Ngawaiya: CHADEMA wanapewa pesa na Marekani kuchochea fujo

Yale yale mara Eu mara marekani ni mpaka nchi hizo zitakapoikatia serikali misaada ndipo athari za uzushi wao zitakapoonekana

Hilo la kukata misaada tayari mkuu muda tu unasubiriwa liwekwe bayana, kabla ya mwisho wa mwezi wa tano utasikia maneno ya wafadhili. Hili halijasababishwa na Chadema bali serikali kuaminiwa na kupewa pesa kupitia GBS halafu wanazitafuna kama mchwa bila kuchukuliana hatua.

CAG reports, reports na maagizo ya kamati za bunge zinazosimamia matumizi ya serikali zote zinapatikana mtandaoni. Donors HQ hawahitaji kuhabarishwa na mtu yeyote kuwaarifu nini kinaendelea hapa wakati wanapata taarifa mtandaoni. Viongozi wa nchi za wenzetu wana tabia ya kusoma, wa kwetu husubiri kuambiwa.
 
Naona wengi wanafikiri kuwa kuitowa CCM madarakani kwa nguvu ndio kutatuwa matatizo, hawaoni wala hawasomi kuwa huo ndio utakuwa mwanzo wa matatizo, wanioneshe nchi moja iliyotolewa serikali iliyopo madarakani kwa fitina yenye kukalika duniani hivi sasa.

Mkuu hapo kwenye red, CCM hawataondoka kwa fitna, wataondoka kwa sababu wameshindwa kuliongoza taifa la Tanzania na kuleta success inayolingana na resources tulizonazo.

Sasa kama wananchi watasema basi hatuwataki tena, hiyo sio fitna, ni wenye nchi hawataki mchwa kwenye shamba lao la mahindi.
 
Du huyu jamaa (Ngawaiya) angekamatwa mara moja atiwe ndani. Kwa kusema hivyo inamaana yeye aliwahi kuihaini nchi kwa pesa za wamarekani. Ah! inauma sana, majitu kama haya....Lakini naamini 'Freedom is coming tomorrow'
 
Kama gawaiwaya aliwahi kuzipikea si akamatwa au kuwa yuko ccm sasa? Lakini nini kazi ya usalama wa taifa? Au ndio wamemtuma aseme? Na walikuwa wapi wakati wakati world wanaifania ujasusi tz wakati adjusted structured program za 1986?

Hakuna fisadi kama Ngawaiya. General tyre wanamjua! Hawezi kukataa fedha huyu! Ngawaiya asidanganye watu. Kama aliambiwa na Mrema arudishe ni kwa sababu Mrema ni Mtanzania damudamu ambalo ni zao la mwalimu lililbakia ndo maana akakosana naye. Mrema anafanya kazi za kitaifa zaidi. Mtu wa usalama yule, Ngawaiya na utapeli wake asingeweza kufanya kazi na Mrema!
 
Nona mshaanza kumsema Obama,mara nyingi haya mambo hufanywa na special interest groups not neccessarily the government.Mfano angalia muswaada wa Uganda kuhusu gays.What I know ni kwamba,CDM is openly getting support from UK conservative party(Tories)
 
Katika wanafiki Tanzania ni huyu Ngawaiya. Nakumbuka aliwahi kuropoka Bungeni. Spika akamtaka athibitishe haraka akaomba msamaha. Ni kati ya wazee waliolelewa kimayai tangu utoto wakiwa wamangi hana lolote kwa nchi hata kijiji chake hajafanya kitu. Hali ya watanzania ni mbaya ikiwa kuna fedha za kuwafanya watanzania wajitoe kwenye matatizo zije tu. Naomba hata Uarabuni nao walete fedha kwa vyama vya upinzani tujikomboe. CCM imewekeza kwa mafisadi na wafanya biashara ambao welewa wao ni mdogo. CDM wamewekeza vyuo vikuu ambao ni wachambuzi na waelewa. Kuzima moto huu ni vigumu sana. Serikali itimize ndotoa wananchi vinginevyo CDM MWENDO MDUNDO.
 
