kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Zimejadili mpango wa kumuua Putin; Marekani yakiri uvujaji wa nyaraka za kijasusi ni jambo hatari.
Marekani imekiri kwamba uvujaji wa nyaraka za siri za Wizara ya Ulinzi wa nchi hiyo, Pentagon ni jambo hatari na kwamba suala hilo ni uvujishaji mkubwa wa taarifa za kijasusi.
Sambamba na hayo gazeti la New York Times limepata moja ya nyaraka za siri zilizovujishwa kuhusu vita vya Ukraine ambao unajadili machaguo manne ya kidhahania ya kuhitimisha vita hivyo ikiwa ni pamoja na kumuua Rais Vladimir Putin wa Russia.
John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Marekani ameviambia vyombo vya habari kuwa: "Kuvujishwa kwa nyaraka hizo za siri za Pentagon ni ukiukaji wa uwezo wetu wa kulinda taarifa za siri, na ndio maana tunalichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa."
Katika muktadha huo, Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, William Burns amesema, kuvuja kwa nyaraka za siri kutoka Wizara ya Ulinzi ni jambo la kusikitisha sana na kwamba Wamarekani wanapaswa kujifunza somo kuhusu jinsi ya kuimarisha hatua zao za usalama kwenye nyaraka kama hizo.
Mkurugenzi wa CIA amesema, "Ni uvujaji mbaya, na inasikitisha sana kwamba umehusu nyaraka zilizoainishwa kama zenye usiri mkubwa." William Burns amesema Serikali ya Marekani inalipa uzito mkubwa suala hilo. Amesema tayari wizara za ulinzi na sheria zinashughulikiia kashfa hiyo.
Maafisa wa Marekani wanafanya juhudi kubwa kusaka chanzo cha uvujaji wa nyaraka hizo za siri za kijeshi na kijasusi zilizosambazwa kwenye mtandao ambazo zinajumuisha maelezo marefu, yakiwemo yale yanayohusiana na ulinzi wa anga wa Ukraine na shirika la ujasusi la Israel (Mossad).
Wataalamu wa usalama wa nchi za Magharibi na maafisa wa Marekani wamesema wanashuku kuwa huenda mtu kutoka Marekani ndiye aliyehusika na uvujaji huo.
Maafisa wanasema upana wa maudhui zilizovujishwa katika nyaraka hizo za siri zinazohusu vita vya Ukraine, Uchina, Mashariki ya Kati na Afrika, unaonyesha kuwa zimevunjishwa na raia wa Marekani na sio nchi mshirika wa taifa hilo.
Kwa upande wake, gazeti la The New York Times lilisema limepata waraka wa kijasusi kati ya nyaraka hizo za Pentagon zilizovuja, unaoeleza mipango iliyoandaliwa kushughulikia hali ya dharura, mwaka mmoja baada ya kuanza vita nchini Ukraine.
Waraka huo unajumuisha uchanganuzi uliofanywa na Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani ambao unabainisha mambo 4 ya kidhahania ikiwa ni pamoja na mpango wa kuuawa Rais wa Russia, Vladimir Putin, mabadiliko ya uongozi wa vikosi vya jeshi la Russia, na mashambulizi ya Ukraine dhidi ya ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin.
Uvujishaji huo wa nyaraka za kijasusi na zenye usiri mkubwa za Pentagon unatajwa kuwa mkubwa zaidi wa masuala ya usalama tangu ule uliofanywa na WikiLeaks 2013, ambao ulijumuisha zaidi ya nyaraka 700,000, video na jumbe za kidiplomasia.