Ni sahihi Rais kuponda vyuo vingine?

Ni sahihi Rais kuponda vyuo vingine?

Je ni vizuri rais baba wa wote kuviponda vyuo vingine ambavyo ni nje ya Dar es salaam, je sisi tuliokuwa na sifa then tukapata nafasi ya kusoma chuo kingine tutajisikiaje, au ndo tujione matabu darasa, kiukweli hakukuwa na haja ya kuongelea vyuo vingine akiwa kama baba watoto wote ni wake anatakiwa atusapoti mi nimejisikia vibaya nimeona kama cheti changu hakina maana kwa sasa kama mkuu wa nchi hakitambui.
Mkuu umeandika matabu darasa,je,ulikusudia kuandika ma tabularasa au?
 
Asee kuna vyuo kama Udom,st John,Rucu,ni majanga mnoo!Wanatoa graduates kwa baadhi ya kada ni maboya sana!Halafu hawa hawa ndio wanaaminiwa na kupewa nafasi za kufanya maamuzi makubwa katika wizara mbali mbali!Futa ama rekebisheni maana mnaaibisha sana elimu ya Tanzania
Sasa unataka wote tusome UDSM, mbona wasomi wa sasa mmekuwa wendawazimu kiasi hicho, ulishawai fanya tafiti kugundua uboya wao acheni fikra nyepesi
 
Tuna kila sababu ya kupimwa IQ zetu tuliosoma nje ya UD na waliosoma UD, kwani ni jambo la kijinga kuona wanaoitwa wasomi kuanza kubishana na kukejeli juu ya vyuo tofauti na UD. Ifahamike kuwa dereva mzuri ni yule anaeendesha sio yule aliye na leseni. Endeleeni na wendawazimu wenu wa kisomi
 
hii topic Salary Slip angeandika "Si sahihi Raisi kuponda vyuo vingine"
 
Ujue hilo ni swali rahisi sana,, pale unapojiuliza inakuaje mtu katumia more than 7 years in learning using the medium of commnctn ambayo bado inampa shida even to state a correct single sentence in English??? Ni uboya wa mtu au walo mtrain wameshindwa???
Mkuu hata wewe hicho kiingereza chako kidogo ulichochomekea hapo kinaonesha cha wasiwasi jasho jingi. Sio kilaini kama ute wa yai.
 
Ni kweli si vyema wala si busara!

Suluhisho:
Wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini nawashauri wavamie (waamie) UDSM ili mkuu awatambue kuwa nao ni wasomi.

Nyongeza:
Ndivyo alivyo! Umieni kidogo tu si sana!
 
Hivi vyuo vikuu vinatakiwa vifanyiwe uhakiki vile ambavyo havikidhi viwango vifutwe kuliko Rais kuishia kuvisema tuu mama professor Ndalichako najua umetake note

Kwani vyuo huwa vinaanzishwa bila kufata taratibu za uanzishwaji hadi visikidhi vigezo
 
1. Kauli ya Mh. Raisii na madhara nakubwa sana, tena sana!! Inadumaza uboreshwaji a vyuo vikuu binafsi.
2. Jee mwekezaji gani atakuwa tayari kuja kuwekeza kwente Elimu ya juu? Mfano kujenga chuo kikuu hadhi ya John Hopkins. Wawekezaji wana kila sababu za msingi kutokuja au kuboresha uwekezaji wao wao Tz.
3. Kwa kauli ile, serikali inaweza kila kitu. Je wafabyakazi ns wanafunzi wa vyuo vya binafsi wanakuwa katika mazingira gani?
4. Mkuu anashughulika na mambo sensitive kizamani. Ndio maana zinaundea tune mbili mbili, ...
5. TCU ina mapungufu makubwa sana!
 
Mkuu kazungumzia tcu, nacte inakuwaje? Zile elfu 30 za udahili inakuwaje?
 
Sasa kingereza c tumedandia tuu cyo lugha yetuu hiyo cyo point tafuta kinginee badala tukikuze kiswahili we unasema English
Tumedandia sawa lakn yeye kasoma kupitia hiyohiyo lugha tuliyoidandia na akafaulu kupitia lugha hiyohiyo lakn inamgogoro kwa upande wake sasa swali alifaulu vp...??
 
In short rais wetu is not fair to all his children. Anajisahau sahau sana hajitambui kuwa yeye ni baba wa wote
 
Mimi nilitoka hapo ila aibu inakuja pale tunapoona kuna PhD ilianzia hapo lakini lugha ya English ni mgogoro
mkuu mbona umebadilisha Ile Avatar picha yako sheikh babu ukaweka hii ya ajab?
 
Nadhani huko sahihi kabisa. Kwanza italeta picha nzuri kama rais ataiamini na kuiachia suala hili mamlaka husika (TCU). Na kama kuna jambo ambalo rais hafurahishwi nalo, ni vema akapata/kutoa maelekezo ya moja kwa moja kwa TCU. Kwa hali ilivyo sasa ni kama kutuchanganya tu wananchi!
Like father like son, Bashite is a son of Sizonje.....what do you expect!!!!!
 
Back
Top Bottom