Jamii hali ni mbayaa katika malezi ya watoto

idiomer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
269
Reaction score
317
Naandika Barua ndefu yenye mawanda mapana kwetu wanajamii.
________________________ MWANAJAMII
JAMII
S.L.P TANZANIA
26-10-2026

Ndg. YAH: SALAMU KWA WANAJAMII WENZANGU

Natumaini wote wazima wa afya. Pia kwa wenye changamoto ya afya au uchumi ni ombi langu Mwenyezi Mungu ajibu maombi yenu.

Kabla ya kuendelea dhumuni la barua hii nianze kwa kukumbusha maana ya Jamii.

Jamii ni kundi la watu wanaoishi pamoja katika eneo fulani au wanaounganishwa na mambo yanayofanana, kama vile lugha, utamaduni, mila, desturi, shughuli za kiuchumi au malengo ya pamoja. (Mfano DIRA 2050)

Pia nikumbushie malezi.

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataicha hata atakapokuwa mzee.
[ Mithali 22:6]

Pia, jukumu la malezi ni la jamii ambapo mtoto ndio hushinda. Jamii inajumuisha mama na baba yake.

Malezi ni mchakato wa kumlea, kumfundisha na kumwongoza mtoto au mtu mwingine ili aweze kukua kimwili, kiakili, kihisia, kijamii na kimaadili, na kuwa mwanajamii mwenye tabia na mwenendo unaokubalika. Kama haitoshi kuna taasisi zilianzishwa kusaidia kuongezea pale jamii ilipoishia na kuwaandaa watu kwa kazi kitaaluma na kuongezea tuu kidogo pale jamii ilipoishia. Taasisi hizi ni za kielimu yaani shule.

Shule ni taasisi rasmi ya elimu inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza maarifa, ujuzi, stadi, maadili na tabia zinazowawezesha kukabiliana na changamoto za maisha na kuchangia maendeleo ya jamii.

Cha ajabu shule badala ya kuongezea zimebeba mzigo wa kufuta matusi, kiburi, uvivu, na tabia mbaya ambazo mtoto hufunza na jamii. Hali ni mbayaaaa anasema Godfrey Tumaini ali maarufu kama "dudu baya"

Watu wengi kwenye jamii ni kawaida yetu kufurahi pale tunapopata mafanikio. Mfano kuongeza umri, watu baadhi hufanya sherehe na kufurahi. Hali kadhalika kumaliza ngazi fulani ya elimu.

Hivyo ni dhahiri wanafunzi kuwa na furaha baada ya kumaliza elimu tena kwa ngazi muhimu. Elimu ya kidato cha nne.

Hapo miaka ya nyuma vijana wa zamani walikua na mtindo wao wa kusherehekea.

Kwa sasa pia mabinti wale wameonesha namna yao ya kufurahia.

Pia kusema depo jipya...Hi kwa vyuo vikuu utasikia container jipya limeingia hivyo ni shangwe kwa wale wanaopenda kubanjuka. Nakupa shida chini naruka juu.

Juma lilizopita ( 23-10-2026) wanafunzi wa kidato cha nne hasa wale wa mchepuo wa sanaa [ hawapendi hesabu] walionekana wanafurahi baada ya kumaliza mtihani wa mwisho kwa mchepuo huo ( Historia).

Hapa kilichooneekana kuchukiza wengi mitandaoni ni lugha mbaya ya matusi iliyotolewa na watoto hao. ( ficheni wanaume zenu).

Kwa haraka niliona Waziri mwenye dhamana akitaka kujua shule na wazazi wa watoto wale. Kwa nafasi yake yupo sahihi sana.

Hii hatua nzuri ila ni kama kuzima moto bila kujua chanzo cha moto.

Ni kwanini moto unatokea? Nini kifanyike ili moto usitokee tena. Masoko na shule yamekua yakiungua mara kwa mara na tume kuundwa nyingiii.

Swali ni kwamba ni nini chanzo cha mtoto? Je ni mfumo mbaya wa umeme? Je ni chuki ? Tuichie TUME. "TAARIFA YA UPEMBUZI MAKINI ULIOTUMIA ELIMU"

Turudi shuleni watoto moja kwa moja wanatoka kwenye jamii. Jamii ina wazazi wao, na makundi ya kila aina. Pia utamaduni wa makabila takribani 120 kila moja likiwa na tamaduni zake.

Walichosema watoto kinaakisi yaliyomo kwenye jamii. Pia upungufu labda kwenye mitaala mfano " matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii"

Zaidi pia inachagiwa na wazazi wao. Je wajua kuna mzazi anajiuza na ana mwanafunzi kidato cha nne??

Twende kwenye uondo. Hapa wengi si wageni ndugu zangu labda kama mgeni Tz kuna ngoma kama baikoko, kanga moja ndembe ndembe, mtoto kuchezwa akibalehe na mambo mengine mengi.

Vuta kiti kaaa unaujua Mziki wa singeli? Umewahi sikiliza baadhi ya jumbe zake? Maudhui yake yameshakubalika na ilifika mahali Waziri mmoja alisikika akisema mziki huu uwe utambulisho kwa Tanzania.

Sijui aliwaza nini, Mwakilishi huyu wa Rais ila tuache hilo aliapa kumwakilisha vema.

Inashangaza sanaaaa!
Kitu anafanya mzazi akifanya mtoto hana maadili, sawa niache simu 2000 niwahi mihogo nikakaange nipate hela ya LUKU El Nino ipo katikati.

Kuna wasanii wanaimba matusi sanaaa na nyimbo hizo zina watazamaji wengi. Watazamaji ni wazazi, wale watoto, mimi na wewe.

Naogopa kukuumiza sana kichwa ndugu yangu, Je umesikia msanii yeyote amekemea au kusema lolote kuhusu watoto wale? Form 4 ya El niño.

Inawezekana wapo mimi sikiwa na bando nijuze sio mbaya ni vizuri kupashana habari. Kwani kuna wazazi pia hawajaona video ya watoto " depo jipya".
WALICHOSEMA WATOTO NI UWAKILISHI TU WA KIDOGO WALICHOJIFUNZA TOKA KWENYE JAMII.

HATUWEZI KUPONYA TAIFA KIMAADILI KWA MIHEMKO.

Hongereni mabinti kwa kumaliza elimu ya kidato cha nne. Ninaamini pia mtafaulu. Kila la kheri. Hakika mmeongeza moja ya hatua katika fanikio la DIRA 2050.

Karibuni mtaani muendelee kujifunza. Yapo mengiii hayo ni machache sasa hakuna pumziko, sheria pia kama shule wala homework muda ni mwingiiiiiiiii.

Dunia sinia pakua unavyoweza. See less
 
Nchi mmeuana kama wadudu, rais kasema nguvu iliyotumika ni sahihi, halafu kuna watu wanafikiri kwamba watoto wa nchi hiyo watakuwa sawa?

Na wanafikiri hawa watoto ndiyo tatizo hapo?

Ni hivi, mpaka tatizo kubwa linatokea watu wanauawa nchi nzima linatokea, hapo maana yake kuna matatizo madogo yametokea kwa muda mrefu yakaachiwa na kupuuzwa mpaka yakatengeneza hilo tatizo kubwa.

Hao watoto wamepiga kura ya kukosa imani kwenye maadili mnayohubiri.

Kisaikolojia hapo wamesema "fvck this fake modesty shit".

Tumemaliza shule, ajira hakuna, tutachukua mabwana zenu.

Ndiyo maisha wanayoyaona.
 
na bado hatujasema nchi imeingia unajisi. hatutakaa tuwe sawa tena mpaka tutakaposafisha unajisi katikati yetu. tumefungua milango na sasa unajisi upo katikati yetu. Ardhi inatuzalia mapooza sababu damu isiyo na hatia inalia kutoka ardhini. Yaani bado hatujasema vizuri, wakati unakuja sauti zitakuwa hazitoki , machozi yatakauka tutabaki kulia kwa kwikwi kama tusipofanya mapema yatupasayo kufanya.
 
Back
Top Bottom