Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Duh Jamani nchi yetu ni balaa tupu maana hakuna hata kiongozi msafi hata mmoja, mara baada ya upepo kugeuka wamekuwa wanasema ni majemedari wa kivita vya ufisadi kumbe nao ni wapo
 
jamani hizi data zinatisha kama za kweli.na ndio hivyo raia tuko powerless na najua waswahili walisema "zimwi likujualo alikuli likakwisha" .jamaa wanajitesea sana sisi wananchi na bado nina imani mwenyezi mungu atawalaani mmoja baada mmoja.
 
heheheeh hata Yo Yo hula kona kupima Ngoma...acheni bwana kama mzee huwa anauza mechi inaonyesha!


Jamii forum- Home of creative thinkers - Is this what it means. I think we are loosing direction and it is also unfair for other members
 
Hizi kashfa kuwa na hawala sio tatizo kwa wa Africa haswa watanzania, lakini suala ambalo Spika akiwa kama mwanasheria mzuri ni kuruhusu hao hawala zake kutumia resource za office yake na za serkali, kama hili ni kweli inabidi lichukuliwe hatua, matumizai yake binafsi kikazi nje na ndani ya nchi si kitu kutokana na hadhi yake na hata suala la matibabu yake binasfi sio ishu...mimi nina sense suala la kuchafuana hapa kama msingi wa hoja hii.
Ujumbe wangu kwa Spika Sitta ni kwamba ajue tumempa heshima kubwa na ni katika watu ambao tunawaamini sana katika uongozi wa nchi yetu na tunaVYODHANI yeye ni katika wale wanaOPINGA ufisadi kwa vitendo, kama alivyoonyesha hisia zake siku raisi alipohutubia bunge...asiyumbishwe na hili na kama anaweza kujisafisha katika tuhuma hizo afanye ili jamii iendelee kumuamini.
binafsi nafurahishwa na jinsi anavyojitahidi kuliendesha bunge japo wakati mwingine nguvu za chama tawala zinamuelea, anatoa nafasi kwa hoja za wapinzani ambao wamekuwa wakiipa wakati mgumu serikali....

Mungu Ibariki Tanzania na Walaaani wasiopenda amani ya nchi yetu...
 
Ikiwa huyu jamaa alotoa hizi tuhuma ana ushahidi wa aliyoyaongea, amwage humu, hii itakuwa si kashfa bali ni kasheshe la mwaka! kama ya kweli basi Six asulubiwe hata kwa maandamano na kama amezuliwa basi huyu aliyezuwa asulubiwe ipasavyo.
 
Nififikiria viongozi wa Taifa inabidi wawe mifano kwa jamii ya watanzania kwanzia katika uongozi, ufamilia na pia uaminifu?

Ila kutokana na comments za watu hapa naona watanzania tunakubali kwamba viongozi wetu kuwa na vimada ni jambo la kawaida? Hivi kweli Ukimwi utaisha kwa namna hii?

Nilikuwa nafikiria Jamii Forum ni ya watu tunayotaka kubadirisha jamii ya watanzania kwanzia kwenye Nyanja ya siasa mpaka maisha bora ya familia. Maana you cant have a vigorous nation without strong family values!!!
 
Kama habari hizo zina ukweli basi Tanzania tutakuwa kwenye matatizo makubwa kwani kumpata kiongozi mwenye uchungu na nchi, asiye mwizi itakuwa kazi kweli kweli.
 
article-0-05762251000005DC-300_233x352.jpg


Pika mpya wa UK ambaye kikadi ni conservative lakini kimrengo ni Labour wa kutupwa

sisi bado tunaendelea kuleawetu ambaye sasa ana escort kubwa kuliko makamo wa rais wa Tanzania

Kisa kanyimwa u PM
 
article-0-05762251000005DC-300_233x352.jpg


Pika mpya wa UK ambaye kikadi ni conservative lakini kimrengo ni Labour wa kutupwa

sisi bado tunaendelea kuleawetu ambaye sasa ana escort kubwa kuliko makamo wa rais wa Tanzania

Kisa kanyimwa u PM

Hey! yamekuwa haya!
 
