Je, ni kweli kuwa Serikali yetu imekosa kabisa ubunifu wa kuzuia ufujaji wa pesa za umma katika miradi ya kuboresha maisha ya watu maskini?

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
886
930
Ukitembea tembea huko mitaani hasa vijijini, utawahurumia sana wananchi wenzetu wanavyoishi kwenye hali duni kabisa kimaisha. Naam, namaanisha uduni wa kukosa huduma za msingi kama vile barabara nzuri, maji safi na salama, elimu bora, matibabu bora, mawasiliano ya uhakika, huduma za nishati n.k.

Natambua kuwa hii nchi yetu bado ni maskini sana ukilinganisha na nchi nyingine zilizoendelea na vilevile kwa kuzingatia viwango vilivyopo vya hali ya maisha ulimwenguni kupitia taasisi za kimataifa kama vile World Bank, IMF n.k. Hata hivyo, nashawishika kusema kuwa waTanzania hawastahili umaskini huu.

Ukiangalia maisha ya anasa wanayoishi viongozi walio wengi, ukatazama na maisha ya watu wa kawaida hasa vijijini, unaweza sema viongozi wetu wanaongoza watu wa nchi nyingine na si hii tuliyonayo hapa Bongo. Ukimleta mgeni atazame viongozi wetu jinsi walivyonona kutokana na utamu wa pesa za wavuja jasho, kisha awatazame na wananchi wa vijijini, atakataa kabisa kuwa hawa viongozi hawatoki kwenye jamii yetu.

Anyway, msingi wa hoja yangu si hali ya umaskini tuliyonayo hapa nyumbani (hali inayotokana na uzembe tu), ila ni namna ambavyo Serikali inashughulika na pesa za umma ambazo huzikusanya au kuzisimamia katika kuboresha maisha ya watu wake.

Ukitizama taarifa za habari, hasahasa ktk ziara za Waziri Mkuu, hutaacha kusikia Waziri Mkuu akilalamika kuhusiana na matumizi ya ovyo na ufujaji wa pesa za umma mahala flani. Tena, nadhani huyu Waziri Mkuu yeye wakati mwingi huwa analalamika lalamika sana na kujaribu kuonesha anachukizwa na mambo ya ovyo yaliyofanyika kuhusiana na ufujaji wa pesa za miradi ya wananchi hasa maskini.

Hata hivyo, huwa anaishia kuagiza kuundwa kwa Tume flani kuchunguza jambo flani na akichukua hatua zaidi basi wahusika huwa wanasimamishwa kupisha uchunguzi na watu wachache sana huwa wanafikishwa mahakamani. Mathalan, watu wanaofikishwa mahakamani, kwa kiasi kikubwa (sio wote), huwa hutupati mrejesho wa hatua za mwisho zilizofanyika.

Kwa kuongezea, kila mwaka utasikia upigaji mkubwa sana kupitia report ya CAG kuhusiana na pesa za nchi hii pendwa yenye umaskini uliopitiliza. Sasa mie huwa najiuliza na kushangaa sana;

i) Ya kwamba, nchi yetu yenye vyombo mahiri kabisa, huwa inashindwa vipi kuzia huu upigaji mpaka kusubiriwa ziara za Waziri Mkuu au kiongozi mwingine wa juu?

ii) Ya kwamba, Serikali yetu sikivu, yenye viongozi mahiri kabisa, imekosa au imeshindwa kabisa kuja na ubunifu wa kuzuia ufujaji wa pesa hizi za umma za watu maskini ktk nchi hii? Ujue nchi yetu si kwamba inakuwa haina pesa za kuboresha huduma za kijamii, isipokuwa, kuna watu wachache tu ndio wanufaika wa hizi pesa huku walio wengi wakiendelea kuwa maskini na fukara.

iii) Ya kwamba, viongozi wetu wanaishia kulalamika tu majukwaani ila wameshindwa kuja na mwarobaini wa tatizo hili? Mbona mambo mengine huwa inaweza kuyafanya kwa ufasaha? Sitaki kuyataja nisije haribu ujumbe wa uzi huu....

