Kila Changamoto ni Fursa, Dalali mkuu nakurahisishia mahitaji yako

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,487
2,739
SHALLOM WANABODI

Ajira imekuwa changamoto sana kupatikana bila kuwa na Connection au Bahati kama ilivyo kwa wengi.

Niliamua kufanya kazi ya udalali ambayo naona kwa kiasi kikubwa inalipa Japo unaweza kukaa mwezi mzima hujapiga dili la maana zaidi ya kupata dili ndogo ndogo za Elfu kumi, ishirini na kuendelea japo kuna muda unapiga dili hata la 5M ila hutokea kwa nadra sana

Mtaani ni kugumu asikuambie mtu yaani asubuhi unaamka alafu hujui uanzie wapi uende kijiweni au ubaki home usikilizie simu ya mteja au uende kwenye kijiwe cha magazeti ukabishane mambo ya mpira

Kwa hiyo wakuu nipo hapa ukihitaji Kuuza Bidhaa yako au kama kuna bidhaa unahitaji usisiste kunitafuta

.Ukihitaji Kiwanja,nyumba,chumba. fremu nicheki tu kwa haraka

Ukihitaji kuuza Bidhaa za sokoni au kufahamu bei ya bidhaa sokoni (mabibo na Ilala)

Ukihitaji nikusafirishie mzigo wako kwenda Mkoa wowote hapa Tanzania

Ukihitaji nikusaidie kufuatilia mambo yako labda upo Mkoani unataka nikusaidie kufuata barua zako posta kupeleka taaisis fulani n.k (Kama anavyofanya Dodoma Mesenger)

Hizi ndio kazi kwa sasa nafanya

Angalizo kuna watu wanakuomba umsaidie kuulizia kitu fulani au kumtafutia wakala wa huduma au bidhaa fulani ukishamuunganisha na yule mtu basi wakimaliza biashara hakutoi hata mia inabidi sasa nianze kuweka na service chaji ukihitaji mawasiliano ya wakala,soko au taasisi fulani ulipie ili kuondoa usumbufu

KARIBUNI WADAU NAMBA YANGU SITAWEKA HAPA MAANA KUNA WATU WAPO HUKU KUTAKA KUJUA TAARIFA BINAFSI ZA WATU, HIVYO NAMBA NITAITOA TU KWA MTEJA AMBAYE ATAKUWA ANA UHITAJI
 
Leta gari iliyonyooka ya milioni mbili unusu kuna mwanakijiji kapata hela ya viazi anataka gari la hiyo bei , ilete hapa posho juu yake .

kwa hiyo bei mshauri ajaribu kutafuta pikipiki aanze biashara ya bodaboda inaweza ikamlipa. Gari ya 2.5M labda kama anataka kujifunza ufundi wa magari
 
Yupo tayari kuwa fundi , maana yeye raha yake hata kama haiwaki anataka aiweke juu ya mlima akae ishuke huku amekaa ameshika usukani kikubwa liwe na brake tu😀😀
 
Back
Top Bottom