Luhaga Mpina: Hakuna hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka Ripoti ya CAG itolewe Machi 2023

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Luhanga Mpina akitoa mchango wake amesema, amesoma taarifa ya CAG mwaka 2021, amesoma majumuisho ya majibu ya serikali na mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG, hakuna sehemu kwenye majumuisho ya mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG inayoonesha hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka Ripoti ya CAG itolewe Machi 2023.

Akiongez kuwa, aliwahi kusema kuwa tumepigwa zaidi ya Trilioni 30 katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 na leo anasisitiza ni zaidi ya trilioni 230, na kwamba hayo yanathibitiswa na maneno ya FIU ambayo inasema zaidi ya trilioni 280 zimehamishwa ndzni na nje nchi na kati ya hizo trilioni 56.6 zimehamishwa fedha taslimu kupitia mipakani na maeneo mengine, trilioni zingine 222.81 zimehamishwa kupitia njia ya mtandao.

Mwigulu akitoa taarifa kutetea upotevu wa matrilioni akapigwa na kitu kizito
Mpina akahoji, kama nchi hii masikini zinaweza kuwa na taarifa shuku trilioni 280 usalama uko wapi?
 
Mhe. Mpina alitoa ushahidi hadharani jinsi hao waheshimiwa walivyohusika na ubadhirifu wa fedha za SGR kutokana na ripoti ya CAG. Kama ushahidi upo mbona Mamlaka iliyowateua haijawachukulia hatua?
 
Samia sio kiongozi, ni mchangamshaji tu anayepitisha muda, kwa hili wala sina shaka nalo.

Inashangaza sana, mtu anajitokeza kufichua maovu kama haya, ajabu yeye yupo kimya tu kuwakumbatia kina Mwigulu waliofeli.

Naamini hili linasababishwa zaidi na upeo wake mdogo wa kuchambua mambo, ni rahisi sana kudanganywa, ndio maana anaona bora abaki na waziri wake anayemdanganya, kuliko kumuamini mbunge anayemuamsha usingizini.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hii ndio awamu imefanya ufisadi na ujambazi kushinda zote lakini wale chawa wako kimya hawaongei zaidi sana wanazidisha mapambio ili kuzima sauti ndogo inayofichua maovu ya bibi na wajukuu zake, vina mwanzo lakini vina mwisho pia
 
Me nadhani kuna watu wanafahamu kila kitu na wanaweza weka mambo yote hadharani ila wanahofia usalama wao maana wapigaji wananguvu kubwa kimalaka na kifedha na roho mbaya hivyo wako tayari kufanya lolote kustili maslahi yao hivyo bila uhakikisho wa usalama binafsi juu kufichua hadha hizi hakuna anaeweza hatarisha maisha yake kirahisi amini nawaambieni.
 
Salaam, Shalom!

Mawaziri hawa katika Riport ya CAG imewagusa waziwazi.

Mnasubiri hadi nini kitokee ndipo waondoshwe?

Karibuni🙏
 
Kama Bodi ya TRC ilivunjwa kwa sababu ya ubadhirifu huo wa SGR mbona CEO wa TRC bado anatamba mitaani tu.
 
Luhanga Mpina akitoa mchango wake amesema, amesoma taarifa ya CAG mwaka 2021, amesoma majumuisho ya majibu ya serikali na mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG, hakuna sehemu kwenye majumuisho ya mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG inayoonesha hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka Ripoti ya CAG itolewe Machi 2023.

Akiongez kuwa, aliwahi kusema kuwa tumepigwa zaidi ya Trilioni 30 katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 na leo anasisitiza ni zaidi ya trilioni 230, na kwamba hayo yanathibitiswa na maneno ya FIU ambayo inasema zaidi ya trilioni 280 zimehamishwa ndzni na nje nchi na kati ya hizo trilioni 56.6 zimehamishwa fedha taslimu kupitia mipakani na maeneo mengine, trilioni zingine 222.81 zimehamishwa kupitia njia ya mtandao.

View attachment 2802651
Mwigulu akitoa taarifa kutetea upotevu wa matrilioni akapigwa na kitu kizito
Mpina akahoji, kama nchi hii masikini zinaweza kuwa na taarifa shuku trilioni 280 usalama uko wapi?

Is why tunahitaji katiba mpya. Kwasababu likija suala la kuwajibika kwa kingozi wanafichana.
Lama nchi hatuwezi kundelea hivi
 
Tunaitaka Mamlaka ya uteuzi ichukue hatua stahiki siyo kuwaonea vidagaa kama Mkurugenzi wa Igunga ambaye kwa sasa ana kesi ya uhujumu uchumi kule Kigoma.
 
Back
Top Bottom