chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,681
Katika nchi ambayo ina wasomi wengi sana nje ya nchi, ni Kenya. Kenya wamewekeza katika elimu ambayo inajibu mahitaji ya soko la dunia, wasomi wao wanakubalika sana duniani.
Katika kuenzi maisha na falsafa za Lowassa, ni vyema tiwekeze katika elimu ya watamzania, na tufungue milango kwa watanzania kwenda nje ya nchi kusaka fursa. Yale maswali yasiyo na maana kwa wanaotaka kwenda nje ya nchi yaondolewe.
Trilioni 10 wanazotuma wakenya nchini kwao ni sawa na robo ya bajeti ya Tanzania ya mwaka mzima. Fedha hiyo ikiingia, uchumi unachangamka.
Hatujachelewa, tuwekeze kwa watanzania katika elimu inayokidhi mahitaji ya soko. Kama ni wanafunzi wa DarTech, wapate elimu ya viwango vya juu, na wale wanafunzi bora wapate mafunzo kwa vitendo huko China, walau miaka miwili. Wale wa SUA waende katika nchi zilizofanikiwa katika kilimo na wakafanye mafunzo kwa vitendo katika vyuo bora vya huko.
Watu wa Wizara ya elimu, wasomi wa vyuo vya sayansi, waende china wakauchimbe mtaala wa elimu wa nchi hiyo, wajue kwa nini umejibu mahitaji ya jamii na sisi tunakwama wapi. Mtaala ufanyiwe analysis na vyuo vikuu bora vya nje ya nchi, ili waupime dhidi ya maslahi ya soko. Wasikae watu wa wizarani waliosoma hadithi za Juma na Roza wakaachiwa kuamua hatma ya kizazi cha artificial intelligence.
The same applies kwa masomo yote ya sayansi, na mengineyo ili tuwe na cream bora kabisa ya taifa hili ikituwakilisha nje ya nchi hii.
Kwa vijana wa sasa, wanaweza kusema Baba Levo na Mwijaku ndio role models wao, kumbe ni watu wa hovyo tu.
R.I.P Leigwanani Edward Ngoyai Lowassa, waliofanya attempts kadhaa juu ya uhai wako, wanakuja kukuombea upumzike kwa amani.