Jamani, kwa akili ya kawaida, kama hizi pesa za miradi za wavuja jasho zimekosa mwarobaini wa kuzisimamia vizuri ili kuwasaidia watu maskini hasa vijijini, ni kwa nini sasa Serikali yetu isikiri kuwa tatizo hili limetushinda sisi waAfrika wa hapa nyumbani?

Kwamba tukubali kuwa upigaji ni jadi yetu sisi waAfrika, na kwamba, hata ufanyeje mtu mweusi huwezi kumtenganiusha na tamaa za pesa na ukosefu wa maadili ikiwemo ustaarabu wa kuheshimu mambo yetu wenyewe. Hivyo tuwaite wageni ambao wao watapewa jukumu la kusimamia miradi yote kwa makubaliano maalumu yaliyo ya wazi wakatumia mbinu kama wanavyofanikiwa huko makwao?

Au la,
Kama upigaji imeshindikana kudhibitiwa kwa mfumo huu wa sasa, ni kwanini wasichaguliwe watu wachache tu kitaifa, walio waaminifu sana, kisha wakapewa jukumu la kusimamia miradi yote nchini ambako pesa zake huishia kupigwa na watu wachache huku idadi kubwa ya waTanzania ikibakia kuwa maskini kwa kukosa huduma bora za kijamii?

Ngoja niishie hapa kwa sasa. Jumapili njema iwe nawe msomaji wa ujumbe huu!
 
Kuna kiongozi wa ngazi ya juu kabisa hapa nchini,aliwahikusikika akiwaambia viongozi wetu kua eti anajua kabisa kuwa wanapiga hela sehemu walizopo,na akawasihi wasipige sana hadi wakapitiza.

Vivyohivyo,amewahi kusikika akiwasihi makatibu sijui makarani,wawe na siri maofisini hatakama wameona king'asti kimeingia muda wa kazi ofisini kwa aliyemuita.

Shida ni madhaifu ya baadhi ya viongozi. Majaliwa, alifaa sana kuchukua kijiti cha huyu Rais,akimaliza muda wake 2030.
 
Hakuna maadili, ni wizi na rushwa kila sehemu.

Halafu ni asilimia kubwa ya wananchi wanatamani wapate ajira serikalini ili waibe. Ukiangalia comments za wengi ambapo Habari ikija ya wizi wa mabilioni utaona wajinga wanakuambia hata ningekuwa mimi nisingeziacha.

Hapo usitegemee uzalendo bali ni mwendo wa kuiba tu. Viongozi hawana aibu na hela wakiiba hawawezi kufungua viwanda bali wanaishia kuwapa hawara zao apartments tu na kuwafungulia salons.

Inasikitisha sana
 
Hawajakosa ubunifu wanafanya maksudi tu kwasababu hatuna cha kuwafanya, mfano mdogo tu ni mgawo wa umeme, kabla ya serikali ya Magu mgawo kila uchao alipoingia yeye akadhibiti kwa 99.9%, haya sasa Magu hayupo tumerudi kulekule, je tuamini kwamba hakuna anayejua mbinu alizotumia Magu kudhibiti hili tatizo?

Jibu ni hapana, ila wanafanya maksudi kwa ajili ya maslahi yao na wanajua hatuna cha kuwafanya, ukiandamana utapigwa marungu na ukisubiri sanduku la kura huko ndio balaa,unaweza ukaambiwa umepata kura sifuri hata kwenye kituo ambacho umejipigia kura.

Huwa nawaonea huruma wale wanaokwenda kwenye mikutano ya hawa viongozi wa CCM bila malipo yoyote.
 
Kuna kiongozi wa ngazi ya juu kabisa hapa nchini,aliwahikusikika akiwaambia viongozi wetu kua eti anajua kabisa kuwa wanapiga hela sehemu walizopo,na akawasihi wasipige sana hadi wakapitiza.

Vivyohivyo,amewahi kusikika akiwasihi makatibu sijui makarani,wawe na siri maofisini hatakama wameona king'asti kimeingia muda wa kazi ofisini kwa aliyemuita.

