Wanafunzi Waliodahiliwa Elimu ya Juu katika Vyuo Mbalimbali Daraja la Kwanza Kidato cha Sita Wapewe Mikopo

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,039
3,486
Wana Jamvi JF,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza niende moja kwa moja kwenye mada. Kabla ya mwaka 2023 wanafunzi waliokuwa wanafaulu kidato cha sita na kudahiliwa katika vyuo mbalimbali Tanzania pamoja na vigezo vya kusomea taaluma maalum za sayansi, udaktari na ualimu kupata asilimia 100% wengine katika taaluma za sheria,, uhasibu, biashara, sanaa nk walikuwa wakipewa asilimia kadhaa kwa mf 50, 60 na 70%.

Hata hivyo mwaka 2023 wanafunzi ambao hawakusoma na kufaulu masomo yenye mahitaji maalum kama sayansi, ualimu, udaktari wengi wao wamekwakaa kigingi kupata furasa ya kupewa mikopo licha ya kufaulu daraja la kwanza huku wakipewa dirisha la kukata rufaa ya masharti ya kuwa wanachama wa TASAF, wenye Ulemavu au Yatima vikwazo ambavyo vinawakatiza ndoto njema vijana kwa malengo ya kulitumikia taifa katika nyanja mbalimbali

RAI kwa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wawape mikopo vijana wote waliofaulu daraja la kwanza ili kutia hamasa zaidi ujifunzaj wenye kuleta tija. Naamini mikopo inayotolwa na serikali inafuatiliwa na wanufaika watarejesh pindi wakihitimu na kuajiriwa.

Kwa heshima kuu namwomba waziri mwenye dhamana hii Prof Adolf Mkenda kulifikiria hili kwa manufaa ya taifa.
 
Back
Top Bottom