asiliyetu kwanza
Member
- Aug 20, 2021
- 24
- 18
Balaa zaidi unapoweka,au pesa Yako inapopitishiwa bank makato yake utakoma ukitoa Benji kupeleka katika simu wanakata na unapotoa katika simu Nako wanakata Kila Kona tozo hatari sana.
Sijui Rais Samia kaziba masikioMtu anafanya biashara kila akifunga anapeleka hela bank then kesho anaenda kuitoa anakatwa chaji za kutoa benki,VAT na tozo unategemea huyu mtu ataendelea kuweka pesa benki?
kila akifanya transfer kulipa suppliers the same,tuwe serious basi na maisha ya watu
Mwigulu anaamini kabisa kuwa sisi ni Mifugo.kukataa kuswagwa kama Ng'ombe kwenye
Tupunguze kukopa nje ili tozo zipungue..nchi inalazimika kuweka tozo nyingi ili kuonesha uhimilivu wa kurejesha madeniHizo tozo na Kodi ndio zinazojengwa vituo vya Afya, shule, zahanati, huduma za maji,umeme Hadi vijijini, kwa hiyo lazima ujuwe kuwa hata ulaya walipitia huku, Hakuna njia fupi katika kupata maendeleo, watanzania wametulia na wanaendelea kumuunga mkono mh Rais kwa kuwa tunaona maendeleo yanayoletwa na mh Rais,
Lazima tuanze kujitegemea wenyewe kwa kuhakikisha kuwa tunachangia maendeleo yetu wenyewe, Tusipende kujirundikia mimadeni tu, maana madeni Ni mzigo na yanaleta utumwa, tujifunge mikanda na tujibane ili kujenga nchi yetu,
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza akaandamana wakati anaona namna mh Rais anavyo fanya kazi usiku na mchana kuijenga nchi hii na kuinua maisha ya watu, hakuna wa kuandamana wakati anaona tozi hizo zikielekezwa katika miradi ya maendeleo, hakuna wa kuandamana wakati kila mtu anaona namna mh Rais alivyo tanguliza maslahi ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa kila sent inayopatikana Ina kwenda kuwekezwa mahali penye kero kwa watu
Wananchi tupo na mh Rais na tunaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu, tunaendelea kuona namna anavyo gusa maisha ya watu wote, tunaona namna mh Rais anavyo fanya kazi kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma
anaona ni hela rahisi haumizi kichwa inaingia ti vrooooom na inaibiwahatari wakimaliza hapa ni kunununa ma vx models za 2022Sijui Rais Samia kaziba masikio
Wasukuma mnapata tabu sana, sasa Jiwe yeye alikuwa akikuta pesa zako bank anachukua nusu yake ila wewe unalia na katozo. Pole mkuuMtu anafanya biashara kila akifunga anapeleka hela bank then kesho anaenda kuitoa anakatwa chaji za kutoa benki,VAT na tozo unategemea huyu mtu ataendelea kuweka pesa benki?
kila akifanya transfer kulipa suppliers the same,tuwe serious basi na maisha ya watu
Nyie sukuma gang mpaka akili ziwakae sawaSijui Rais Samia kaziba masikio
Hii ni dhahiri kama tungesimama pamoja tutaweza kuondoa huu ukatili uliopindukia wa bwana fedha tena uliojaa kebehi na dharau kubwa.Kwa lugha rahisi tu wananchi sisi ndio wenye nchi na huyu Mwigulu Nchemba na mama sisi ndio mabosi wao, sisi siyo vijakazi wao hili lieleweke dhahiri shairi.