Ipo siku mtawajua hawa chadema nia yao ni ipi baada ya nchi hii kutotawalika kabisa kama wao wanavyotaka endeleeni kuwaanini
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.
Wewe nimjinga kama huyo Jingawia lako, kama yeye alikuwa akipewa hizo pesa mbona hakutuambia wakati huo kama kweli ana nia njema na taifa unafiki mtupu na lazima tumshitaki adhibitishe madai hayo Foolish
 
Ipo siku mtawajua hawa chadema nia yao ni ipi baada ya nchi hii kutotawalika kabisa kama wao wanavyotaka endeleeni kuwaanini
kwa ufisadi wa ccm kwani hata sasa nchi inatawalika mkuu!?? au ni unafiki umejaaa tuuu!
Ona kikwete wanavyomuuza watu wake wakaribu.
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.
Wewe nimjinga kama huyo Jingawia lako, kama yeye alikuwa akipewa hizo pesa mbona hakutuambia wakati huo kama kweli ana nia njema na taifa? unafiki mtupu na lazima tumshitaki adhibitishe madai hayo!! Foolish!!
 
Naona wengi wanafikiri kuwa kuitowa CCM madarakani kwa nguvu ndio kutatuwa matatizo, hawaoni wala hawasomi kuwa huo ndio utakuwa mwanzo wa matatizo, wanioneshe nchi moja iliyotolewa serikali iliyopo madarakani kwa fitina yenye kukalika duniani hivi sasa.

Hivi mkuu ina maana Ethiopia sio nchi au haijui kilichotokea 1991 raisi aliposhindwa kuongoza nchi na wako salama mpaka sasa??
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.
Ushahidi uko wapi? Ngawaiya ni sawa na Tambwe Hiza. Ni desperados wanaotafuta pa kuemea ili siku ziende. Wanataka waonekane wao ni CCM zaidi kuliko hata waasisi wa chama chenyewe.Talk about being more catholic than the Pope!!!!
 
Mi nadhani it is another stupid trick to divert attention from important nationa matters.

Who is Ngawaiya hadi camera crew ya itv imfuate huko porini akiotesha miti, na mwenyewe anaongea kwa uhakika huku akiwa bize kama watu wanaoigiza sinema
Crap tricks of the corrupt party which will never get into our mind. They are trying to divert us from the new constution matters especially because Chadema leader have volunteered to make sure that Tanzanians participate in the discussion which the craps don't want!
 
Wewe nimjinga kama huyo Jingawia lako, kama yeye alikuwa akipewa hizo pesa mbona hakutuambia wakati huo kama kweli ana nia njema na taifa? unafiki mtupu na lazima tumshitaki adhibitishe madai hayo!! Foolish!!
Munkari wa nini?...Tangu lini umeona capitalis party like CDM ikijali maisha ya walalahoi? Hawa wanasiasa wengi ni wezi tu huna haja ya kumtukana mtu kwa ajili ya wanasiasa usiowajua,You don't even know what kind of a party CDM is,are you a socialist or capitalist?...be open,theres no centrist party in this world.
You cant stay neutral(as in shift....gear) when the trainwreck is about to happen.
 
Tumemuelewa Ngawaiya anamaanisha CCM inapewa hela na Marekani ili IWAGANDAMIZE, kuwaziba midomo watanzania na kuwaibia na kuwafilisi bila jasho! Wanaoenda Marekani na Ulaya kuomba omba kila siku tunawajua na Bajeti yao mpaka leo 50 years after independence asilimia kubwa inategemea wafadhili.
 
Naona wengi wanafikiri kuwa kuitowa CCM madarakani kwa nguvu ndio kutatuwa matatizo, hawaoni wala hawasomi kuwa huo ndio utakuwa mwanzo wa matatizo, wanioneshe nchi moja iliyotolewa serikali iliyopo madarakani kwa fitina yenye kukalika duniani hivi sasa.
Hehehehehe!!!! Hivi kuitoa CCM madarakani kwa nguvu ya uma au vinginevyo itakuwa ni fitina? Rwanda walimtoa Habyalimana. Hapakaliki? DRC walimtoa Mobutu.Hapakaliki? Uganda waliwatoa Amini na Obote. Hapakaliki?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom