aaaahhh!!!....🙁dola elfu nane sio nyingi ila umasikini ndio umewadumaza na kuona ni ela kubwa ,hivi mnaelewa kuwa kwa kila mtz anaemiliki simu ya mkononi (mobile phone au cellular phone) anaweza kumiliki honda pikipiki au gari ndogo ? Mmewahi hata kulifikiria ? Au just mnaona watu wakiagizia vocha ,na kutwa yupo na simu sikioni ?
Kwa hili naona itakuwa mnamuonea tu ,kuna aina mbili za fedha ,inawezekana mtu akasema apewe fedha cash na atajihudumikia mwenyewe na inawezekana serikali inamlipia ,sasa spika analipa mwenyewe au analipiwa ?
...na kama hiyo haitoshi yule mheshimiwa ile bedroom ya kulala pale ndio utafikiri jamaa anakaa kwenye penthouse
Ikiwa analipiwa au analipwa wa kumlaumu na kuilaumu ni serikali ,sio spika wala mic. Yeye ameajiriwa na analipwa na muajiri wake sasa makelele ipigieni serikali ya CCM kuwa ndio inayoimaliza nchi hii,vinginevyo itakuwa choyo tu.Sasa kama hajalipwa hizo hela hapa kwao Tz akalipwe wapi, China ? Halafu hiki cheo ni dhamana kubwa sana ,lazima kiwe na hadhi ya aina yake ,kwa mnavoonyesha hata akilipwa dola 1000 mtaziona nyingi.
Mkuu Mwiba hapa nadhani ndo hoja ilipo, ni tatizo la kimfumo, na mtu anaweza kutoa hoja kwamba anapewa vikolombwezo hivo vote na serikali ili pia asiwe na nguvu za kuibana serikali au miswada mbali mbali hata yenye utata ipitishwe au hoja za kuzima zizimwe, maadamu ssipika kasema kuwa hii sio hoja. au imecheleweshwa au ni ya hovyo hovyo, na hayo tumeshayaona tayari yakitokea
Kinyume na hapo, kwa nini aache nyumba ya serikali akapangishe, eti kuwa sio ya hadhi yake?
Kesho tutamsikia raisi kapanga kule Tabata kwa sababu Ikulu sio ya hadhi yake si imejengwa tangu enzi za mjeremani? sasa hapo tutakuwa tumefikishana wapi?
Vyovyote vile hiyo nyumba ni ghali sana hata mkiitetea.
kama inalipwa na serikali basi kwa uhakika watu wamekula 10% kama ilivyo jadi. huhitaji phd kupata hisia ya bei za nyumba za kuishi TZ, labda iwe ranchi kama ya Michael jackson ndio itakaribia but nyumba tuu. mhh
Umeshaiona au?, nenda ukaitembelee ndani kisha njoo upinge!
Dola elfu nane sio nyingi ila umasikini ndio umewadumaza na kuona ni ela kubwa ,hivi mnaelewa kuwa kwa kila Mtz anaemiliki simu ya mkononi (mobile phone au cellular phone) anaweza kumiliki honda pikipiki au gari ndogo ? Mmewahi hata kulifikiria ? AU just mnaona watu wakiagizia vocha ,na kutwa yupo na simu sikioni ?
Wakuu sasa hapana tunamlaumu Sitta as a person au systme inayomruhusu Spika hata ukiwa wewe au mimi kukaa kwenye nyumba ya gharama hiyo. Kuna institutional corruption lazima tuikemee pia. Tatizo hakuna mwenye uwezo na hakuna mechanism ya kupambana na bunge as institution.
.Wewe Mwiba huu utafiti umeufanya lini? Au data hizi umezipata wapi? Mimi kiwango cha juu cha matumizi yangu ya simu ni sh. 10,000 kwa kwezi ina maana kwa mwaka natumia si zaidi ya sh. 120,000. Sasa hii pesa inaweza kununua pikipiki au gari? Wengine hawazidishi sh. 5000 kwa mwezi. Sasa ni miaka mingapi atakusanya mpaka anunue pikipiki au gari?
Nyumba ya dola 8,000 kwa kwa mwezi kwa Tanzania ni nyingi sana. Huu ni ufisadi kabisa.
Well, yeye ni kiongozi na alipaswa kuona kwamba kupangisha nyumba ya milioni 10 na kutumia milioni zaidi ya 200 kununua thamani ni tatizo kubwa katika nchi maskini kama Tanzania. Sasa kama yeye haoni kuwa hilo ni tatizo ili aweze kubadilisha, then he is a problem as an individual. Remember, institutional problems are caused by individuals and it is individuals who work in those institutions who should fix them.