Hizi ndiyo Tozo mpya za miamala ya Simu na Benki kuanzia leo Ockoba 1, 2022

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 ambalo Mwananchi imeliona imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).

Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999 ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.

Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.

Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.

Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Kifungu cha 46A (2) kimeelezea kanuni za marekebisho ya kanuni za tozo ya miamala ya fedha ya kielektroniki za mwaka 2022 na zimeanza kutumika jana Oktoba mosi.

“Kanuni hizi zitajulikana kama kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki za Mwaka 2022, na zitasomwa pamoja na Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki, 2022 ambazo hapa zitarejewa kama “Kanuni Kuu”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kanuni Kuu zinarekebishwa katika kanuni ya 3 kwa kufuta tafsiri ya neno “kuhamisha fedha” na badala yake kuweka “kuhamisha fedha” maana yake ni kuhamisha fedha kielektroniki kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji.

Tafsiri hiyo inaendelea kusema, Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo;

“Akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji huyo huyo na akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo.”

Screenshot_20221001-194323_1.jpg
Screenshot_20221001-194528_1.jpg
Screenshot_20221001-194532_1.jpg
 
Watu wa uchumi,njooni mtueleweshe kwa ufupi.Nimekaa hapa na Msukuma Phd,tunasubiri uchambuzi wenu,i.e mtuwekee in simple words.
 
Niliwahi kumuona mheshimiwa Mramba(marehemu) kwenye foleni pale hospitali fulani, hii ni baada ya kutuambia tule nyasi....

Tumsubiri tu, si anasomesha mtoto wa Bongo movie saa hii!
 
Inasemwa zimeanza kutumika Jana October mosi ,,Ili hali leo bado ni tr 01oct,,au unareport kutokea wapi.

Hata hivyo kuna unafuu kidogo ,,sijui kwenye kutoa kwa wakala
 
Alie elewa anieleweshe, hiyo ni MIAMALA ipi? ya kibenki au simu to simu? Serikali muwe mnafafanua watu wajue mnamaani kitu gani
 
Kifupi ni kwamba tozo ziko palepale....

Isipokuwa kama unajihamishia mwenyewe kwenye akaunti zako..
 
Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 ambalo Mwananchi imeliona imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).

Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999 ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.

Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.

Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.

Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Kifungu cha 46A (2) kimeelezea kanuni za marekebisho ya kanuni za tozo ya miamala ya fedha ya kielektroniki za mwaka 2022 na zimeanza kutumika jana Oktoba mosi.

“Kanuni hizi zitajulikana kama kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki za Mwaka 2022, na zitasomwa pamoja na Kanuni za Tozo ya Miamala ya Fedha ya Kielektroniki, 2022 ambazo hapa zitarejewa kama “Kanuni Kuu”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kanuni Kuu zinarekebishwa katika kanuni ya 3 kwa kufuta tafsiri ya neno “kuhamisha fedha” na badala yake kuweka “kuhamisha fedha” maana yake ni kuhamisha fedha kielektroniki kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji.

Tafsiri hiyo inaendelea kusema, Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo;

“Akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya simu ya mtumiaji huyo huyo na akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji, isipokuwa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya benki ya mtumiaji kwenda akaunti ya benki ya mtumiaji huyo huyo.”

View attachment 2374020View attachment 2374021View attachment 2374022
Kanuni zimeandikwa kwa Kiswanglish.
 
Angalau !!
 
Haijambo haijambo hongera Waziri, ila ma V8 nayo myauze hayo tutumie defender,Vanguard au cruiser mkonge uchumi wa dunia umekuwa mgumu sana.
 
Back
Top Bottom