Ni lini vyuo vyetu vya elimu ya juu vitakua chanzo cha mapato kwa Taifa kwa kusajili wanafunzi nje ya Tanzania?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Kumekua na ongezeko kubwa la vyuo vya elimu ya juu, tofauti na idadi tuliyokuwa nayo mpaka miaka ya 90. Licha ya elimu nje ya bara la Afrika, kuna waliobahatika kupata elimu ya juu katika nchi za Afrika hususan Makerere Uganda, Kenyata Kenya, Afrika ya Kusini, Nigeria, Misri, Botswana.

Hizi ni baadhi tu ya nchi zinazochukua kwa wingi wanafunzi kutoka nje ya nchi zao. Wanafunzi wanapokwenda kusoma huongeza pato la taifa kuanzia mishahara ya watumishi wa chuo na hata mzunguko wa pesa katika mahitaji yao ya kila siku.

Hiki kinaweze kuwa chanzo kungine cha mapato badala ya kumkamua mwanachi kwa ongezeko la kodi kila uchao.
 
Naunga mkono hoja.

Now, Sky Eclat , pretend you are a foreigner. And you want to apply for an undergraduate degree in a Tanzanian university. Does the university application portal accommodate you?

Sisi wa vyuo, hasa vya umma, na wadhibiti wetu, hilo unalolisema liko chini sana miongoni mwa vipaumbele vyetu.

Miaka fulani nilienda Naijeria. Katika mazungumzo baada ya habari, jamaa wakaniambia kuhusu kozi fulani inayotolewa hapa Tanzania, ambayo kule Naijeria, waombaji ni wengi kuliko nafasi zilizoko, na kwamba, sisi tukifanya promo kidogo tu, tutavutia baadhi ya hao kuja kusoma Tanzania.

Niliporudi TZ, jitihada za kushawishi chuo husika, hazikuweza kuzaa matunda yoyote, kwani zilikuwa brushed aside, na business went as usual.

Safari bado ndefu.
 
Kabla ya kutumia pesa nyingi kujenga majengo ya chuo haya ni mambo yanapaswa kufikiriwa kwanza. Ikiwezekana mnaangalia nchi iliyofanikiwa katika jambo hilo na kupeleka watu wachache kujifunza

Elimu ikiwa bora ni biashara inayo uzika mno duniani.
 
Back
Top Bottom