Ngawaiya: CHADEMA wanapewa pesa na Marekani kuchochea fujo

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Amekaririwa na ITV kwenye taarifa ya saa tano na robo usiku huu

Jina lake kamili ni Thomas Ngawaiya, aliwahi kuwa mbunge wa Moshi vijijini kwa tiketi ya TLP, baada ya kukorofishana na Mrema akajisalimisha ccm

Ameongea kwa kutumia wadhifa wake wa Mkiti wa wazazi wa ccm mkoa wa Kilimanjaro

Amesema yeye na MREMA waliwahi kupewa pesa na serikali ya marekani ili wachochee vurugu tz watu wauane ili nchi ionekane ni ya machafuko kama kenya. Amesema alikuja pesa na kuanzisha maandamano sana Dar

Amesema baadaye Mrema alimwambia kwamba hizi pesa wanazopewa kuanzisha vurugu kwenye nchi Yao wakati wamarekani wamekaa kwao kwa amani hazifai. Wakawakatalia wamarekani halafu mrija wa pesa ukakatwa.

Amesema ni staili hiyo wamarekani wametumia kuleta uasi huko afrika kaskazini. Kwamba Hapa tz wamewapatia Chadema hizo pesa ili wachochee uasi Kama ule wa afrika kaskazini. Kwamba ndo maana Chadema "wanachochea vurugu" kwa sababu wameshalipwa pesa.

Alikuwa anaongea kwa kujiamini huku akieonekana kama yuko kwenye group activity fulani, sikuina vizuri, labda walikuwa wanapanda miti.
 
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.
 
Kwani wao CCM hawapati pesa kutoka nje. Kama hawapati wanazotumia zinatoka wapi kama siyo kuwanyonya wananchi? tumewagundua!!! Propaganda hizo hazifai!!!
 
Kama gawaiwaya aliwahi kuzipikea si akamatwa au kuwa yuko ccm sasa? Lakini nini kazi ya usalama wa taifa? Au ndio wamemtuma aseme? Na walikuwa wapi wakati wakati world wanaifania ujasusi tz wakati adjusted structured program za 1986?
 
Mi nadhani it is another stupid trick to divert attention from important nationa matters.

Who is Ngawaiya hadi camera crew ya itv imfuate huko porini akiotesha miti, na mwenyewe anaongea kwa uhakika huku akiwa bize kama watu wanaoigiza sinema
 
Acha wawatie vidole vya machoni hao Wamarekani na washirika wao kwa kubwabwaja hovyo, siku watakapochoka kusingiziwa na kuamua kufanya kweli waandae na mashimo ya kukimbilia.
 
Huyo Ngawaiya atoe ushahidi wake wenye vielelezo, mana sasa porojo bila vielelezo tumezichoka, Sophia Simba aliibuka na EU kuwa ndo wanawafund CDM sasa leo kaibuka huyu kibaraka mwingine na USA, watupe vielelezo vyenye uthibitisho!:bored:
 
muhosni ... hii post yako ni very strong evidence against the accusations of mr. Ngawaiya to the US government ... ukiitwa kutoa ushahidi usisite.. hii mipuuzi ya sisiem ambayo ni political failures isijeleta mtafaruku... hakuna mtanzania anayedanganyika ...

viva peoples power
 
Sasa kama Ngawaiya aliwahi kupewa hizo pesa akiwa NCCR ya Chadema amejuaje. Na kama kipindi chote hicho amekaa kimya tutajuaje ahakuzipokea na kunufaika nazo zikamfikisha hapo alipo. Nashangaa CCM kumuweka mwizi msaliti kama huyu kwenye uongozi maana hakuna uaminifu wowote.
Hana ushahidi wowote zaidi ya porojo...na CCM itang'oka either kwa pesa za marekani au pesa zetu wenyewe.
 