IMEBAINIKA kuwa, Ofisi ya Bunge imetumia vibaya mamilioni ya shilingi yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2007/2008.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika mahojiano yao na Tanzania Daima Jumatano yaliyofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma kwa wakati tofauti.
Wakizungumza kwa sharti la majina yao kutoandikwa gazetini, kwa kile walichoeleza kuwa ni kuogopa kuandamwa na baadhi ya wabunge wenzao, walisema ushahidi wa maelezo yao umo katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CGA) ya mwaka wa fedha wa 2007/2008.
Mmoja wa wabunge hao alieleza kuwa licha ya ripoti ya CGA kubainisha matumizi mabaya ya mamilioni ya fedha katika Ofisi ya Bunge, Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo, alizuia kujadiliwa kwa ripoti hiyo baada ya kushauriana na baadhi ya vigogo wa Ofisi ya Bunge, jambo ambalo linazuia kuchukuliwa hatua zozote za kisheria au kurekebisha hali hiyo hadi sasa.
Alisema Ofisi ya Bunge imekuwa ikifanya jitihada za makusudi kuhakikisha ripoti hiyo haijadiliwi na PAC, kwa hofu kwamba inaweza kusababisha baadhi ya watendaji kuwajibishwa na baadhi ya wanasiasa kuchafuka majina yao.
Cheyo, Mwenyekiti wa PAC na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alipoulizwa na gazeti hili kuhusu madai hayo, alisema ni kweli ripoti ya CAG kuhusu matumizi ya fedha za serikali katika Ofisi ya Bunge si nzuri, kwa sababu inaonyesha upungufu mkubwa wa urejeshaji masufuru pamoja na matumuzi mengine mabaya ya fedha za ofisi hiyo.
Hata hivyo, alikana kuikalia ripoti hiyo kwa namna yoyote na kueleza kuwa, aliamua kuiweka pembeni baada ya kushauriana na kukubaliana na wajumbe wote wa kamati hiyo kuwa hawawezi kuijadili, kwa sababu walishindwa kumhoji Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, ambaye wakati kamati hiyo akikutana kujadili ripoti mbalimbali za CGA kuhusu hesabu za taasisi za serikali, alikuwa hajaapishwa na rais kushika wadhifa huo.
“Ni kweli ripoti ya CAG kuhusu matumuzi ya fedha katika Ofisi ya Bunge si nzuri, inaonyesha upungufu mkubwa katika urejeshaji wa masurufu, na ripoti zote ambazo zinaonyesha hivyo kihasibu huwa ni mbaya. Sasa kwa Spika hii si nzuri, inamtia doa, anaweza asiaminike tena iwapo itawekwa wazi, kwa sababu ataonekana hafanani na kauli zake.
“Siyasemi haya kwa sababu nina kisasi na Spika, bali ni kwa sababu umeniuliza. Unajua Spika amenijeruhi hivi karibuni, sasa sitaki nionekana kama ninalipa kisasi. Lakini ukweli unabaki pale pale kwa sababu umeandikwa vitabuni kuwa kuna kasoro katika Ofisi ya Bunge ambayo inasimamiwa na Spika,” alisema Cheyo.
Spika Sitta alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Cheyo, alisema hahusiki kwa namna yoyote na uchukuaji wa masurufu, hivyo hapaswi kunyooshewa kidole iwapo imebainika kuwapo kwa kasoro zozote za matumuzi mabaya ya fedha za serikali katika ofisi yake.
Spika alisema taratibu ziko wazi kuwa wanaochukua masufuru kwa ajili yake ni wasaidizi wake
 
“Mimi sihusiki kuchukua masurufu, wanaohusika ni wasaidizi wangu, sasa kama kuna kasoro, wao ndio wanajua. Nina ofisi yangu binafsi kama viongozi wengine wakuu wa kitaifa, sitembei na fedha mfukoni, wasaidizi wangu wa ofisi hiyo ndio wanaoniandalia safari na ziara zangu zote. Wao ndio wanaonilipia kila kitu, walinzi, maradhi, kila kitu, ndio wanaochukua fedha za masurufu kwa niaba yangu,” alisema Spika Sitta.
Alipoulizwa kuhusu madai kuwa alitumia fedha nyingi za Ofisi ya Bunge kugharamia vikao na tafrija zilizokuwa zikifanyikia nyumbani kwake wakati mkewe, Margaret Sitta, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akiwania nafasi ya kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), alisema madai hayo inabidi yafafanuliwe.
“Ninachokijua mimi kuhusu hili, ni kweli kulikuwa na vitu vya aina hiyo wakati huo, lakini ninachokumbuka ni kwamba gharama nyingi za mikusanyiko hiyo nilikuwa ninatumia fedha zangu za mfukoni, nilikuwa nalipa mwenyewe. Lakini hili ili nilielewe vizuri, inabidi lifafanuliwe,” alisema.
Naye Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alisema hawezi kuzungumza jambo hilo, kwa sababu alipoingia katika wadhifa huo alikuta hali hiyo imeshatokea.
Alibainisha kuwa ni kweli hakuhojiwa na Kamati ya PAC kwa sababu alikuwa hajaapishwa na rais, lakini kwa sasa kamati hiyo inaweza kuendelea na kazi zake kama kawaida, bila kupata kipingamizi kutoka kwa mtu yeyote.
“Mimi nilipoingia katika ofisi hii, hali hiyo niliikuta, hivyo siwezi kusema kitu, kwa sababu sikuwapo, siwezi kuizungumzia. Ninachoweza kukitolea maelezo ni kile ambacho kimefanyika wakati wa kipindi changu.
“Lakini suala la ripoti hiyo kukaliwa halipo, PAC ikitaka kukaa kuijadili hata kesho ni sawa tu, hakuna tatizo, waje wakae, wao wana ratiba zao za vikao, kuna ripoti nyingi tu hazijajadiliwa, hizi hazijakaliwa, naomba kwa sababu linahusu Ofisi ya Spika, isichukuliwe kuwa linazimwa,” alisema Dk. Kashililah.
Ripoti ya CAG, ambayo Tanzania Daima Jumatano imeiona, katika ukurasa wake wa 43, fungu la 42, inaitaja Ofisi ya Bunge katika orodha ya taasisi za serikali zilizopewa hati zenye shaka, kwa kukiuka taratibu za kihasibu.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa Ofisi ya Bunge ilifanya malipo ya matibabu nje ya nchi ya zaidi ya sh milioni 101 bila kuidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, uhamisho wa fedha wa zaidi ya sh milioni 63 kutoka kifungu kimoja kwenda kingine bila kibali na malipo yenye thamani ya sh milioni 7.8 yalifanyika bila kibali.
Upungufu mwingine uliotajwa katika ripoti hiyo ni malipo yenye nyaraka pungufu ya sh milioni 526, malipo yasiyo halali ya sh milioni 102.5, malipo yenye shaka ya sh milioni 63.9, mishahara isiyolipwa na ambayo haikurejeshwa Hazina sh milioni 17.1, sh milioni 3.4 za mishahara ya watumishi walioachishwa kazi inayoendelea kulipwa kwenye akaunti zao benki na usuluhisho wa tofauti ya sh milioni 1.1 kati ya bakaa ya benki na bakaa inayoonyeshwa katika daftari la mapato na matumizi haukufanyika.
Marekebisho yasiyostahili yaliyojumuishwa kwenye hundi ambazo hazijawasilishwa benki ni sh milioni tano, masurufu maalumu ya sh milioni 50.2
 
