Ni sawa dalali kufanya kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?

naomba kupata Uelewa kuna jamaa mmoja ni dalali wa magari na mambo kama hayo ila anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkow fulani hivi hii iko sawa! ????
Kwa taratibu na sheria za kazi si sahihi kabisa! Kibongobongo na kula kwa urefu wa kamba haina noma kabisa
 
Kama haiathiri ratiba za mwajiri wake ama haiingiliani kimaslahi na masuala ya mwajiri wake sidhani kama kuna tatizo. Hiyo ni kazi ya ziada acha ajiongezee kipato
 
Sioni tatizo ukizingatia ofisi zenyewe ndo hizo watu wanastaafu wakiwa hawana kitu, au hutaki mwenzako apate hela
 
naomba kupata Uelewa kuna jamaa mmoja ni dalali wa magari na mambo kama hayo ila anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkow fulani hivi hii iko sawa! ????
Hujaeleweka mkuu.

Yaani jamaa anafanya kazi kwa mkuu wa mkoa ila baadae akiwa nje ya ofisi anafanya kazi ya udalali?

Au ni dalali ila kazi hiyo anaifanyia kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa? (Kwamba amepanga chumba hapo au anakaa kabisa ofisi ya mkuu wa mkoa akifanya shughuli zake za udalali?

Kama suala ni ishu ya kwanza. Ni sahihi kwa mtumishi wa umma kuwa na kazi ya ngongeza nje ya kazi yake rasmi.
 
Kwa taratibu na sheria za kazi si sahihi kabisa! Kibongobongo na kula kwa urefu wa kamba haina noma kabisa
Brother mshana msome vizuri alichokiandika hapo then mjibu

Now day udalali umebadilika hasa huo wa magari kuna watu walimu wa vyuo na hata wafanyakazi wa serikali hata ma bank.

Wanafanya kazi hii ya udalali unakuta mfanyakazi mwenzenu ofisini kila mwezi anabadilisha hata gari tano anauza na kununua,akitaka gari anatafuta madalali wamtafutie gari anarekebisha then hao hao wanamsaidia kumletea wateja.

Kwangu mimi hapo sijaona kosa sababu hata nikiwa mfanyakazi wa serikali au hata hazina ni kosa kisheria kumsaidia boss wangu kupata mteja wa gari yake au sheria inanifunga kukagulisha gari yangu na kuuza ofisini?
 
naomba kupata Uelewa kuna jamaa mmoja ni dalali wa magari na mambo kama hayo ila anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkow fulani hivi hii iko sawa! ????
Hakuna ubaya endapo anafanya udalali baada ya muda wa kazi wa serikali kuisha. Mbona wapo wanaofanya kazi kama, boda boda
 
Ndivyo inavyotakiwa kuliko kuiba fedha za umma, ni sawa na wewe umeajiriwa huku unafuga kuku uuze mayai ili ujiongezee kipato.
 
Julio ni kocha wa mpira ligi kuu halafu ni dalali wa Magari pale kisuma Bar.So mkuu usichukulie ule udalali wako wa kizamani now day's watu wako smart sana.
 
Sema ni mstari mwembamba sana unamtenganisha Dalali na Tapeli...,
Kua dalali kunakaribisha janja janja, Uongo, ambavyo ni vitu tofauti na utumishi....
Otherwise SIONI kosa.
 
Back
Top Bottom