sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Tamaa ni moja ya sifa kuu inayowatafuna vijana wengi sana hasa wenye kupenda vitu vyenye gharama kuzidi uwezo wao.
Sikuhizi kwenye makundi mengi ya vijana ili uonekane kijana wa kisasa inaaminika inabidi uwe na simu nzuri zenye brand kubwa kama iphone, Samsung, Google pixel, Nokia, n.k.
Kijana wetu kadakwa kwa kununua simu ya wizi na sasa yupo Polisi.
simu aliinunua mwezi wa pili kwa bei mteremko laki 4 , dukani ilikuwa laki 9,
Kwa bahati nzuri mwenye simu hataki mambo yafike mbali, yeye anachotaka ni pesa tu kesi inaisha.
Shilingi milioni 1 ndio inahitajika kumnasua huyu ndugu na hapo tunashukuru mwenye simu anahisi aliibiwa kwa kuisahau simu mahala, Ingekua vinginevyo kwamba aliibiwa na vitu vingine, kujeruhiwa au hata angeamua tu kudanganya ili kumtia adabu huyu ndugu yangu basi si ajabu angehitaji pesa nyingi ama ndugu kwenda jela miaka 20.
Siku hizi kuna ofisi zimejazana kibao za wanasheria / attorneys, ni hawa ndio tunaowatumia kutuandalia mikataba ya kisheria tunapouziana magari, mashamba, nyumba, n.k. hivyo kama unataka kununua simu iliyotumika hata kama ni ya mjomba wako hakikisha mnauziana kwa mkataba.
Wanasheria watawaandalia mkataba wa mauziano wenye taarifa za simu muhimu kama Imei, taarifa za muuzaji na mnunuzi, malipo, n.k. baada ya hapo kila moja atasaini na kupewa nakala ya mkataba, lolote likitokea jua kwamba sheria inakulinda kupitia mkataba.
ni heri umpe attorney elf 30 kwajili ya mkataba kuliko kukamatwa uchi huna nyaraka yoyote ya kuthibitisha unamiliki simu kihalali, utaingia gharama kubwa sana ama kwenda kuozea jela.
Mchango wa wadau, rafiki yake kafungwa miaka 30 kuuziwa simu iliyoporwa na kumuua mmliliki
Rafiki yangu mmoja yupo jela baada ya kuhukumiwa miaka 30 tokea 2020. Alinunua simu ambayo baada tu ya kuanza kuitumia ilikuja kufahamika iliporwa pamoja na vitu vingine na wakati wa uporaji mwenye mali alipigwa na kufariki wiki moja baadae.
Bahati mbaya sana hakumfahamu vyema aliyemuuzia maana alidakishwa tu kijiweni na mtu asiyemjua na yeye akapachika line yake. Hivyo alituhumiwa kwa mauaji ya kukusudia na uporaji.