Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena
Unapokutana na fikra za kijana wa Tanzania mwenye smartphone na anauwezo wakuingia JF anaandika hivi inatia kinyaa sana. Tena inawezekana na kasoma hadi chuo kikuu.

Raisi hata angekua anasikiliza kero za wananchi elfu moja kwa siku kwa hiyo miaka mitano asingewamaliza watanzania wote. So taratibu za kutatua kero zipo zifuatwe ikishindikana mahakama zipo.

Raisi anatakiwa adeal na mambo makubwamakubwa sio petty issues za vibanda vya masoko sijui choo cha stand nooo. Raisi anadeal na taasisi anadeal na mataifa na kuwapa mrejesho wananchi kwa ujumla kupitia hotuba na sio kudeal na mwananchi mmoja mmoja. Sawa kijana?
 
Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena✋
wananchi hawana kero hata moja. jpm alikuwa analazimisha wawe na kero ili aendelee kuuza sura. kero huwa zinatatuliwa kisayansi siyo majukwaani kama lile jamaa lililouawa na waranzania tukamshukuru mungu
 
Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena✋
MATAGA huwa hamjui uongozi, tayari kuna RC NA DC, na mawaziri, alipo waapisha aliwaambiwa wasikilize kero za wananchi, usimfananishe SAMIA na JIWE , jiwe alikuwa naenda MBEZI KUSKILIZA KERO YA KULIPIA CHOO CHA SHS 500, ambayo ilipaswa isikilizwe na afisa mtendaji au balozi wa nyumba kumi;

ATAFANYA ZIARA ila kuskiza kero za kitaifa si kero eti kesi ya miradhi imechelewa kuskizwa, eboo, yani JIWE BHANA.
 
Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena✋
Wabunge na madiwani wenu wana kazi gani?

Amandla...
 
Ila mama anasafiri sana,tangu aanze urais hajatulia kabisa sijui muda wa kufanya maamuzi sahihi anaupata sangapi,muda wa kufikiria changamoto za wananchi na namna za kuzitatua,hata muda wa Ibada na Mwenyezi Mungu anaupata kweli,kila leo safari,events....na ndo ameanza tu majukumu
Urais ni taasisi ,sio kila kitu anafanya yeye Safari zake hazina shida Mana Kuna watu wapo pia
 
Afadhali mara mia ila alikuwa anaiona Tanzania anayoiongoza ipo ktk hali gani
Mwaka jana wakati wa kampeni Rais wa sasa alizunguka kuliko aliyepita. Anaijua vizuri nchi yake.

Tunachokihitaji ni majawabu yatakayoshughulikia matatizo na kero kwa ujumla wake na sio mmoja mmoja ambae anapata kuongea nae.

Hatutaki mtu mmoja alipiwe gharama zake za kutibiwa bali tunataka mfumo uangaliwe ili uwe na nafuu kwa watanzania wengi.

Amandla...
 
Rais ana makatibu tarafa, ma DC, RC, wakurugenzi, mawaziri, hao ndiyo wa kuzurula, kusikiliza kero, kuzitatua na kuzifikisha mbele ya baraza la mawaziri.
Organization structure. Delegation.
Rais anazurulaje kufanya kazi za DC?

Au ndiyo mtego, mnataka mseme mwendazake, alitumia magari tu, huyu anatumia both ndege na misafara ya magari??

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Unaona sasa ulivyo na akili fupi...ukidhani humu unabishana na watoto wenzio.

Shika adabu mjukuu wangu.

Nahisi hata nilichokiandika hujakielewa,na nilikuwa nalenga nini....akili imekujaa maupupu tuu na kuropoka hovyo.

Tunajuaje kuwa wewe ni mtu mzima?,

What comes out of your mind it defines your maturity,nenda kamsaidie house girl kufua nguo
 
Sasa kazi ya wakuu wa mikoa, wilaya,watendaji wa kata,wabunge,TISS n.k itakuwa ni nini.

