Ngawaiya: CHADEMA wanapewa pesa na Marekani kuchochea fujo

It doesn`t matter,tunachotaka ni Tanzania mpya na wala si tz yenye mafisadi,rushwa na umaskini mkubwa huku tukijifariji na amani,amani pasipo haki na maendeleo si kitu na amani haiji bila upanga.CDM kupewa pesa ni sahihi kabisa.
 
Hata Makaburu walitumia propaganda nyingi sana kuwapaka matope ANC na Mandela, lakini zote ziligonga mwamba, Vijana wazalendo wa Tanzania tumeshaamua tunataka Nchi yetu ambayo Mafisadi wameuziwa na Chama Cha Mafisadi, hatudanganyiki na vibaraka wao waganga njaa, CDM mbele hadi kieleweke!
 
Usalama wa taifa mmerahisishiwa kazi. Mtu kakiri hadharani kupokea pesa na kufanya uchochezi na amemtaja na mwenzake Mrema, bado polisi na Usalama wa taifa mnasubiri nini?? Au kwa sababu sasa hivi yuko CCM??

Kamata huyu mtu, weka ndani, chukua maelezo yake na atoe uthibitisho wa CDM kupokea pesa kama hizo. Vinginevyo kweli tutajua serikali iko likizo. Hatuwezi tukaacha mtu anaropoka tu mambo serious namna hiyo, halafu mseme kuna serikali!!??
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.

Sasa huu ndio uzushi wenye nia mbaya, mbona hamuonyeshi ushahidi wa tuhuma zenu? Uasi huu kama kweli upo kwanini usianzie Mtwara au Lindi ambako wananchi wamechoshwa na uongo wa serikali?
 
Ngawaiya sawa na Tambwe et al,hiyo kauli yake ikijulikana ni kweli naye ana kesi ya kujibu,vilevile anasahau kwamba hayupo salama kuwakejeli watanzania
 
duuuuuuuuuu kumbe ccm imeficha vibaka wengi eheee? uyu babu kumbe alikula ela haramu na mrema??????? Mimi nawashukuru wafadhiri akiwemo na sabodo kwa kuwagemea cdm vi ela vya kutuamasisha, kama marekani kuna vi ela vingine watusaidie tumtoe fisadi pangoni!!!!!!!!!!!!!
 
I just cant wait to hear the responce from the Americans kwa kupitia Ubalozi wao. Kwa hili Ngawaiya kalikoroga kwa kuipanga Marekani upande wa Chadema tena kwa kutumia tuhuma zisizo na msingi wa Kiakili. Walipochakachua uchaguzi uliopita America 'held its horses'... Kwa hili watazungumza na hii itajibu tuhuma sizizo na msingi zinazotolewa kila kukicha kwamba maandamano yanafadhiliwa kutoka nje. Hakuna asiyejua kwamba wananchi wa Tanzania wanavyutwa na hoja zinazowagusa zinazotolewa na Chadema. Asiyeliona/kulikubali hili ni Msaliti wa Wananchi au Mjinga.
 
Kama SIKWELI ambassador wa US ataongea hawezi kukaa kimya nchi yake ikitukanwa. Kama akikaa kimya bila kuwauliza CCM basi itakuwa ni KWELI . Kwenye mandamano siendi tena manake mimi niandamane bure wenza wale $$$. Ngoja tusubiri!
 
Kama ni kweli huyo Mzee amesema hivyo kwa nini vyombo vya Usalama havimtii nguvuni?
Its like unakiri hadharani umeiba then watu wanakuacha tu,duuuh,hii nchi ni ya ajabu na maajabu!!!!!
 
Munkari wa nini?...Tangu lini umeona capitalis party like CDM ikijali maisha ya walalahoi? Hawa wanasiasa wengi ni wezi tu huna haja ya kumtukana mtu kwa ajili ya wanasiasa usiowajua,You don't even know what kind of a party CDM is,are you a socialist or capitalist?...be open,theres no centrist party in this world.
You cant stay neutral(as in shift....gear) when the trainwreck is about to happen.

