Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Hiyo bei ya pango si tatizo inawezekana kabisa ikawa ni sahihi kutegemeana na aina ya nyumba maana hapa bongo zipo apatment simple tu lakini pango lake ni dola 3500 hadi 5000, mfano mzuri ni hizo gorofa zinazooteshwa kama uyoga huko upanga na kariakoo. Mie nina mtu namfahamu anaishi apatimenti hapo karibu na slipway. Ni ya kawaida tu lakini bei ni dola 3500. Pale kariakoo wanapouza vifaa vya umeme kuna gorofa jipya pale. niliwapigia simu kuuliza bei, ni dola 3000. sasa kama huyo mzee 6 amepangishiwa kasri ya kifalme unategemea isifike hiyo bei?

Mimi nadhani kwa suala la utawala bora wangeamua hiyo nyumba kuinunua au kujenga nyingine kwa hiyo dola 450 000, hiyo ingesaidia hata Spika wengine baada ya 6 wangeitumia.

Kuhusu office hilo mimi halinisumbui maana hakuna mtu anaependa kukaa kwenye office iliyo rafu.

Baada ya kusema hayo hebu chunguzeni makamu Spika nae anaishi nyumba ya bei gani?

Mawaziri je? Wabunge? Makatibu wakuu? Ukifuatilia haya maisha ya viongozi utaumiza Moyo wako bureeeeeeeee, wee jitahidi uwe mwanasiasa uingie ulingoni uone kama na wewe hutokuwa kama wao.

Hili ni tatizo letu waafrika. Watu wanajipenda binafsi tu. watu wanapenda kuona wengine wako chini wao wako juu wakati wote.

Waache wenye nafasi wajinafasi
 
Give me a second,

Wajameni, spika ni mtu anaye-report kwa jamhuri ni mtu mkubwa sana, dola 8000 is nothing kwa cheo chake, lazima spika awe sehemu ambayo hatapenda kuhemea kwa kwenda visafari visivyokuwa na maana.

Tumeona watu wengi nyumba za pango ya dola 5000, ni za kawaida sana maeneo ya oysterbay...

Common Kasheshe, huwezi kuniambia dola 8,000 is nothing kwa cheo chake. You must be kidding. Hao unaosema 'wengi nyumba za pango ya dola 5000' ni akina nani? Are you seriously suggesting kwamba dola 8000 ni 'za kawaida'?.

You're defending something that is clearly indefensible. Huwezi kuhalalisha dola 8,000 kwa pango na dola zaidi ya 200,000 kwa thamani katika nchi maskini kama Tanzania hata kama zingetumika kwa Rais wa nchi. Ni rahisi kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro kuliko kuhalalisha hayo matumizi. Simply put, huo nao ni ufisadi, tena unaonuka kabisa!
 
Ebana Kitila ulipotelea wapi bana? Nimekutafuta weeeee lakini wapi. Naona ulisepa baada ya joto la yule hausigeli kuzidi...Lol...
 
Kama habari hii ni ya kweli, ni dhahiri kwamba si yeye peke yake anayeishi kwa style hii.
Swali linakuja, kwanini ametajwa kwanza spika Sitta?
 
Ndo tatizo la kuchagua uongozi wa hovyo maana na matendo yao yanakuwa ya hovyo hovyo..
....kajisemea Mdada Dambisa Moyo:umefika wakati Wa-afrika tunapopiga kura chaguo liwe ni ama the B.Gate's Foundation au Unicef maana ndo-angalau wanatusaidia ktk sekta za Afya/Elimu... otherwise ni nini umuhimu wa hizi serikali zetu basi??
 
Give me a second,

Wajameni, spika ni mtu anaye-report kwa jamhuri ni mtu mkubwa sana, dola 8000 is nothing kwa cheo chake, lazima spika awe sehemu ambayo hatapenda kuhemea kwa kwenda visafari visivyokuwa na maana.

Tumeona watu wengi nyumba za pango ya dola 5000, ni za kawaida sana maeneo ya oysterbay...

Kasheshe sasa unaleta kasheshe ndani ya JF. Unafikiri kukaa nyumba ya USD 8,000 ina uhusiano gani na kumzuia kwenda safari spika? Hilo ni pango la nyumba na kwenda safari ni kwa ajili yake, so tofautisha kabisa mkuu. Pango la USD 8000 kwa Tanzania ni ufisadi. Kwanza si bei halisi hii, lazima kuna cha juu. Hakuna nyumba ambayo ni empty inapangishwa kwa USD 8000 TZ. Nasema empty kwa sababu wamenunua samani za Mil. 200 ambazo nazo lazima kuna cha juu ni samani gani hizo za kufikia pesa hizo? Ni za kujaza ukumbi wa mikutano?

Let us be realistic kasheshe.
 
Ebana Kitila ulipotelea wapi bana? Nimekutafuta weeeee lakini wapi. Naona ulisepa baada ya joto la yule hausigeli kuzidi...Lol...

Aah wapi, mimi nimejaa tele kabisa. Busy tu. Sasa nimepata nafasi kidogo nipo Mtwara kwa wiki moja ndio nimepata nafasi kidogo ya kuingia JF. Wewe unafikiri Bongo ni mchezo, acha bana hata muda wa kuingia JF ni issue!!
 
Wakuu sasa hapana tunamlaumu Sitta as a person au systme inayomruhusu Spika hata ukiwa wewe au mimi kukaa kwenye nyumba ya gharama hiyo. Kuna institutional corruption lazima tuikemee pia. Tatizo hakuna mwenye uwezo na hakuna mechanism ya kupambana na bunge as institution.

The unabashed temerity characterized by this culture of sheer grandiosity and wanton largesse will sooner than later bankrupt our sovereign coffers

1. Pamoja na institutional corruption, pia kuna personal responsibility na integrity hapa.Kama mtu ana responsibility kwa wananchi masikini na intact integrity, anaweza kukataa hili na kuanzisha movement ya kubana matumizi.Sitta hakufanya hivi bila ya aibu, kwa hiyo as much as kuna institutional corruption, lakini institutions ni nini? institutions si zinajengwa na watu? Na watu wenyewe si ndio hawa viongozi wa hizi institutions kama kina Sitta? Sasa kwangu mimi Sitta badala ya kuwa absolved lawama anabeba lawama twofold, moja kwa kutokuwa na personal integrity na kukubali hizi hela, na mbili kwa kukosa institutional leadership ya kuweza sio tu kukataa yeye mwenyewe, bali kujenga movement ya kukataa ubadhirifu huu wa mali ya umma.

2.Kuhusu bunge kukosa mechanism ya kulikosoa, even in the failure of the Grecian trias politica checks and balance as a mean of separation of powers, in theory wananchi wana uwezo wa kuliadibisha bunge.Sitta anajifanya anaijua sana hela, OK, next uchaguzi tunamtoa ubunge tuone kama atakuwa Spika kwa nguvu.I understand unaposema hakuna mechanism practically kwa sababu watanzania hawapigi kura on the issues or merit of a person, kwa hiyo hii ni moja ya kazi zetu kujenga grassroot organizations zitakazoonyesha ukweli na kuweza kuanzisha huu utamaduni wa uwajibikaji kwa wananchi.
 
Last edited:
Aah wapi, mimi nimejaa tele kabisa. Busy tu. Sasa nimepata nafasi kidogo nipo Mtwara kwa wiki moja ndio nimepata nafasi kidogo ya kuingia JF. Wewe unafikiri Bongo ni mchezo, acha bana hata muda wa kuingia JF ni issue!!

Alaaa kumbe uko Mtwara...unakumbuka kuna siku nilisema kuwa Mtwara kuko freshi kuna beach za nguvu halafu ukaniuliza kama nshawahi kufika au nilikuwa naleta longolongo tu...sasa wewe unapaonaje?
 
Alaaa kumbe uko Mtwara...unakumbuka kuna siku nilisema kuwa Mtwara kuko freshi kuna beach za nguvu halafu ukaniuliza kama nshawahi kufika au nilikuwa naleta longolongo tu...sasa wewe unapaonaje?

Bomba sana, leo nimetembelea bandara ya Mtwara iliyotelekezwa. Hii bandari ingetumika kidogo tu inge-turn around kabisa maisha ya hawa wamakonde hapa, lakini wapi bana!!

Lakini maisha magumu sana hapa, hotel sh 60,000, ugali/chips/wali kuku 8000-Mtwara!!

Anyway achana na hizi habari wewe, mada hapa ni Spika Sitta-sasa mambo ya Mtwara unayaleta ya nini hapa.

Unaambiwa Spika kupangishiwa nyumba ya dola 8,000, thamani za dola 200,000, benzi ya dola 300,000 katika nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya wananchi wake wanapata chini ya dola 1 kwa siku ni UFISADI ULIOTUKUKA, mimi nakubali wewe unasemaji? Changia mada hii usilete longolongo!
 
Jamani siyo sitta peke yake, angalia maprofesa wote wa vyuo vikuu ni kwamba wanalipwa hela ya kupanga nyumba sh. 1,000,000/- kwa mwezi lakini wanakaa ktk nyumba zao walizo kwisha jenga. Je, hiyo ni sawa??

Ndiyo maana ufisadi hauwezi kuisha na utaendelea. Kwamnza muulizeni VC wa mzumbe mbona ameacha nyumba yake ya kikazi pale MU na sasa anaishi Moro mjini na wakati huo huo analipwa pesa ya nyumba (housing allowance) kila mwezi??

Miafrika ndivyo tulivyo!!!!

Hiki ni kitu tofauti kabisa.Posho ya nyumba, kama iko reasonable haina tatizo, na haijalishi kama mtu anakaa kwenye nyumba yake au anatumia hizo hela kupanga.The point ni kwamba kama unapanga tumia hizi hela kupanga, kama ulishajenga unaweza kufanya hizi hela kama compensation, bottom line ni kwamba muajiri ame ji commit kulipia malazi, regardless kama muajiriwa ana malazi au hana, ni right yake.

Kinachopingwa si posho ya nyumba, ni kiasi kinachotolewa, ukitilia maanani umasikini wetu.

Kama unapinga wahadhiri wenye nyumba kulipwa posho ya nyumba sitakuelewa, je kwa kutumia msingi huo huo unaweza kupinga wahadhiri wanaotoka familia tajiri kulipwa mshahara? Principle ni ile ile, mhadhiri anakuwa rewarded kutokana na kazi yake, regardless kama anahitaji anachokuwa rewarded au la.

Lakini kama unachokataa ni hiyo figure ya milioni moja, kwa upande mmoja wengine watakwambia wahadhiri kwa hadhi yao hapo ni sawia, na kuwaminya sana kunaweza kusababisha wahadhiri wetu wakimbie nchi, na wengine watasema wahadhiri wanaweza kupata nyumba nzuri tu za hadhi zao kwa nusu ya posho hiyo.
 
Bomba sana, leo nimetembelea bandara ya Mtwara iliyotelekezwa. Hii bandari ingetumika kidogo tu inge-turn around kabisa maisha ya hawa wamakonde hapa, lakini wapi bana!!

Lakini maisha magumu sana hapa, hotel sh 60,000, ugali/chips/wali kuku 8000-Mtwara!!

Anyway achana na hizi habari wewe, mada hapa ni Spika Sitta-sasa mambo ya Mtwara unayaleta ya nini hapa.

Wewe ndo umeleta mambo ya Ntwara...Lol

Unaambiwa Spika kupangishiwa nyumba ya dola 8,000, thamani za dola 200,000, benzi ya dola 300,000 katika nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya wananchi wake wanapata chini ya dola 1 kwa siku ni UFISADI ULIOTUKUKA, mimi nakubali wewe unasemaji? Changia mada hii usilete longolongo!

Kulaleki walahi! Nyumba ya dolari elfu nane kwa mwezi? Hii mijamaa inakula nji yetu aisee. Unajua Marekani mortgage note ya dolari elfu nane kwa mwezi ni ya jumba la aina gani?

Halafu hilo benzi la dolari 300,000 ni benzi gani hilo? Maybach? Na samani za laki mbili? Hapana bana...hii haiwezi kuwa kweli....ila kama ni kweli sisi tuko mijinga sana. Unajua kwa mfano hizo laki mbili za samani na hizo laki tatu za benzi zingeweza kutumika ku furnish madawati na vitanda vya hospitali vingapi?

Unajua hata lile Cadillac la Obama usikute hata halifiki dola laki tatu...au hata kama likifika angalau wao watakuwa na justification kuwa raisi wao anatafutwa kuuliwa na Al Keda 24/7.....sasa sisi li spika letu nani anataka kulidhuru? Mimi hata nikiliona linadandia kipanya sita maindi.
 
Nchi hii. Tanzania hii. Ina watu hawana huruma. Na si hivyo tu hawana hata chembe ya haya.

Fikiri mtu na akili yake yote. May be ni msomi wa juu kabisa. Kakaa mbele ya key board yake anaona ni sawa waheshimiwa wetu kuwa extravagant mbele ya umaskini wetu huu ambao watoto wetu wamekosa mikopo ya kwenda vyuoni na wanaopata wanapata asilimia 40% wakatafute nyingine wenyewe! Wale wa sekondari wanalazimika kufunga shule mwezi mmoja kabla maana wazabuni hawatoi chakula kwa kutolipwa stahili zao!

Hivi kama ni wewe waweza kufikiliaje watu wa aina hii?

Gggggggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Jamani siyo sitta peke yake, angalia maprofesa wote wa vyuo vikuu ni kwamba wanalipwa hela ya kupanga nyumba sh. 1,000,000/- kwa mwezi lakini wanakaa ktk nyumba zao walizo kwisha jenga. Je, hiyo ni sawa??

Ndiyo maana ufisadi hauwezi kuisha na utaendelea. Kwamnza muulizeni VC wa mzumbe mbona ameacha nyumba yake ya kikazi pale MU na sasa anaishi Moro mjini na wakati huo huo analipwa pesa ya nyumba (housing allowance) kila mwezi??