Kweli kichaa alifanikisha kuwabrainwash wapumbavu wengi.
Rais wetu anakwepa, majukumu yake. Basi ingekuwa kutumia watendaji wake hata huko nje asingeenda, angeacha waziri wa mambo ya nje amwakilishe. Kwani majukumu ya Waziri wa mambo ya nje ni nini?
Katiba inatoa haki ya wananchi kusikilizwa na Rais wao. Si migogoro au Kero zote uweza kutatuliwa na wakuu wa wilaya au Wakuu wa mikoa. Mfano kuna mgogoro ulishawahi tokea, halmashauri iliona vyema kubadili eneo litumike kama makazi. Hivyo viwanja viligawiwa kwa wananchi na wananchi walijenga.
Wizara ikaibuka ikasema hapana, eneo libaki kama hifadhi. Mkuu wa mkoa nae akawa upande wa wananchi.
Nakumbuka ilibidi Rais kuingilia kwani hata hao watendaji wa wizara kidogo wapingwe na wananchi walipojitokeza eneo husika.

Pia kuna migogoro baina ya maeneo ya jeshi na raia, mara nyingi uhitajika kauli ya Rais kama Amiri Jeshi Mkuu. Si hayo tu ni mengi kivyovyote Rais hawezi kukwepa majukumu akasingizia ana wawakilishi. Hatukatai kuwa na wawakilishi, na wanasaidia mengi.

Ila ajue kama mama hawezi acha kila jambo dani ya nyumba kutatuliwa na dada wa kazi. Kuna watoto wakorofi hawatomsikiliza dada au kumtii mpaka wasikie sauti ya mama. Huu ni mfano tu.

Wakuu wa mikoa wapo ila kutokana na utendaji na kanuni za kiutumishi kuna maeneo wanakwama.
Mfano kuna mama alikwamishwa malipo ya haki ya kijana wake kulipwa ambaye alifariki akiwa kazini. Katika kufatilia kote shida ilikuwa wizara ya fedha, walimsumbua yule mama miaka 9 bila kupewa haki ya kijana wake huyu mama alikuwa mzee kaachiwa wajukuu. Na aliishi mikoani.

Mkuu wa mkoa akashughulika na hii kesi ila Wizarani wakawa wanazingua pamoja na kuwepo kwa mawasiliano lukuki.
Mkuu wa mkoa hawezi mwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha.

Kivyovyote kuna mengi ambayo Rais anatakiwa apate muda wa kuwasikiliza wananchi. Asikwepe kijanja. Kama vipi abaki ikulu kukaa tu kwani wawakilishi anao kila mahala. Tujue moja.
Hata marais wote walio pita waliwasikiliza wananchi. Atakuwa Rais wa pekee kukwepa kinamna majukumu yake. Kwanza ukiwasikiliza wananchi, unaelewa nini kinaendelea katika mfumo mzima wa utawala. Wakati mwingine wasaidizi udanganya kwa manufaa yao.
 
Sasa kazi ya wakuu wa mikoa, wilaya,watendaji wa kata,wabunge,TISS n.k itakuwa ni nini.

Kweli kichaa alifanikisha kuwabrainwash wapumbavu wengi.
Kwahiyo Mama hatakiwi kwenda kwa wananchi? Ila ikifika wakati wa Uchaguzi Mkuu ndio aende sio? Washauri wa Mama Oyeeeeeeeee!!!!
 
Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena✋
Kweli Mwendazake aliwapumbazs sana, yaani mnataka mpaka tatizo la shule kukosa choo huko kwenu mtipuka Rais atoke Dodoma kuja kutatua hiyo kero, na wewe unarudhika kabisa na kuona kweli Rais anafanyakazi.

Sasa sijui kazi ya kijiji, uongozi wa kata, wilaya na mkoa, halafu waziri wa elimu na Tamisemi wao kazi yao itakuwa ni ipi?
 
Aende kwa wananchi kufanya nini?? Mfuate Ikulu kama shida yako imeshindwa kutataliwa na msururu wa viongozi kuanzia mwenyekiti wako wa kijiji.

Hata asipoenda wakati wa uchaguzi mkuu atashinda tu akitaka, usijipe umuhimu sana.
Kwahiyo Mama hatakiwi kwenda kwa wananchi? Ila ikifika wakati wa Uchaguzi Mkuu ndio aende sio? Washauri wa Mama Oyeeeeeeeee!!!!
 
Aende kwa wananchi kufanya nini?? Mfuate Ikulu kama shida yako imeshindwa kutataliwa na msururu wa viongozi kuanzia mwenyekiti wako wa kijiji.

Hata asipoenda wakati wa uchaguzi mkuu atashinda tu akitaka, usijipe umuhimu sana.
Sawa
 
Rais ana makatibu tarafa, ma DC, RC, wakurugenzi, mawaziri, hao ndiyo wa kuzurula, kusikiliza kero, kuzitatua na kuzifikisha mbele ya baraza la mawaziri.
Organization structure. Delegation.
Rais anazurulaje kufanya kazi za DC?

Au ndiyo mtego, mnataka mseme mwendazake, alitumia magari tu, huyu anatumia both ndege na misafara ya magari??

Everyday is Saturday............................... :cool:
Nasisitiza kuwa toka tupate uhuru, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete hadi Magufuli, wote waliwasikiliza wananchi na kutatua kero zao. Kuna migogoro ambayo kiutatuzi lazima imfikie Rais au inahitaji utatuzi kutoka kwake. Ndo maana utaratibu toka zamani, kukiwa na jambo limeshindikana Mkuu wa Mkoa huto kibali cha mwenye malalamiko au mgogoro kumuona Rais, kama ametembelea mkoa huo au mlalamikaji kwenda Ikulu.
Nakumbuka kipindi cha mzee ruksa, kila mwezi alitenga siku ya kuwasikiliza wananchi Ikulu. tena alisisitiza anataka watu wa hali ya chini ambao wanamigogoro au malalamiko yaloshindikana. Na toka mikoani ilisisitizwa Ofisi au wakuu wa mikoa kuhakikisha watu wenye malalamiko wanafika kuonana na Rais Ikulu.
Nyerere yeye walienda hadi nyumbani kwake, Msasani au Butiama kufikisha malalamiko na aliwasikiliza. Rais Kikwete alikuwa huru popote alipo kuwa anamsikiliza mtu yoyote hata iwe Msoga.
Mama yetu tafadhali, litazame hili kwa namna nyingine. Hawa ndo waliokuchagua. Ukisema unawawakilishi, basi waachie kila kitu kwani tunajua Rais unawawakilishi kila sekta na kila sehemu weye kaa tu Ikulu ule na kulala. Hadi Bungeni unawawakilishi basi usingeenda kuhutubia Bungeni kwani Waziri Mkuu yupo anae wakilisha serikali pia kuna mawaziri bila kumsahau Waziri anae tetea serikali Mama JenisterMhagama!
 
Ndugu hii ni awamu ya 6. Mwinyi aliwasubiri ikulu, wewe unataka awatembelee, unajuaje kama yeye mama hatowakaribisha pia wananchi ikulu??

Muacheni mama Rais, ajipangie anachotaka, apangilie safu yake ya uongozi na aweke vision yake 2021-2035.
Atake asitake tutampa nchi hata milele😂

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Sasa kazi ya wakuu wa mikoa, wilaya,watendaji wa kata,wabunge,TISS n.k itakuwa ni nini.

Kweli kichaa alifanikisha kuwabrainwash wapumbavu wengi.
Na ikifika uchaguzi awatume hao hao wakuu wa wilaya na TISS kuomba kura.
 
Japokua hayati alikua anaendesha nchi kibabe, lakini kuna baadi yamambo aliyafanya yalitupendezea hata sisi wananchi wanyonge tunaoshi chini ya dola moja kwa siku,

ziara za sehemu mbalimbali kusikiliza kero za wananchi zilitufariji sana,

kwa heshima na taadhima tunakuomba mama yetu, Amiri jeshi mkuu, President material mweshimiwa Rais samia suluhu uanze ziara za kusikiliza kero za wananchi wako wanyonge na kuzitafutia ufumbuzi

tunakupenda sana

asante sana

mitano tena✋
Achana na unyonge mkuu. Tanzania ina ardhi kubwa,maji, dhahabu, mvua za kutosha,watu wengi kwa nini ujipe unyonge.Yani umekubali kuwa maskini.
Ukitaka favor za unyonge utazeeka ukiwa maskini.
 
Wanyonge mnyongwe zenu,na haki zenu msipewe tuh,nyinyi ndiyo mlikuwa mnapa bichwa yule mwendazake aliposema kuwa matajir waishi kama mashetani,na mkawa mnashangiliiiaa, wachawi wanyonge
Ila masikini ni ana roho chafu kama masizi

I strongly hate poverty
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom