Mawimba
Senior Member
- Apr 29, 2013
- 155
- 158
Habari zenu wanaJf, poleni na miangahiko yakusukuma gurudumu la maisha. Napenda nitangulize radhi kwenu kwa matatizo ya kiuandishi yatakayo jitokeza katika uandishi wangu.
Ndugu zangu kama nilivyo taadharisha hapo juu. kunawizi unaendelea Na Ndugu yangu kakutana na hii adha.
Tukio lenyewe lilivyokuwa...
siku ya tukio Jamaa yangu akiwa katika shughuri zake za kila siku majira ya saa 8 mchana akakutana na vijana wasajiri laini. Wakamueleza wanasajiri laini na wanabadilisha mfumo kutoka 3G kwenda 4G, kutokana na changamoto ya mtandao wa kijiji anachoishi akavutiwa na huduma ya Kuamishwa kwenye 3G Kwenda 4G.
Akawaomba wasaidie kwa hilo. Wakachukua simu yake wakatoa laini wakaiweka kwenye simu yao wakafanya yakufanya Wakamwambia tumemaliza teyari umeshahamishwa hivyo Hakikisha huduma zako za kifedha ambazo zipo kwenye hii laini. Akachukua simu Akaingia kwenye menyu ya tigo Pesa ilipofunguka Hakuangalia hata salio akakata kisha akaingia kwenye menyu ya benki akaingiza namba ya siri Ilipofunguka hakufanya chochote akakata akawaambia nimejiridhisha teyari (kipindi anafanya hizo shughuri alijitenga nao akawa peke yake) wakachukua hile simu yao wakatoa laini wakamkabidhi mwenye akairudisha kwenye simu yake, akaachana nao akaenda kuendelea na shughuri zake za kila siku.
saa 2 usiku akapata mesegi kutoka benki ikionesha ametuma pesa Milioni mbili na laki tano kwenda kwenye namba ya simu.
kipindi anatafakari mesegi zikaingia mesegi zingine zikiwa na miamala mingine, Akashtuka akapiga simu Tigo wakamwambia awapigie wabenki husika Akafanya hivyo lakini hakuwapata Ikabidi aende benki kuzuia huduma kwenye ATM.
Siku iliofatia akaenda Benki kufuatilia na kulalamika Akapatiwa barua aende polisi lakini nao wanafutilia kwenye kitengo cha Fraud.
lakini polisi waliomba taarifa ya IMEI namba ya kifaa kilichowezesha muamala Hile benki wakakataa kutoa.
Mteja akalalamika kwenye Benki wanampa maneno yakusubiri Hadi sasa miezi minne Dana dana tu zimekuwa.
hili tatizo ni wazi hizi baadhi ya benki zetu katika mifumo ya huduma za kibenk Mkononi Usalama wake ni mdogo.
au ni wafanyakazi wa hizi benki wanahusika kuwezesha huu uhuni.