Global education link daraja kwa wanafunzi nje ya nchi

Apr 9, 2022
66
32


Global Education Link yawakaribisha Wanafunzi wa ngazi mbalimbali za Elimu ya juu kutembelea katika Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 18 ya vyuo vikuu nchini Yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jiji Dar es salaam ili kupata nafasi yakuunganishwa na Vyuo Vikuu mbalimbali Duniani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link Abdulmalik Mollel amewaomba wanafunzi na Taasisi zinazofadhili wanafunzi wanao kwenda kusoma nje ya Nchi, kufika kwenye banda la Global link na kuunganishwa na Vyuo Vikuu vyenye ubora na gharama nafuu.

"Wako wanafunzi, zipo Taasisi zinatamani kuwafadhili wanafunzi wa Tanzania, zinatamani kupata Vyuo vya gharama nafuu na hawajui watavipata wapi, wako wafanyakazi ambao wako maofisini wanahitaji kujiendekeza na Elimu ya juu lakini hawawezi kusafiri, wako na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu wanahitaji kuongeza maarifa yao kwenye upande PHD ama Master's ...,waje kwenye Vyuo Vikuu vya Milioni 3,4,5 ambavyo ni Affordable lakini vyenye quality ya juu ya Elimu. Amesema Molel.

Aidha amevihimiza Vyuo Vikuu vya Nchini Tanzania vinavyohitaji ushirikiano na Vyuo Vikuu vya Nje kwa kufanya kazi kwa pamoja, wawasiliane na Global link ilikuweza kuunganishwa na Vyuo hivyo moja kwa moja.

"Ikiwa kuna Chuo kitahitaji kupata Collaboration na Vyuo Vikuu vya nje eidha kuanza kufundisha Mitaala yetu ya Tanzania katika Vyuo vya Nje ama kuwakaribisha wenzetu kufanya kazi na Vyuo Vikuu vya Ndani waelewe kwamba Vyuo Vikuu 16 kutoka katika Nchi Nane Dunia vipo hapa kwenye mabanda ya Global Education Link,Jukumu langu kama mtanzania ni kusilmamia Vyuo Vikuu vya Ndani na vya Nje ili visaini makubaliano kwamaana MOU of understanding yenye tija". Amesema Abdulmalik.
 
Back
Top Bottom