Ni sahihi Rais kuponda vyuo vingine?

Ni sahihi Rais kuponda vyuo vingine?

Kw
Nadhani huko sahihi kabisa. Kwanza italeta picha nzuri kama rais ataiamini na kuiachia suala hili mamlaka husika (TCU). Na kama kuna jambo ambalo rais hafurahishwi nalo, ni vema akapata/kutoa maelekezo ya moja kwa moja kwa TCU. Kwa hali ilivyo sasa ni kama kutuchanganya tu wananchi!
Kwani yeye anajua kila kitu? Unataka kuniambia TCU na NACTE ambao ndio wanao coordinate ubora wa elimu inayotolewa na vyuo na kisha kutoa ithibati hawajui wanachofanya? Pole, sna wewe unayekatishwa tamaa na tamko la jukwaani. Chuo kinapokuwa na ithibati kinatambulika na mamlaka inayoratibu ubora wa elimu katika nchi husika. Wewe unavunjika moyo kwa kuwa hujasoma udsm? Ndio nini sasa? au kwakuwa kiranja ametamka sijui nini? Japo mimi sijui alitamka nini. Hii ndio imetufanya watanzania tufike hapa tulipofika. Miaka ya themanini na tisini mwanzoni, mtu amefaulu kusoma chuo kikuu unaambiwa nafasi zimejaa. Nchi za wenzetu walianza mfumo wa distance learning muda mrefu na sisi tukabakia kurudia mitihani ili uende udsm, maskini wtz. Soma kijana, soma popote utakapo pata udahili, achana na inferiority complex ya kutokusoma udsm.
 
serikali inayofanya biashara haiwezi pia kuangalia maslahi ya wananchi wake,hicho chuo anachokiponda kimesajiliwa na NACTE,na VETA vyombo muhimu vya seikali ila chuo hicho hicho unaambiwa ni cha mtaani,kama kungekua na nia ya dhati ya serikali kuangalia ubora wa elimu kwa watu ingekua mapema hivi vyuo hata kabla ya usajili inavifutilia mbali juu kwa juu ila kwa kuwa serikali inataka pesa za wenye hivyo vyuo matokeo yake ndio haya mkuu anavikanyagia majukwaani,hivi seikali ina uwingi wa vyuo kufanya watu wote wakasome huko? kwa nini kusiwe na chombo cha kuangalia hivi vyuo ubora wake ili wanachi waondokane na hii hadha?
 
Umekwishasema English medium ambako mtoto anaanza kufundishwa kingereza tangu akiwa mtoto hivyo kuwa rahisi kwake kuwa vizuri kwenye lugha hiyo!

Ambao hatujasoma englishi medium kingereza tunakitumia tu kwenye masomo ambapo kujua inategemea zaidi unasoma masomo gani. Sio rahisi sana mtu anayesoma sayansi kujua kingereza kwa kiwango unachotaka wewe.

Kumbuka kingereza cha kuongea na cha darasani/kujifunzia viko tofauti mkuu
Mjomba m cmnang rais. Naongea ukweli, Binafsi ningeona Aibu.
Kuna watu wapo ikulu, wamsaidie rais. Nakumbuka hata jk alikuwa na shida ya kiingereza.

Our president is highly efficient.
 
Mjomba m cmnang rais. Naongea ukweli, Binafsi ningeona Aibu.
Kuna watu wapo ikulu, wamsaidie rais. Nakumbuka hata jk alikuwa na shida ya kiingereza.

Our president is highly efficient.
Unaona aibu mtu kushindwa kuongea lugha ambayo sio yake?

Mataifa mangapi maraisi wao anaongea lugha zao?
 
udsm imetoa mtu aina yake ambaye ana phD na kingereza kinamshinda ilihali alijifunza kwa kingereza na akafauli.binafsi sishangai yeye kuponda vyuo vingine
mimi nimekuelewa. ila acha uchochezi[emoji2]
 
Mimi nilimuelewa vizuri sana kuwa TCU iwape wanafunzi first priority chuo alichochagua badala ya kuwakimbuzia vyuo vya private hajakichagua hapo hapo alichochagua hakijajaa na sifa ya kuingia pale anazo.... tuwege na fadhila sometimes kosa lake liko wapi hapo sasa anawatetea watoto wetu halafu tunafurukuta
kama ni hivyo yuko sahihi, tcu ni wahuni wanashirikiana na baadhi ya vyuo kupiga pesa
 
Mkuu hata wewe hicho kiingereza chako kidogo ulichochomekea hapo kinaonesha cha wasiwasi jasho jingi. Sio kilaini kama ute wa yai.

toa correction,, zozote zile,, grammer or whatever,,!!
and mind you,, we speak not the formal language,, but am sure ain't wrong
 
toa correction,, zozote zile,, grammer or whatever,,!!
and mind you,, we speak not the formal language,, but am sure ain't wrong
Jamani kama uzi umekuja kwa kiswahili tujibu kwa kiswahili, kha!! Hadi mnatuchanganya sisi wakongo man. "but am sure ain't wrong" ubarikiwe.
 
Mimi nilitoka hapo ila aibu inakuja pale tunapoona kuna PhD ilianzia hapo lakini lugha ya English ni mgogoro
Aibu sana kwa kuviponda vyuo vingine wakati yy ametokea udsm na hajui hata lugha ya kiingereza na masomo yote amesoma kwa lugha hiyo ina maana alifoji cheti au ndio kibashite bashite
 
Kile chuo kikuu cha Bukoba kinaitwaje?
 
Nadhani hakuna haja ya kujali sana. Kikubwa fanyia kazi Elimu yako. Suala si kusoma udsm bali ubora wa unachokipata popote unaposoma.

Vyuo hutofautiana duniani kote. Vyuo vilivyoko Uingereza Havina ubora sawa. Marekani hali kadhalika sembuse vyuo vya Tanzania!!

Wenye akili waliruhusu vyuo vianze ili taratibu vikue na kuwa miongoni mwa vyuo bora. Pia ni nafasi ya ajira nchini. Vyuo hutoa fursa kubwa na nyingi za ajira na hivyo kupunguza kelele za uhaba wa ajira.

Leo tunalilia Tanzania ya viwanda lkn hapo hapo tunataka kufunga vyuo. Hiyo udsm yenyewe miaka yake ya kutembea dede haikuwa ilivyo sasa. Cha maana ni kuhakikisha vyuo vinatoa Elimu bora kabisa. Viwanda vinahitaji wasomi.

Watu wanakuwa wachache siyo tu kwa ile michezo aliyoisema. Nayo kama IPO tunaikemea kwa nguvu zote. Huo ni uhuni wa hali ya juu na hauwezi kuvumilika.

Lkn sababu nyingine ni kukosa Mikopo. Nawafaham vijana zaidi ya kumi ambao wameahirisha masomo mwaka huu kisa hawajapata mkopo. Hili jambo liangaliwe vizuri.
 
Back
Top Bottom