habari hiyo ambayo imetoka kwenye gazeti la tanzania daima la jana ni vita binafsi ya mwandishi some body kilinda na spika sitta na its known.kuhusu ripoti ya CAG imetolewa tangu mwezi april na it is a public document so jamaa ndo jana kaitoa as if ni ishu kubwa recently huo ndo ukanjanja wenyewe.
 
habari hiyo ambayo imetoka kwenye gazeti la tanzania daima la jana ni vita binafsi ya mwandishi some body kilinda na spika sitta na its known.kuhusu ripoti ya CAG imetolewa tangu mwezi april na it is a public document so jamaa ndo jana kaitoa as if ni ishu kubwa recently huo ndo ukanjanja wenyewe.

PHD;UKANJA KWA SABABU KATAJWA SITTA....EPA UNAJUA ILIPOTOKEA....???WACHA WAANDISHI WAWE HURU....TUWE WAZI KILA SEHEMU TUSIBAGUE MAFISADI FISADI NI FISADI....HATA IWEJE
 
Kwa ujumla, ofisi nyingi za serikali hukutwa na mapungufu makubwa tu ya hapa na pale. Lakini hili la Ofisi ya Bunge kuandikwa na Tanzania Daima ni mfululizo tu wa vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na akina RA na EL kutaka kulipa kisasi kwa Spika baada ya suala la Richmond. Hawa mafisadi wamegundua udhaifu wa wahariri wa Tanzania Daima hivyo wanawatumia ipasavyo! Jaribuni kufuatilia makala na maoni yao kuhusu Spika Sitta. Zinachefua, kwani unaona kabisa hawa watu wanatumiwa. Shame on you guys!-
 
Kila mtu sasa hivi anataka aajiriwe serikalini au taasisi zake kwa sababu ya madudu yanayoendelea huko. Wakubwa wenyewe wanaongoza kwa kuitafuna serikali. Mzee Wassira alikuwa hoi kwelikweli kabla ya kuukwaa tena uwaziri hapo 2005. Sasa hivi pamoja na sura yake ilivyo anapendeza sana.
 
Ufisadi wa Spika Sitta naona ni mchezo wa mafisadi kwani ilishaongelewa na CAG. Sitta tuongozee Bunge la viwango waache mafisadi watapetape.
 
Kila mtu sasa hivi anataka aajiriwe serikalini au taasisi zake kwa sababu ya madudu yanayoendelea huko. Wakubwa wenyewe wanaongoza kwa kuitafuna serikali. Mzee Wassira alikuwa hoi kwelikweli kabla ya kuukwaa tena uwaziri hapo 2005. Sasa hivi pamoja na sura yake ilivyo anapendeza sana.
Hela ya RA hiyo.
 
Mimi hapo ninachojiuliza ni kwamba kwani huyo katibu wa bunge alipohapishwa imeonekana bado hastahili kuojiwa?Au ndo watatoa majibu yao mepesi kwa maswali magumu kama kawaida yao? Hawakawii kujibu kuwa wakati hayo yanafanyika hakuwepo. Binafsi naona hata isipojadiliwa bado spika anajulikana kua mara nyingi haendani na kauli zake.amekuwa kwa upande mkubwa mdhibiti wa mabomu yanayoelekea kulipuka na kuonyesha uozo kwa ujumla
 
Back
Top Bottom