Miafrika ndivyo tulivyo!!!!

Magezi, serikalini ukifikia level fulani ya mshahara unakuwa entitled 30 % ya mshahara wako kama House allowance si kwa maprofesa peke yao. Na hii ni halali kabisa. Sasa kwanini nikae kwenye nyumba ya serikali wakati nina nyumba yangu? Vilevile kumbuka kuna wengine wamekaa kwenye hizo nyumba za serikali na wakajisahau wanakuja kushtuka wakati wanapostaafu na kuambiwa wahame kwenye nyumba. Wengine wameishia kuwa frustrated na kuishi maisha ya taabu sana baada ya kustaafu.
 
Unajua mimi niko majuu natengeneza kisu kizuri, naishi vizuri, simfisadi mtu, nasaidia ndugu, dhamiri yangu hainishitaki halafu mtu aje eti anishawishi nirudi nikafanye kazi bongo. I just can't. I'm not used to being a fisadi and I can't live the life I live now over there depending only on employment...
 
Give me a second,

Wajameni, spika ni mtu anaye-report kwa jamhuri ni mtu mkubwa sana, dola 8000 is nothing kwa cheo chake, lazima spika awe sehemu ambayo hatapenda kuhemea kwa kwenda visafari visivyokuwa na maana.

Tumeona watu wengi nyumba za pango ya dola 5000, ni za kawaida sana maeneo ya oysterbay...
Don't be a pompous fanatic:
AngloAmerican PLC executive analipwa house allowance dollar 6000 kwa sababu anazalisha
Glencore AG Marketing executive analipwa allowance ya dollar 4000 kwa sababu anazalsha
Swedesh Government official from a rank of minister haruhusiwi kukaa kwenye hotel above 4 star hotel akisafiri
Ma-Officer wa Bank ya dunia (wakotoaji wa msaada) wakisafiri na Ma-officer wa Bank Of Tanzania (wapokeaji wa msaada) kwenye ndege, Watoaji msaada hukaa business class, na wapokeaji msaada (Tanzania) hukaa first Class!
Uliona last week kwenye CNN Mshahara wa Obama/Biden/Clinton ni Kiasi gani?
Do you know Mawaziri wa China nchi ambayo inawapa misaada akina sita mishahara yao haizidi dollar 3000?

Masikini hajijui. Tukishaanza kujitambua kuwa sisi ni masikini basi hapo ndiyo tu-discuss maendeleo! Kwa sasa tunampigia ng'ombe filimbi!

Mungu atuhurumie!
 
Hapa ndipo tutakapo zikumbuka nyumba za serikali, hiyo Government Agency ya serikali ilitakiwa kuanza mkakati wa kubomoa nyumba za zamani na kujenga Maflay ambayo yangeweza kuweka wafanyakazi wengi zaidi na kutengeneza mazingira ya maeneo hayo, na pale wafanyakazi wa serikali wakiamua kuka katika nyumba zao, basi hizoi nyumba zingepangishwa kwa mtu yoyote, mradi pesa ya muhusika, kuhusu viongozi wanao stahili nyumba za serikali kutokana na nafasi zao basi wangelazimishwa kuka katika nyumba stahili ambazo zinamilikiwa na serikali, kama Mkuu wa jeshi, polisi, Mkuu wa Chuo Kikuu, Spika, Raisi , makamu wa Raisi, Waziri Mkuu etc au wafanye study wa nchi zingine wanavyo wapatia nyumba viongozi husika, au hiyo housing allowance. Na kwa kweli kiongozi atakaye shinda uchaguzi mwaka 2010 itabidi afanye mkakati huo wa kuona njia iliyo bora ya serikali kuwa na nyumba stahili kwa baadhi ya watumishi wake au ndio system ya Chuo kikuu ya Housing allowance ya 1m ni ipi inafaa? kuwapa mtaji zaidi hao government agency au tupeane mkononi kila mtu akajenge nyumba yake kwa kutumia hiyo housing allowance.
 
Nderemo na Ukwasi wa Misaada!
Sasa akimaliza mda, kwa vile ni mstaafu(bado atakuwa na hadhi fulani ya kipaza sauti)
Hatoweza kwenda chini ya hapo...Unakubali?

Kichwa cha Habari in faiv iaz

'SPIKA ANUNULIWA NYUMBA YENYE HADHI'
  • Alipiwa '$459,000' sic
  • Aachiwa Benzi lake la Kifahari!

Yangu mimacho(see avatar)
 
Haijawahi kutokea na haitatokea kwingine,hizi ni harakati za kampeni.CCM DAIMA DUMU!!
 
Back
Top Bottom