Nchi inakumbwa na hofu kubwa ya njaa na kupanda sana kwa bei za vyakula. Rais aandae wananchi kukabiliana na hali hii na ashugulikie kwa udharura

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Hali ni mbaya. Kuna maeneo watu wamechanganyikiwa hawajui walime nini.

Naona Serikali na viongozi wako bize na uchaguzi 2025.

Natamani Serikali itoke adharani kufanya Mambo yafuatayo:

1. Kuhamasisha ulimaji wa mazao ya muda mfupi na yanayostaimili ukame kama mtama, mahindi na maharage.

2. Kuingilia Kati mfumuko wa Bei kwa kuruhusu uagizaji wa mahindi na mchele kutoka brazili na nje ya nchi bila ushuru au mashariti yoyote ya kibiashara isipokuwa ya kiafya na Ubora.

3. Kuwahakikishia wananchi kuwa hakuna mtu atakufa njaa ili waondoe hofu na wachape Kazi.

4. Kutoruhusu kutoka nje kwa nafaka.

Najua viongozi wanaweza wasieleHalhali halisi waje vijijini watu wamekata tamaa kabisa.
 
Climate changes mabadiliko tabia nchi kuna maeneo ni maarufu kwa kilimo hayajapata mvua toka Sept 2021 kuna maeneo yamepata mafuriko makubwa hii ni priority area hatusikii mikakati yoyote inayopangwa kukabili hili janga hata kama hipo haipewi uzito
 
Watu wako bize na 2025
 
mkuu kwa huku kanda ya magharbi mvua hasa katavi kigoma sumbawanga,songwe mvua inajitahidi hivyo laabda tutawaokowa kwa mazao japo sijui kama kuna uwezekano wa kulisha nchi
 
Hali ni mbaya. Kuna maeneo watu wamechanganyikiwa hawajui walime nini.

Naona Serikali na viongozi wako bize na uchaguzi 2025.

Natamani Serikali itoke adharani kufanya Mambo yafuatayo:

1. Kuhamasisha ulimaji wa mazao ya muda mfupi na yanayostaimili ukame kama mtama, mahindi na maharage.

2. Kuingilia Kati mfumuko wa Bei kwa kuruhusu uagizaji wa mahindi na mchele kutoka brazili na nje ya nchi bila ushuru au mashariti yoyote ya kibiashara isipokuwa ya kiafya na Ubora.

3. Kuwahakikishia wananchi kuwa hakuna mtu atakufa njaa ili waondoe hofu na wachape Kazi.

4. Kutoruhusu kutoka nje kwa nafaka.

Najua viongozi wanaweza wasieleHalhali halisi waje vijijini watu wamekata tamaa kabisa.
Samia yeye hajali kuhusu maisha ya masikini...yupo bize na urais
 
Najua fika hii haitachukua muda mrefu tutazoea huu mfumuko wa bei. Kwa sasa maji tu ndio hayajapanda bei.
Mo tambi 1200 sasa zamani 1000
Dawa za meno zote zimepanda
Lita ya mafuta 6000 na hauna kipimo cha 500 tena
Mchele chenga kg 1 ni 1500 toka 700.

Pamoja na yote viongozi wa serikali wanashangaa na watanzania wanashangaa hakuna anaeweza kuchukua hatua kama serikali iliyopita, kula tunataka na kuishi tunataka hatuwezi kususa

Ombi langu kwa watanzania hii kwa muda tu,tuvumilie muda si mrefu tutazoea mfumuko huu.
 
Ruvuma inakolisha tz huku saiz ni neema mvua ipo ya kutosha ishu mbolea zipo juu ila baadhi ya mashamba mahindi kalibu yanakomaa,na wengine ndio wanapanda,selikari ipunguze mbolea
 
Unga wa ngano kitoka 1200tsh 17/march 2021 mpaka 1900tsh leo hii 13/feb 2022 alafu kuna mthenge mmoja utasikia anasema eti mama anaiponya nchi.
 
Back
Top Bottom