Shida ni madhaifu ya baadhi ya viongozi. Majaliwa, alifaa sana kuchukua kijiti cha huyu Rais,akimaliza muda wake 2030.

Majariwa huyu huyu kitochi, ambaye mwanae anahusika kwenye magendo ya makontena ya vitenge, huyu huyu aliyesema JPM yupo ofisini anachapa kazi kumbe jpm anapigania uhai wake kitandani mbaya zaidi uongo huo kautoa akiwa msikitini.

Hivi unawajua madalali wakubwa wa korosho
 
Majariwa huyu huyu kitochi,ambaye mwanae anahusika kwenye magendo ya makontena ya vitenge,huyu huyu aliyesema jpm yupo ofisini anachapa kazi kumbe jpm anapigania uhai wake kitandani mbaya zaidi uongo huo kautoa akiwa msikitini.

Hivi unawajua madalali wakubwa wa korosho
Tena ni mtu hatari sn huyu mzee
 
Hakuna maadili, ni wizi na rushwa kila sehemu
Halafu ni asilimia kubwa ya wananchi wanatamani wapate ajira serikalini ili waibe
Ukiangalia comments za wengi ambapo Habari ikija ya wizi wa mabilioni utaona wajinga wanakuambia hata ningekuwa mimi nisingeziacha

Hapo usitegemee uzalendo bali ni mwendo wa kuiba tu
Viongozi hawana aibu na hela wakiiba hawawezi kufungua viwanda bali wanaishia kuwapa hawara zao apartments tu na kuwafungulia salons

Inasikitisha sana
Kuna sehemu niliandika tukiendelea hivi ndani ya miaka 20 ijayo tutakuwa taifa bovu kuliko Congo.
 
Majariwa huyu huyu kitochi,ambaye mwanae anahusika kwenye magendo ya makontena ya vitenge,huyu huyu aliyesema jpm yupo ofisini anachapa kazi kumbe jpm anapigania uhai wake kitandani mbaya zaidi uongo huo kautoa akiwa msikitini.

Hivi unawajua madalali wakubwa wa korosho
Duh!

Toba....!!!
 
Kuna sehemu niliandika tukiendelea hivi ndani ya miaka 20 ijayo tutakuwa taifa bovu kuliko Congo.
Kwa kweli sintashangaa kabisa kwa sababu kila leo ni bora kuliko jana
Watz hawana tabia ya kuhama nchi yaani anaona ataanzaje maisha mapya
Watakaa hapo hapo bila mabadiliko
Jembe la mkono hesabu miaka 50 mingine
 
Ukifika mkoa wa Katavi utawahurumia wananchi! Ni mateso makubwa, kuna sehemu watoto wanatembea zaidi ya kilomita 10 kufuta shule za msingi na Sekondari! Hospital au vituo vya afya havipo!
Hata Wewe ukipata fursa ya kuwa Kiongozi utakuwa Mwizi tu kama hao waliopo sasa

hata katika level yako tu ya shughuli za kila siku pengine huwa unafanya ubadhirifu wa hapa na pale kwa maslahi binafsi

sie Binadam tunakuwa na maarifa na utu sana kama tu hatuna kitu au tunawakosoa wenzetu.

Hujawahi kuona Mama anamlaumu Mke wa Kijana wake kwa kwa kufanya Mume aelekeze nguvu kubwa kusaidia ukweni kuliko kwa Wazazi wake lakini hapo hapo anashabikia na kufurahia Mume wa Binti yake akisahau kwao na kuelekeza Maokoto yote kwake ?
 
Mkuu, Je unataka kumanisha kuwa haiwezekani kuwa na Jamii yenye watu Waadilifu? Kwamba sisi binadamu wa huku Afrika, hatuwezi kabisa kujitenga na makando kando kwenye pesa au kazi za Umma?
 
