Rais Samia atenga siku moja kila mwezi kusikiliza kero za watanzania

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,705
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja

"Amefanya hivyo kwa sababu kuu tatu moja ni kuwafanya viongozi wengine wawe na tabia ya kusikiliza kero za Wananchi, sababu ya pili ni kumuenzi Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na jambo la tatu ni kutoa nafasi ya kutumia cheo na nyadhifa za uongozi kuwasaidia Wananchi"

Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa CCM​
 
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja"

Kwa hiyo siku nyingine zote zilizobaki za Mwezi atakua anafanya shughuli gani!?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja
...
Another comedy.

Hivi ni kweli Ccm na serikali yooote hawajui kero za wananchi?? Kwa miaka 63 ya utawala wake?

Ukisikia kwamba Ccm ina tuona wajinga ni statment kama hizi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja

"Amefanya hivyo kwa sababu kuu tatu moja ni kuwafanya viongozi wengine wawe na tabia ya kusikiliza kero za Wananchi, sababu ya pili ni kumuenzi Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na jambo la tatu ni kutoa nafasi ya kutumia cheo na nyadhifa za uongozi kuwasaidia Wananchi"

Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na mafunzo wa CCM
Anakumbuka shuka wakati kumekucha,too late.Anaenda Mikoani akikuta Wananchi njia asimami na akisimama asikilizi kero za Wananchi.
 
Siku nyingine anaziba masikio ? Huu ni Muendelezo wa Maigizo Rais ni Taasisi kama hajui shida zinazoendelea basi hatumii vizuri resources zake...; Kusikiliza maana yake nini ni muda wa kutatua issues sidhani kama mfumuko wa Bei, na changamoto nyingine anahitaji kusikiliza ili atekeleze
 
Kwahiyo Sukari imepanda atatuongezea hicho cha juu na sisi tunywe Uji
 
Popote pale duniani Ukiona Rais anaamua kukutana na Wananchi yeye binafsi basi ujue machinery ya Wasaidizi inafeli kuwahudumia Wananchi

Tumeona jinsi komredi Makonda alivyokuwa analetewa matatizo kibao kana kwamba Nchi hii haina Mawaziri na maDED

Tumeona Maandamano ya Chadema yalivyosheheni mabango ya Matatizo ya Wananchi

Je ni Makonda na Mbowe Ndio wamepelekea Rais Samia kuamua kukutana na Wananchi yeye binafsi?
 
Back
Top Bottom