Paul Makonda Kufanya ziara Kigoma hapo kesho

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya Mheshimiwa Paul Makonda kusimamisha ziara yake kwa siku chache ili kuungana na kushiriki katika ziara ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan pale mkoani Mwanza alipokuwa amekuja kwa ajili ya kugawa boti za kisasa kwa wavuvi ,sasa ziara za Mheshimiwa Makonda katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM Pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua inaendelea hapo kesho kwa kishindo kikuu kule mwisho wa Reli kigoma.

Mheshimiwa Makonda ambaye kwa sasa anatambulika kama chifu Nsumbantale yaani msaidizi wa chifu mkuu Hangaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa ,lakini pia akifahamika na kutambulika kama kijana jasiri kuwahi kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara kwa siku za hivi karibuni. Anatarajiwa kufanya ukaguzi wa kina juu ya utekelezaji wa ilani,kuangalia namna wananchi wanavyohudumiwa pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuwapatia majibu papo kwa papo.

Mheshimiwa Makonda ambaye anaendelea kuteka hisia za watu na kugusa mioyo ya watanzania ameendelea kuwa gumzo hapa nchini na hata nje ya mipaka ya Tanzania ,kutokana na staili yake ya kuwasikiliza wananchi kero zao na kuwaita au kuwapigia simu wahusika papo kwa papo ili watoe majibu na ufafanuzi.ziara zake zimekuwa ni mwiba mkali na mchungu sana kwa viongozi wazembe,wala rushwa,wanaofanya kazi kwa mazoea na kushindwa kuwahudumia wananchi.

Lakini kwa upande mwingine ziara zake zimekuwa Tumaini,faraja,nuru mpya katikati ya giza,kimbilio la watanzania wanyonge,walioonewa kwa kunyimwa haki zao au kutelekezwa au kucheleweshewa miradi inayotakiwa kukamilika kwa haraka ili kuwapunguzia na kuwaondolea adha za kuhangaika kutafuta huduma.

Tukae kwa utulivu kusubili kuona na kusikia kitakachojili katika ziara yake hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa sana na wanakigoma ,ambao wanatamani kumuona Mheshimiwa akikanyaga ardhi yao.maana wanajuwa ni sauti ya wanyonge na tumaini la wenye kuonewa na kudhulumiwa haki zao.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240120-WA0007.jpg
IMG-20240115-WA0007.jpg
 
Ila wajuba mnakaza sana. Nyuzi za huyu ndugu huwa zina ukame sana wa likes.

Sio Mchezo
 
Safi sana mimi nipo hapa Iyagala Kigoma mtetezi wa Wanyonge atakuwa Kwetu leo nitalala Kigoma kumpokea Mh.Makonda kwà kweli ametukosha sana sisi wanyonge.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya Mheshimiwa Paul Makonda kusimamisha ziara yake kwa siku chache ili kuungana na kushiriki katika ziara ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan pale mkoani Mwanza alipokuwa amekuja kwa ajili ya kugawa boti za kisasa kwa wavuvi ,sasa ziara za Mheshimiwa Makonda katika ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM Pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua inaendelea hapo kesho kwa kishindo kikuu kule mwisho wa Reli kigoma.

Mheshimiwa Makonda ambaye kwa sasa anatambulika kama chifu Nsumbantale yaani msaidizi wa chifu mkuu Hangaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa ,lakini pia akifahamika na kutambulika kama kijana jasiri kuwahi kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara kwa siku za hivi karibuni. Anatarajiwa kufanya ukaguzi wa kina juu ya utekelezaji wa ilani,kuangalia namna wananchi wanavyohudumiwa pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuwapatia majibu papo kwa papo.

Mheshimiwa Makonda ambaye anaendelea kuteka hisia za watu na kugusa mioyo ya watanzania ameendelea kuwa gumzo hapa nchini na hata nje ya mipaka ya Tanzania ,kutokana na staili yake ya kuwasikiliza wananchi kero zao na kuwaita au kuwapigia simu wahusika papo kwa papo ili watoe majibu na ufafanuzi.ziara zake zimekuwa ni mwiba mkali na mchungu sana kwa viongozi wazembe,wala rushwa,wanaofanya kazi kwa mazoea na kushindwa kuwahudumia wananchi.

Lakini kwa upande mwingine ziara zake zimekuwa Tumaini,faraja,nuru mpya katikati ya giza,kimbilio la watanzania wanyonge,walioonewa kwa kunyimwa haki zao au kutelekezwa au kucheleweshewa miradi inayotakiwa kukamilika kwa haraka ili kuwapunguzia na kuwaondolea adha za kuhangaika kutafuta huduma.

Tukae kwa utulivu kusubili kuona na kusikia kitakachojili katika ziara yake hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa sana na wanakigoma ,ambao wanatamani kumuona Mheshimiwa akikanyaga ardhi yao.maana wanajuwa ni sauti ya wanyonge na tumaini la wenye kuonewa na kudhulumiwa haki zao.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.View attachment 2890589View attachment 2890590
Dada unateseka sana loh !!
 
Back
Top Bottom