Mkuu, Je unataka kumanisha kuwa haiwezekani kuwa na Jamii yenye watu Waadilifu? Kwamba sisi binadamu wa huku Afrika, hatuwezi kabisa kujitenga na makando kando kwenye pesa au kazi za Umma?
Usizungumzie Jamii, anza kwanza Wewe binafsi

Jee wewe ni Muadilifu? sio uaminifu kwa mujibu wa sheria za kibinadamu …kwa mujibu wa Sheria za Mungu na moral values , yaani huibi hata kama unaweza kuficha usionekane umeiba, hudhulumu Mtu hata kama yule Mtu hatojua kama kadhulumiwa

ukiona umeacha kuiba au kudhulumu kwa kuwa utashtakiwa hapo tunakutambua kama Mtii sheria bila shuruti ila kwny kundi la Waadilifu haupo
 
Ukiona yafuatayo ktk taifa ujue taifa hilo kamwe haliwezi kupiga hatua:-
1. Matajiri ni wanasiasa.
2. Kila mtu (hata wasomi na wanataaluma) anatamani kuwa mwanasiasa.
 
Ukiona yafuatayo ktk taifa ujue taifa hilo kamwe haliwezi kupiga hatua:-
1. Matajiri ni wanasiasa.
2. Kila mtu (hata wasomi na wanataaluma) anatamani kuwa mwanasiasa.
Sahihi kabisa

wanaoshauri vijana waachane na siasa na wajikite kwny kilimo kinalipa watoto wao wanawachomeka kwny nafasi za uchipukizi tangu wakiwa chini ya miaka 10 ili waje kuwa Wanasiasa kama wao.
 
Usizungumzie Jamii, anza kwanza Wewe binafsi

Jee wewe ni Muadilifu? sio uaminifu kwa mujibu wa sheria za kibinadamu …kwa mujibu wa Sheria za Mungu na moral values , yaani huibi hata kama unaweza kuficha usionenekane umeiba, hudhulumu Mtu hata kama yule Mtu hatojua kama kadhulumiwa

ukioba kuiba au kudhulumu kwa kuwa utashtakiwa hapo tunakutambua kama Mtii sheria bila shuruti ila kwny kundi la Waadilifu haupo
Kwa bahati mbaya tunakutana hapa na anonymous ID na hivyo hatufahamiani. Kwahiyo hata nikikujibu inaweza isisaidie jambo maana hatujuani. Ukweli utakabia ndani ya moyo wangu.

Pamoja na ukengeufu mkubwa wa Mwanadamu, nachoamini ni kuwa, bado inawezekana kuwa na watu wenye kujali misingi ya maadili, wasiokuwa na tamaa ya mali, wenye kutosheka, wenye nidhamu na wenye kufuata misingi ya kistaarabu.

Nachoamini pia ni kuwa, Serikali ina uwezo wa kutengeneza jamii yenye kujali misingi tajwa hapo juu maana kazi ya kubadili tabia za watu ni jambo linalowezekana kabisa. Ukitembea tembea huko kwa wenzetu utaona utofauti kati yetu na wao.

Kwa kumalizia, ninachoamini pia ni kuwa, Serikali inao uwezo kabisa wa kuhakikisha kuwa fedha zote za umma zinatumika bila kuibwa hata senti moja endapo itaamua kufanya hivyo. Hilo linawezekana kabisa, hata wakinipa mie niliye mwananchi wa kawaida, hiyo kazi ya kutengeneza strategies za kuhakikisha pesa za miradi ya umma zinafanya kazi yake bila kuibwa naweza.

Nikuhakikishie kuwa ktk nchi hii wapo watu wengi tu wenye kujali misingi ya maadili na ambao wakipewa kusimamia zoezi la kufanikisha miradi ya umma wanaweza kufanya kazi hiyo bila kunyofoa hata senti moja.
 
kama una muda na upo interested, google usome kwa kirefu kwanini utopian socialism ya kina Karl max haikuweza ku survive, utajifunza mengi sana kuhusu hiyo dhana mnayoifikiria, walishaifikiria watu wenye brain kubwa sana karne kadhaa zilizopita

kama haikuwezekana wakati huo sidhan kama sasa hivi itawezekana
 
Asante nitasoma.
 
Back
Top Bottom