Wabunge wa Hayati Magufuli wanaopanga kuleta sintofahamu Bungeni mnatakiwa kutambua ufisadi alifanya aliyewaingiza Bungeni

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
CAG afichua Serikali ya Magufuli ilivyoisababishia taifa hasara ya Sh 1.7 Trilioni mradi wa SGR

Ripoti mpya ya CAG iliyotolewa Aprili 6, 2023, yasema Serikali ya Awamu ya 5 ilivunja sheria ya nchi kwenye utoaji wa kandarasi ya reli llikubali masharti mabovu ya Benki ya StanChart kuwapa kandarasi Waturuki kwa gharama ya juu bila tenda ya wazi ya ushindani.

Serikali ya Awamu ya Tano ya Hayati Rais John Magufuli ililingizia taifa hasara ya Dola za Marekani milioni 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR baada ya kukubali masharti mabovu ya mkopo wa benki ya Standard Chartered.

Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2021/22 iliyotolewa juzi na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilisema kuwa hasara hiyo kwa taifa ilitokana na Serikali ya Magufuli kukubali masharti ya ajabu ya mkopo wa kibiashara wa Dola za Marekani Bilioni 1.46 kutoka kwa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa SGR uliotolewa mwaka 2020.

Moja ya masharti ya mkopo huo ni kuwa Serikali ivunje Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutoa kandarasi mbili za ujenzi wa reli ya SGR kwa kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkezi Insaat VE Sanayi As bila zabuni ya wazi ya kushindanisha kampuni nyingine, Serikali ya Magufuli ilikubali masharti hayo ya ajabu kwa kutoa kandarasi kwa waturuki kinyume cha sheria za nchi.

CAG alibaini kuwa gharama za ujenzi wa kipande cha reli ya Makutupora-Tabora (Lot 3) iliongezeka kwa Dola za Marekani milioni 1.3 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3) kwa kila kilomita wakati gharama ya ujenzi wa kipande cha reli ya Tabora-lsaka (Lot 4) illiongezeka kwa Dola milioni 1.6 (Shilingi Bilioni 3.74) kwa kila kilomita.

"Shirika la Reli Tanzania (TRC) halikutumia njia ya ununuzi ya ushindani katika ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha tatu na cha nne na kusababisha kuongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 1.3 na milioni 1.6 kwa kilomita mtawalia ikilinganishwa na mikataba ya awali," alisema CAG Reli ya Makutupora-Tabora yenye urefu wa kilomita 368 inajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani Bilioni 1.9, wakati kipande cha Tabora-lsaka chenye urefu wa kilomita 165, kinajengwa kwa gharama za Dola za Marekani milioni 900.

Maana yake ni kuwa taifa limeingia jumla ya hasara ya Dola za Marekani 742.4 (zaidi ya Shilingi trilioni 1.7) kwenye vipande hivyo viwili vya reli, "Mapitio yangu ya njia za ununuzi zilizotumika katika ununuzi wa mkandarasi wa reli ya kisasa (SGR)
kipande cha 3 na 4 yalibainisha kuwa Benki ya Standard Chartered ambako
Serikali ilipata mkopo iliweka masharti kwamba ingekubalijukumu la kuwa Mratibu wa Kimataifa, na Wakala Kiongozi Aliye na Mamlaka kupanga ufadhili na mkopo kwa Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) tu kwa masharti kwamba kampuni ya Yapi Markezi iteuliwe kama Mkandarasi," alisema CAG kwenye ripoti hiyo.

"Wizara ya Fedha na Mipango (MOFP) ilikubali mkopo huo kwa masharti
yasiyofaa kutoka Benki ya Standard Chartered kupitia barua yake yenye kumbukumbu namba PST/GEN/2021/01/55.Wakati barua hiyo inaandikwa, Doto James ndiye aliyekua Katibu Mkuu wa Hazina (PST) kwenye Wizara ya Fedha na Mipango.

CAG amebaini zaidi kuwa TRC iliamua kuchagua njia ya kutoa zabuni kwa njia
mzabuni mmoja licha ya ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa
Ununuzi wa Umma (PPRA) na Bodi ya Zabuni, ambayo iliishia kuigharimu
serikali fedha zaidi, ambayo ingeweza kuepukwa.

"Ni maoni yangu kwamba, hakuna mfadhili anayeweza kuitaka Serikali ya
Tanzania kumpa mkataba mkandarasi pasipo kuwa na uwazi, ushindani, usawa na haki kwa wakandarasi wote wenye sifa na wanaostahili katika mchakato wa ununuzi," alisema CAG.

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa baada ya Serikali ya Magufuli kukubali masharti yasiyofaa ya kuwapa kandarasi ya Lot 3 na Lot 4 kwa Yapi Merkezi bila tenda ya wazi ya ushindani, Waturuki hao wakaongeza gharama ya ujenzi kuliko kawaida na kuliingizia taifa hasara kubwa.
 
Kwa hiyo baada ya Samia na kundi lake kuiba na kuimaliza hazina!

Sasa ndio mnatafuta wa kumuangushia zigo?

Huyo CAG si nae ndoyo sehemu ya wezi wakuu sasa hivi!

Ebu kama mnabisha serikali ikubali wakaguzi wa taasisi huru kutoka nje ya nchi waje wakatr mzizi wa fitna!

Mtaaibika mpaka mkimbie nchi.
 
JPM hachafuki kirahisi hivyo japo hawezi jitetea ila hamuwezi kumchafua. Itatuchukua miongo kadhaa kupata jembe la namna ile.
Ni kweli alikosea lkn hamfikiii huyu wa miaka 2 na nusu na kaboronga vyakutosha
 
Tuambie na Mabehewa na Vichwa vya Treni basi mzee baba vyenyewe vilinunuliwa kwa aina gani ya tenda?

Maana nijuavyo navyenyewe vilinunuliwa kupitia tenda ya mzabuni mmoja (single source) na kuliingizia Taida hasara ya Dola za Marekani Milioni 215.

Be objective mzee, huu mchezo hautaki hasira. 🤫🤫
 
"Akili mbovu na wiziwizi tu"
Utakopaje mikopo ya kibiashara ukaiingiza kwenye projects za serekali ambazo hulipwa kwa muda mrefu 15yr-50yrs.😇😇😇
 
Back
Top Bottom