Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 14,585
- 25,668
Mbona USA watengeneza ndege hawamiliki ndege kama tumeshindwa biashara ya korosho, madini na utalii huko kunakohitaji utaalamu sio siasa hatuwezi kufanikisha msijidanganye ..Sasa hao wanaotaka kuanza kujadili; wanao huo uelewa wa jinsi gani mashirika ya ndege yanaendeshwa? Kuendesha shirika la ndege sio sawa sawa na biashara ya kuuza nyanya, ambayo unanunua "stock ya nyanya" asubuhi, baada ya siku mbili au tatu unaweza kupiga hesabu umepata faida kiasi gani.
Ndege ni tofauti; unanunua ndege leo - inabidi uanzishe route mpya; uwe na mikakati ya bei, masoko ili kuweza kupata abiria. Na tatizo hao abiria ni lazima wakuamini pia kama hilo shilika liko reliable; kabla hawajaanza kulitumia. Hiyo yote inachukua muda. Ndio maana mashirika ya ndege huwa yanakuwa na muda waliojiwekea "PLANNED LOSSES". Kipindi ambacho wanategemea watakuwa wanapata hasara kuelekea kwenye faida.
Hivyo kutegemea ATCL iwe imepata faida ndani ya miaka 3 au 4 ya kujiendesha, hiyo sio sawa. Muhimu ni kuangalia hiyo hasara wanayoipata; inapungua??? Inaleta matumaini kuelekea kwenye faida kwenye miaka ijayo??? Na hiyo pia iangaliwe kwa pamoja na contribution yake kwenye maeneo mengine ya uchumi; ikiwemo utalii.
Kuhusu kubinafsihwa kwa TRC - hapo watuambie tu kama kuna janja janja za kuanza kutaka kujiuzia hilo shirika jipya na SGR yake. TRC ilishabinafsishwa wakati fulani; kwa wale wahindi; sijui walikuwa wanaitwa RITES???? Nini kilitokea???? Nina hakika Spika wa sasa nae alishakuwa Mbunge wakati ule?? TRC si ilikwisha kabisa mpaka serikali ikaamua kulichukua tena kwa asilimia 100??? Mbona hao RITES hawakujenga SGR??????
Mwekezaji Binafsi yeyote anakuja kwa kuangalia kwa upana maslahi yake binafsi. Hiyo ni hatari kwa hii miundombinu mikubwa ambayo inategemewa kuwa ndio "lifeline" ya Uchumi wetu. Ndio maana nchi zilizoendelea; miundo mbinu mikubwa ambayo ndio inachochea kukua kwa uchumi; inamilikiwa na serikali mpaka sasa. Na hiyo ikiwemo Bandari; Reli na Mashirika ya Ndege.