Huyu Ngawaiya anajaribu kuiga staili ya Tambwe Hiza kuropoka ili anajipenda na anakipigania sana chama. waliohamia ccm wanahitutumua waonekane wanaufahamu upinzani fika na wanauchukia na wanaweza kupambana nao!

Isipokuwa nadhani katika hili, hao vigogo wa ccm wenyewe nadhani watamtosa kwa sababu wanasafiri kwenda marekani kila mara na serikali inafadhiliwa sana na marekani.
Nobody in da gov wants to be seen to be pointing finger to da US. Vigogo wengi wa ccm ni mafisadi they don't want to risk exposure. Mkono wa US ni mrefu na una nguvu mno. Mara moja atavuliwa nguo hadharani, kama Chenge na EL na RA
 
  • Thanks
Reactions: Iza
Hii ni kweli. Kati ya chama chenye dalili ya kuiasi serilikali ni chadema. Na uasi huo wamepanga kuanzia Arusha, Ki
limanjaro na Mwanza. Hela zote zipo kwa ndesamburo. Njia za kuasi serikali ni kushawishi vijana na wanavyuo kama ilivyo Libya.

Ndoto za mchana ni jinamizi
 
Sasa kama Ngawaiya aliwahi kupewa hizo pesa akiwa NCCR ya Chadema amejuaje. Na kama kipindi chote hicho amekaa kimya tutajuaje ahakuzipokea na kunufaika nazo zikamfikisha hapo alipo. Nashangaa CCM kumuweka mwizi msaliti kama huyu kwenye uongozi.

mkuu alikuwa anatamba kwamba hizo pesa alizipokea sana na kuzila yeye na Mrema. Kwamba ccm wanampa mwizi uongozi, huko ndiko kwao, kwa hiyo Ngawaiya yuko nyumbani na ndo maana alikuwa anaongea kwa uhakika kwamba Hana wasiwasi anatia chama chake aibu na msukosuko wa kidiplomasia
 
Amekaririwa na ITV kwenye taarifa ya saa tano na robo usiku huu

Jina lake kamili ni Thomas Ngawaiya, aliwahi kuwa mbunge wa Moshi vijijini kwa tiketi ya TLP, baada ya kukorofishana na Mrema akajisalimisha ccm

Ameongea kwa kutumia wadhifa wake wa Mkiti wa wazazi wa ccm mkoa wa Kilimanjaro

Amesema yeye waliwahi kupewa pesa na serikali ya marekani ili wachochee vurugu tz watu wauane ili nchi ionekane ni ya machafuko kama kenya. Amesema alikuja pesa na kuanzisha maandamano sana Dar

Amesema baadaye Mrema alimwambia kwamba hizi pesa wanazopewa kuanzisha vurugu kwenye nchi Yao wakati wamarekani wamekaa kwao kwa amani hazifai. Wakawakatalia wamarekani halafu mrija wa pesa ukakatwa.

Amesema ni staili hiyo wamarekani wametumia kuleta uasi huko afrika kaskazini. Kwamba Hapa tz wamewapatia Chadema hizo pesa ili wachochee uasi Kama ule wa afrika kaskazini. Kwamba ndo maana Chadema "wanachochea vurugu" kwa sababu wameshalipwa pesa.

Alikuwa anaongea kwa kujiamini huku akieonekana kama yuko kwenye group activity fulani, sikuina vizuri, labda walikuwa wanapanda miti.
childish!
 
Du so now its JK against Obama (ligi itakuwa tamu sana)-CCM vs Obama teteetetetetet. Waacheni wafu wawazike wafu wenzao
 
Huyu jamaa analeta utani huyu anamshika simba sharubu... jamaa wakiuliza tu Vasco da Gama anamkana na kuwakabidhi wamchukue waende nae.... anafikiria tz ni sawa na cuba au venezuela... subiri niandike email sasa hivi kuumuuliza barozi wa marekani kama hayo madai ya huyu jamaa ni ya kweli, tumechoka ni hizi propaganda za kitoto!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom