Ni nini sababu ya binadamu kuletwa Duniani?

Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Tumeumbwa ili tuabudu.
 
Sasa wewe kwa akili yako unafikiri baada ya kuumbwa tulistahili kuwa wapi?
Tuwe sehemu salama yenye furaha ya milele na isiyo na maumivu ili kuleta maana zaidi ya kuishi
 
Usilazimishe kwamba chanzo kipo…… ndio maana binadamu wamemtengeneza Mungu na sayansi imetengeneza Nadharia kwasababu ya Kulazimisha lazima kuna chanzo.

HOJA ya kwamba kila kitu LAZIMA KINA CHANZO inatengeneza mnyororo usio na mwisho….. Ukipata chanzo cha binadamu ni kipi utataka kujua na hicho chanzo nini chanzo chake……

Binadamu ni kiumbe MDADISI…. Wala sio kosa kujiuliza

Ukweli tunao ujua ni kwamba tumejikuta tu tumezaliwa na tutakufa
Sawa mkuu
 
Yaani Mwenyezi Mungu (ALLAH A.S) ametuweka Duniani kutupima, watakaofaulu mtihani wa kutenda mema kama alivyoagiza ndio watakaofaulu kuingia peponi

Kwahiyo tupo katika Mchujo

Usiniukie kwa waliofariki wakiwa watoto wachanga au wadogo walipimwa vipi, kifupi wao wameshafaulu huo mtihani nahisi

🤣🤣🤣
😂😂😂🤝
 
HAITOSHI kabisaa
Mungu muweza wa yote anatengenezaje dunia lenye mabalaa yote haya na binadamu wa mfano wake wenye UKATILI usio elezeka?

Kili mshinda nini kuumba dunia yenye AMANI tu?
Hivi tunaposema katuumba kwa mfano wake inamaanisha sifa hizi tulizonazo binadamu yeye si anazo kama ukatiri, jeuri, chuki, dharau, wema, furaha n.k?
 
Exactly
 
Hukutengenezewa kama upungufu, ni zawadi, kwamba uwe na free will. changamoto tu ni kuwa will power haina mipaka, na unaweza ukafanya jambo hata kinyume na aliyekupa huo uwezo wa kuchagua. Hasa ndo kinachokutesa.

Hasira ya Mungu ipo kwasababu uliumbwa ukiwa mkamilifu. Kwa hiyo mapungufu uliyonayo ni ya kujitakia tu, ni kama unavyolea mtoto wako alaf afanye kitu tofauti na unavyo mwelekeza utakasirika
Swali lao ni kuwa kwanini Mungu akawawekea watu hali ya kuweza kuwa na udhaifu??? Halafu baadae anawahukumu kutokana na huo udhaifu?
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Tumtumikie Mungu tupate kufika naye mbinguni.. Rejea katekisimu Katoliki jimbo la Iringa.
 
Huo unaosemwa naona sio udhaifu bali ni Power.
Mfano. Mtu aliyeamua kumuua mwenzake; kwa haraka utaona ana nguvu na ameamua kuzitumia vibaya, kwahiyo atahukumiwa kifungo. Hapo hawezi sema ameua kwasababu ya udhaifu maana ni kitu kilicho ndani ya control yake

Kila sheria aliyoiweka Mungu, ipo ndani ya uwezo wa mwanadamu na maamuzi yake.

Swali: hivi unafikiri shetani aliasi kwasababu ya udhaifu au nguvu?
 
Huo ni udhaifu wa kushindwa kuzuia hasira. Hata Uzinzi ni udhaifu pia wa kushindwa kucontrol hisia....kuweza kustahimili hizo hisia ndio Uimara kiroho (In spiritual context)
 
Tumtumikie Mungu tupate kufika naye mbinguni.. Rejea katekisimu Katoliki jimbo la Iringa.
Yeye yuko wapi kwa sasa mpaka tufuatane naye hapo baadae?
 
Habari wanaJf
Nimekuwa nikijiuliza swali moja la msingi sana lakini majibu thabiti nimekuwa nikikosa kabisa...

Kwa wale wanaoamini kuhusu uwepo wa Mungu naomba wanijuze kwanini tumeletwa hapa duniani ambako tunaishi maisha mafupi na kupita, je Mungu hakuona namna nyingine ya kutufanya tufike huko kwenye maisha ya milele kunakosemwa na vitabu vyake bila kupitia hapa duniani kwenye shida na karaha?
Kulikuwa na haja ipi kutupitisha kwenye mateso hali ya kuwa ipo sehemu salama tunaelekea? ( Kwanini alitupitisha duniani?)

Hata wale wasioamini uwepo wa Mungu nao naomba wanisaidie kujua juu ya hili swali langu...kama hakuna maisha baada ya haya kwanini tupitishwe hii sehemu yenye taabu na mateso mengi tena kwenye maisha mafupi..kwanini tumetolewa huko tulikokuwa na kuletwa hapa duniani ambako kuishi kwetu ni muda mfupi na tisingebaki huko huko kama tulikuwa na maisha kabla?

Nini sababu ya sisi binadamu kuletwa/kupitishwa hapa duniani?
Ukisoma kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia utagundua kuwa alitupenda sana,na akatupa vitu vyote vizuri bali dhambi zetu ndio zilisababisha leo tunapitia tabu na haya mateso,lkn bado anatuwazia mema,something good is yet to come,keep on living the promises of God hautajutia kamwe...
 
Back
Top Bottom