Tangu lini CCM ikawa socialist party? nijuavyo mimi CCM wamepoteza mwelekeo tangu 1991, matokeo yake wakaamua kujenga ubepari wa kikasino ambapo viongozi wake wamekazana kukusanya mtaji kwa njia zote haramu ikiwa ni pamoja na kupora raslimali za taifa, rushwa, ufisadi na nyingine unaweza kuziongeza wewe.
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.


Hauifahamu chadema, hawana cha kuiasi serikali, achanei kuwa waoga hivyo.....chadema kinakua na kinaweza kukamata nchi muda wowote ule kwa sababu ya lile wanaloliamini.
 
Hauifahamu chadema, hawana cha kuiasi serikali, achanei kuwa waoga hivyo.....chadema kinakua na kinaweza kukamata nchi muda wowote ule kwa sababu ya lile wanaloliamini.
Utashangazwa kuna watu hata hawajui maana ya kuhasi,uelewa wao hauwaruhusu kutambua kuwa tuko kwenye nyakati za tofauti.Eti CHADEMA watai hasi serikali,CHADEMA inaunda serikali?Hawa watu hamnazo kabisa.
 
Hauifahamu chadema, hawana cha kuiasi serikali, achanei kuwa waoga hivyo.....chadema kinakua na kinaweza kukamata nchi muda wowote ule kwa sababu ya lile wanaloliamini.

Mkuu;
Unapofanya mabadiliko nafikiri yanahitajika yawe yenye tija, na sio for the sake tu ya mabadiliko. To be sincere, sioni tofauti kati ya CCM na CHADEMA, japo siku za karibuni wameamuua kujifananisha zaidi kwa kujiita CDM. Wakiwa na tofauti ya 400.
 
Naamini huyu ndiye aliifanyia kazi hotuba ya Sumaye kwa umakini pale Sumaye alipodai kuwa ukitaka biashara yako ifanikiwe, jiunge na CCM. Ngawaiya anaficha kitu nyuma yake, yaani leo ndiyo kawa msafi wa kutamka kuwa walipewa hela na US kuvuruga amani. Alikuwa wapi kusema huo ukweli hata pale aliporudi kujiunga na CCM? Chadema isn't NCCR-Mageuzi na wala Mageuzi-NCCR si Chadema.

Kama alipewa pesa kuvuruga amani nchini kwake, na akiwa na akili zake timamu akazipokea ili achafue amani nchini kwake........basi atakuwa PU-MBWA-VUU wa hali ya kati.
 
Katika falsafa tunaambiwa "watu wanapenda kujielezea tabia zao kupitia kwa watu wengine." Mwizi akikuona umesimama sehemu ambapo yeye amezoea kusimama akifanya mawindo basi atafanya conclusion kuwa nawe upo mawindoni kwa sababu yeye huwa anafanya hivyo.

Kama Ngawaiya aliwahi kuchukua fedha alete vurugu nchini basi siwezi kumshangaa kwa mawazo anayowawazia chadema chama cha wasafi na wanaukombozi wa kweli. Cha muhimu alete ushahid sio maneno kama muimba taarabu.
 
Siasa za wajinga hizo. Kama Marekani inawapa cdm mbona ccm na kikwete siku zote wanapokea pesa za mikopo toka kwa donors toka Marekani? IMF na WB nani anachangia hiyo mifuko? Ujinga sio kosa lake ila watanzania wasiojua kusoma na kuandika ndio hapo tutawaona wakiingiza hisia zao. Hiki chama cha ccm mbona kinachukua muda kufa?
 
:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed:Huyu Ngawaiya **** tu hana jipya. Kumbukeni karibu wakuu wa wilaya watateuliwa anvizia uteuzi. Yeye alipopewa kama alivyokiri na mwenzake Mkuu wa nnji hii walikula hadi wakadhurika afya zao. kama hela hizi zitasaidia kuwang'oa mafisadi basi poooooaaa tu. Kaza uzi CHADEMA hadi kieleweke. Wanaovunjia nyumba wananchi wa TEGETA na JANGWANI mbona hmsemi wamepata wapi hela ya kuwapa umasikini wananchi ambao wamejijengea vibanda vyao leo vimepigwa chini tena usiku wakiwa wamelala. CCM lazima ife kwa mtindo huu:love::love::love::love::love:
 
Ngawaiya anatufanya sisi watanzania wajinga? Ni mara ya pili kusikia anafananisha Tz na nchi za Kiarabu akidai US ndiyo inayotoa hela ili nchi isitawalike! Kabla ya kujadili Tz, jiulize US ingeweza kutoa hela ili Hosn Mubarak aondolewe madarakani?, Au Ben Ali akimbizwe?

Hii inanipa tafsiri ya kuwa ana uelewa mdogo sana katika siasa za dunia. Kwa kigezo hicho, hasitaili kupewa nafasi kupotosha jamii yetu. Eti Kenya ilikuwa na vurugu kwasababu ya pesa ya US? Kwa maana nyingine US ilimwambia Kibaki na Kiviutu kuvuruga uchaguzi?

Upeo wa viongozi hawa ni kama ule wa Gaddafi. Badala ya kuona matatizo yaliko kwenye nchi zao na kuyatatua wao uishia kujilidhisha eti hizo kelele si za wananchi bali zinachochewa na nchi za magharibi.

Kupewa kwake pesa na Mrema siwezi kumkatalia, lakini kama nchi itakuwa na vurugu baada ya huu Mswaada unaopingwa na watu wengi. Je na hapa Ngawaiya atatwambia ni US imelipa pesa ili nchi iwe na vurugu? Au anamaanisha ile ya kulipa mishahara watumishi wa umma (wanasheria walioandaa mswada) wanaoliandalia giza taifa letu kwa manufaa yao binafsi.

TAFAKARI!
 
It doesn`t matter,tunachotaka ni Tanzania mpya na wala si tz yenye mafisadi,rushwa na umaskini mkubwa huku tukijifariji na amani,amani pasipo haki na maendeleo si kitu na amani haiji bila upanga.CDM kupewa pesa ni sahihi kabisa.

Sitaki Chadema wapewe pesa na wazungu ili sisi tujikomboe. Hao wazungu wanatarajia vipi kirudisha pesa zao? Kwa nini wanaingia garama hivyo ili sisi tujikomboe?

Sioni ni kwa nini tulipwe ndipo tujikomboe. Mimi nimejihusisha sana na harakati za kujikomboa lakini silipwi na sitaki nilipwe.

Kwa nini viongozi wa Chadema walipwe pesa kwa kazi ambayo tayari wananchi tunaifanya kwa nguvu na hiari yetu? Si ni utapeli? Si wakiingia madarakani watakuwa wanawajibika kwa wafadhili badala ya kwa wananchi, kama wanavyofanya ccm?
 
Sitaki Chadema wapewe pesa na wazungu ili sisi tujikomboe. Hao wazungu wanatarajia vipi kirudisha pesa zao? Kwa nini wanaingia garama hivyo ili sisi tujikomboe?

Sioni ni kwa nini tulipwe ndipo tujikomboe. Mimi nimejihusisha sana na harakati za kujikomboa lakini silipwi na sitaki nilipwe.

Kwa nini viongozi wa Chadema walipwe pesa kwa kazi ambayo tayari wananchi tunaifanya kwa nguvu na hiari yetu? Si ni utapeli? Si wakiingia madarakani watakuwa wanawajibika kwa wafadhili badala ya kwa wananchi, kama wanavyofanya ccm?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom