Nawezaje kuwazuia paka kuingia kwangu?

Nawezaje kuwazuia paka kuingia kwangu?

Mbwambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
625
Reaction score
95
Jamani ninaomba msaada wa mtaalamu wa wanyama ili anisaidie kitu gani kitawazuia paka wa jirani kuingia kwangu.

Paka hawa huingia kwenye fence yangu na kukesha wakilia nyuma ya nyumba yangu, imekuwa ni kero kiukweli.

Naomba msaada nitamlipa akinifanikisha.

Asanteni kwa ushauri

Kwa wataalam wa umeme, nimekuwa mara nyingi paka wanavamia banda la kuku wanakula, nimefuga mbwa lakini wamekuwa wakitoa wire za banda na kupita, sasa Natala ushauri kwa wana umeme, paka anapigwa shock? Kama ndio, nafanyaje kuwatega?
 
Hahaa kumbe tuko wengi,mimi kwangu mpaka watoto wameanza kucheza nao yaani nimepiga hao paka hawasikii imefikia hata wakibeba mimba wanazalia kwangu.Ngoja nifanyie kazi huo ushauri wa BADILI TABIA naona unaweza kufanya kazi.
 
Last edited by a moderator:
Achana na utaalamu wa Bagamoyo....Tafuta mbwa watakimbia wenyewe. Hata kama hatakuwa mkali kwa paka wewe mfundishe kuwakimbiza. Akiwaona mwambie KAMATA.
 
Mkuu, umeniwahi kwa jibu hilo. Kwangu paka ni historia baada ya kufuga mbwa. Siku za mwanzo paka walikuwa wabishi. Tulikuwa tunakuta mizoga asubuhi mbwa wamefanya kazi yao.

Na hiyo ndio dawa yao tu kwani hakuna namna nyingine.
Ni sawa sawa na panya wewe fuga paka , mchezo kwisha kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Mbwa ndio dawa ya paka akuna kingine watakimbia wote
 
Nyunyiza pilipili ya unga uani kwako sehemu zote wanazopitia na wanazopenda kufanya vurugu.
 
Ww inaonekana unatabia ya kumwagamwaga chakula hovyo ndio maana manyau yanaingia kwako.
 
wawekee vipande vya samaki nguru... wakishavitafuna tu hawatokuja tena ..
 
ushauri wa kufuga mbwa ni mzuri but vipi kwa watu wanaoogopa mbwa?? mbwa atanifukuzia wageni na kelele tu
 
Ushauri wa bure: wakianza kulia wewe toka nje kinyume nyume ukiwa uchi hadi sehemu walipo kisha hakikisha unaj.mba kwa sauti kuu hawatarudi tena. cc ambiere mshana jr

Hahahahaaaaaaa kama ni paka wa kishirikina weka mfupa au kinyesi cha kiti moto hutawaona tena
 
Last edited by a moderator:
Aiseeeee mie niliwawekea hadi sumu hawakufa...
Tatizo popo, kunguru, njiwa wamejaa
 
Mapaka ya uchawi hayo. Tafuta mtaalamu. Mbwa hawawezi fukuza wachawi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom