Rais Samia, inakuwaje kero za Wananchi kuletwa Ikulu wakati kuna viongozi kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kijiji?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,049
49,731
My Take
Serikali ibadilishe sheria inayosimamia mamlaka za serikali za mitaa Ili Viongozi wa kuanzia ngazi ya Mkoa wachaguliwe na kuwajibika Moja kwa Moja kwa Wananchi.

---
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa ngazi zote za serikali kuacha tabia ya kukaa ofisini badala ya kushuka chini kusikiliza na kutatua kero ambapo ameeleza kusikitishwa kuona kero za wananchi wa vijijini zinapelekwa Ikulu wakati kwenye maeneo yao kuna viongozi.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 17,2023 katika mkutano na wananchi wa Mangaka Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kusini.

View: https://www.instagram.com/reel/CxSw316NjOv/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
My Take
Serikali ibadilishe sheria inayosimamia mamlaka za serikali za mitaa Ili Viongozi wa kuanzia ngazi ya Mkoa wachaguliwe na kuwajibika Moja kwa Moja kwa Wananchi.

View: https://www.instagram.com/reel/CxSw316NjOv/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Watu wa kusini wanaangushwa na viongozi wao ngazi ya mkoa mpk chini

Wanaletewa Mashine na serikali CT scan eti wanakosa pa kuiweka,wanataka kujengewa kila kitu

Watachelewa sana,kuendelea ni mindset ndio maana wapo nyuma sana kimaendeleo
 
Watu wa kusini wanaangushwa na viongozi wao ngazi ya mkoa mpk chini

Wanaletewa Mashine na serikali MRI eti wanakosa pa kuiweka,wanataka kujengewa kila kitu

Watachelewa sana,kuendelea ni mindset ndio maana wapo nyuma sana kimaendeleo
Hilo sio swala la Kusini ni shida iliyopo maeneo mengi sana ya Nchi.Rukwa huko Hadi Leo hii Mashine ya CT Scan imewekwa tuu ila jengo lometelekeswa wakati Mikoa mingine majengo yanafanya kazi.
 
Rais aanze kwa kukemea tabia ya watu kumsifiasifia hovyo hovyo, watu wasifie serikali. Sasa hivi hata dc akienda kuwasikiliza wananchi, watu hawaisifii serikali au chama tawala au serikali ya wilaya/mkoa, wanamsiu rais yeye binafsi na anaona ni sawa tu.

Kwa nini alalamike watu wanapompelekea shida ndogondogo hata za kutatuliwa na serikali za mitaa?
 
Sasa kama kwa Kila tukio sifa zote anapewa chifu Hangaya (awepo asiwepo) kwanini matatizo pia asipewe??
 
Back
Top Bottom