Puncler
JF-Expert Member
- Jul 17, 2017
- 1,388
- 1,884
Stupidity at it's highest level, hebu rudia kusoma uozo ulioandika na ujitathmini uwezo wako kiakili.Nasisitiza kuwa toka tupate uhuru, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hadi Magufuli, wote waliwasikiliza wananchi na kutatua kero zao. Kuna migogoro ambayo kiutatuzi lazima imfikie Rais au inahitaji utatuzi kutoka kwake. Ndo maana utaratibu toka zamani, kukiwa na jambo limeshindikana Mkuu wa Mkoa huto kibali cha mwenye malalamiko au mgogoro kumuona Rais, kama ametembelea mkoa huo au mlalamikaji kwenda Ikulu.
Nakumbuka kipindi cha mzee ruksa, kila mwezi alitenga siku ya kuwasikiliza wananchi Ikulu. tena alisisitiza anataka watu wa hali ya chini ambao wanamigogoro au malalamiko yaloshindikana. Na toka mikoani ilisisitizwa Ofisi au wakuu wa mikoa kuhakikisha watu wenye malalamiko wanafika kuonana na Rais Ikulu.
Nyerere yeye walienda hadi nyumbani kwake, Msasani au Butiama kufikisha malalamiko na aliwasikiliza. Rais Kikwete alikuwa huru popote alipo kuwa anamsikiliza mtu yoyote hata iwe Msoga.
Mama yetu tafadhali, litazame hili kwa namna nyingine. Hawa ndo waliokuchagua. Ukisema unawawakilishi, basi waachie kila kitu kwani tunajua Rais unawawakilishi kila sekta na kila sehemu weye kaa tu Ikulu ule na kulala. Hadi Bungeni unawawakilishi basi usingeenda kuhutubia Bungeni kwani Waziri Mkuu yupo anae wakilisha serikali pia kuna mawaziri bila kumsahau Waziri anae tetea serikali Mama JenisterMhagama!