Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Upon mfumumuko mkubwa wa za bidhaa nchini, maeneo yaliyoathirika Zaidi ni nishati na chakula.
Kupanda kwa bei hizi kulipaswa kuwa agenda za kujadiliwa kabla ya kujadili siasa. Mtu mwenye njaa ni mwepesi kurubuniwa akawa mwovu lakini aliyeshiba siku zote ukumbuka mkono uliomlisha na kuulinda usidhurike.
Wamachinga wanatoka kundi la watu wa vipato vya chini lakini walipokutana na Mhe Rais walijikita kwenye hoja zakitajiri. Hakuna alimweleza Mhe. Rais Kwamba watu Wana njaa na wakiwa na njaa nivigumu kujadili nao kesho yao maana wakati wanaugulia maumivu ya njaa wanashuhudia majirani zao waliopo nafasi za juu wakila na kusaza. Kwanini machinga awakuona mfumuko wa bei kama agenda kwenye kikao Chao?
Viongozi wa dini wanaongoza nafsi zetu ziweze kwenda Mbinguni. Katika Hali ya kibinadamu tunahitaji watu walioshiba ndio tuwape neno la Mungu na kupanga nao mipango ya Mbinguni. Maana yake Nini, hakuna kiaongozi wa dini ataongoza Misa masaa manne au zaidi huku akijua wazi familia yake Haina msosi. Hakuna kiongozi wa dini atazunguka kutoa huduma ya kiroho wiki nzima bila kuacha chakula nyumbani. Nilitegemea viongozi wa dini wamwombe Rais aeleze ana mkakati Gani wa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa?
Machief wengi ni watu wa Hali ya chini, wanaishi vijijini na wanaona Hali halisi ilivyo. Kipaombele kwao kilipaswa kumwambia Mhe Rais tusaidie tujue Kuna mpango gani wakupunguza kupanda kwa bei ya bidhaa? Kwa Bei hizi tutaweza kula? Tukila tutaweza kujenga nyumba za bati?
Kwanini bati lipande kutoka shs 22,000 Hadi 30,000 ndani mwaka mmoja na hakuna tamko la serikali kuhusu mfumuko huu? Haya maswali na mengine hakuna aliyeuliza maana yake Mhe. Rais anaamini sisi wananchi tumeshiba na tunaendelea kufanya maendeleo kumbe tunachoweza kufanya kutumikia tumbo.
Kwa Hali hii ndipo ninapojiuliza kwanini hakuna aliyezungumzia kupanda kwa kasi Kwa Bei ya ;
1. Vyakula
2. Mafuta ya kupikia
3. Vifaa vya ujenzi kama saruji,nondo,matati na marumaru
Nani amejiuliza umuhimu wa nondo kwenye miradi mikubwa inayojengwa? Kama nondo imepanda kwa kiasi kiki hivi Bado tunaamini gharama za miradi zitabaki palepale? Je kama kuna hujuma inafanywa Kwa wenye viwanda vya nondo kupata asilimia flani Nani atadhibiti kama viongozi wa dini wasipopata maono kama haya nakumweleza Rais?
Cement inatumika kwenye miradi yote mikubwa na imepanda mara dufu means gharama za miradi nazo zinapanda relatively to price ya malighafi, kwanini cement ipande Kwa kiasi hiki? Hakuna sarbotage hapa? Nani ananufaika na hii sabortage? Kama viongozi wa dini watashindwa kupata maono haya nakumweleza Mhe. Rais Nani atamsaidia Rais kupambana na kupanda kwa hizi gharama?
Nadhani nikiamini Kwamba hizi ni hujuma nitakuwa sahihi na nikiendelea kuamini Kwamba wanaokutana na Mhe Rais wanatumia muda mwingi kumsifia kuliko kumshauri ntakuwa sahihi. Kama wao waliopewa nafasi ya kukaa na mfalme wameshindwa kumsaidia naomba Mimi binafsi Beatrice Kamugisha nimsaidie Mhe. Rais Kwamba Kuna maswali mengi kwenye mfumuko wa bei, atume vyombo vyake vikafanye utafiti na wampe majibu ni kipi kimepelekea haya na Je hakuna watu au makampuni yanatumia miradi ya kimkakati kujipatia faida kubwa? Bei ya cement, bati na nondo ingekuwa chini naamini tungejenga madarasa mengi zaidi ya tuliyojenga na tusingeona picha za watoto wakikaa chini.