Rais Samia: Nendeni mkasikilize kero za wananchi. Huko ndiyo kura ziliko

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
"Nendeni mkasikilize kero za wananchi" - Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.

---
---
Makonda amezunguka mmeona mfano, Wananchi wana kero kadhaa, nyingine nyepesi tu za kutatuliwa huko chini, hawasikilizwi. Na wasiposikilizwa zile ndiyo kura zetu.

Akipita mwingine akiwaambia mimi nikiingia ntawasikiliza watampa. Kwamba sisi tumewapuuza hatuwasikilizi. Kule ndiko ulipo ushindi wa chama kilichokuwekeni.

Mkifanya vingine wengine watakuja wabebe ushindi waondoke nao. Kwahiyo niwasisitize sana kusikiliza Wananchi
 
Back
Top Bottom