Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,252
- 11,649
Wakuu sasa hapana tunamlaumu Sitta as a person au systme inayomruhusu Spika hata ukiwa wewe au mimi kukaa kwenye nyumba ya gharama hiyo. Kuna institutional corruption lazima tuikemee pia. Tatizo hakuna mwenye uwezo na hakuna mechanism ya kupambana na bunge as institution.
Hapa bwana Sitta ana lawama. Kwa nini yeye akubali kuishi kwenye nyumba ya bei kubwa kiasi hicho wakati Bunge linakabiliwa na ukata. Hao waliofanya mpango wa kuitafuta ama wanajikomba kwake au nao wana dili la nguvu. Kwa hiyo ni vizuri tukaijua hiyo hadhi ya Spika na gharama yake (in terms of monetary value) ili tujue kweli kama anastahili kula $8K kwa pango la nyumba (rent) kwa mwezi. Pia tuwekwe wazi hiyo nyumba ni mali ya nani na mchakato wa kuipata ulikuwaje? Ikiwezekana tuoneshwe nyumba yenyewe (kama kuna mtu ana photo atuwekee tafadhali). Vinginevyo jamaa wamechonga dili la kupata pesa ili Mzee asiukose ubunge 2010 au akalazimika kulamba viatu vya RA. Hiyo bei naamini inashindana na zile za DC au NY wakati mji wenyewe ni Dom. Nitakuwa mtu wa mwisho au kiazi kuamini kuwa hili suala ni kweli (it's real) na si ulaji mwingine wa kufyonza besi za umma kiulaini.
Ila hili la mhasibi kihiyo kufanya kazi za bunge nalo ni hatari. Mhhh, Bongo Dar ni kila mahali!!