more wanatafuta baskeli ya kuwapeleka wodini wakajifungue?were not serious
 
Yaani, kama analipiwa dola 8000 kwa miezi 18 iliyobakia na exchange rateya 1200 tsh.. ina maana hadi ikiisha miezi hiyo itakuwa imegharimu 172.8 milioni. Ukiongeza na hizo za samani, ni 372.8.

Je tunaweza kujenga nyumba ya serikali ambayo itatumiwa na maspika wote wa sasa na hao wajao na ikawa na hadhi ya Spika. If we can't.. then we more than screwed!


Unaposema nyumba ya hadhi ya Spika unamaanisha ni haswa ? Nyumba ni just part tuu ya tatizo , mbona watu hamzungumzii fanicha na hilo gari zilizoigharimu taifa zaidi ya milioni 400.Ni vizuri na hizo kuziweka katika hiyo persepective uliyozungumzia. Ni hadhi gani aliyonayo spika wa Tanzania ( moja kati ya nchi kumi masikini duniani), ambayo tunajaribu kuilinda kwa hizo gharama. Ni hadhi gani ya spika inayozidi annual salary ya Rais wa Marekani?

While children and pregnant women are dying everyday due to lack of health care, our government is spending a lot of money in maintaining Spika's lavish lifestyle. This is plainly pathetic! Instead of utilizing our scarce resources cautiously, these few greedy politicians have embarked on spending spree like drunken sailors. It seems like hadhi ya Spika is more important than serving a child's life. What is wrong with our society nowadays?

Huu ni ufisadi , na hakuna mtu anayeweza kuuweka katika persepective. Hawa watu wanachofanya ni kutafuta mianya ya kuiba tuu. Narudia tena ,Spika Sitta and Rostam share one thing in common, they are both FISADIS.
 
8,000 x 12 x 5 = usd 480,000 in five years only housing; kweli masikini hajijui kuwa ni masikini; hata akili haifanyi kazi. Hata Raisi hana akili![/QUOTE]

Mkuu hapo mmmh, Heri mimi sijaesema aaaahh aahaha aaaaha.
Kwa mtazamo wangu nafikiri Raisi ana akili ila busara ndo MPATUPU. Watu wanaomzunguka ni bure kabisa. Huwezi kufanya hivi vitu kama huna 10% kickbacks, hapa kuna samsing'
 
Back
Top Bottom