Mkuu wangu nakubaliana sana na wewe toka mwanzo isipokuwa nilichoitaka kusema ni kwamba ulijaribu kutolisema wazi kwamba mbegu ya matatizo yetu ni AFYA kuwa biashara.Mkuu Mkandara,
Ukinisoma between the lines, utabaini kwamba mimi na wewe tunaongea kitu hicho hicho. Kwa mtazamo wangu, lugha zetu sawa, inawezekana tunachopishana ni 'lafudhi' tu. Vinginevyo, nia yangu ilikuwa sio zaidi ya ile iliyolenga to 'stimulate' a debate juu ya jambo hili, tuweze kuliangalia tatizo hili kwa undani zaidi. In that line, nikawasilisha takwimu za sekta ya afya kama zilivyo, ili kwa pamoja tusaidiane kubaini tatizo lipo wapi, na kupendekeza suluhisho la kudumu. Kwa kweli, sijawa as subjective katika maelezo yangu ya awali kwani - sijatetea sekta binafsi, sijatetea sekta ya umma, na wala sijatetea sekta ya NGO, zaidi ya kuelezea hali halisi kama ilivyo, na kumalizia kwa maswali.
Lakini kuna vitu viwili tu ambavyo ningependa kuvijadili, kama majibu yangu kwa hoja zako.
1. Kwanza ni kuhusu hoja yako kwamba "Afya ni Biashara." Nimeipenda hoja hii, kwani katika thread yangu nyingine, nilizungumzia kwa kirefu vacuum ya ideology inayolikabili taifa letu, especially in practicalities za vyama vyetu vya siasa ambavyo malengo yake ni kushinda chaguzi, kuunda serikali, na kuja na sera zenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania, sera zitokanazo na itikadi, sio sera zitokanazo na leo waziri au katibu mkuu ameamkaje.Sasa, kuhusu Afya ni Biashara, hii ni itikadi ya kihafidhiana (Conservatism), unlike mtazamo kwamba Afya ni Huduma msingi katika Jamii ni itikadi ya mrengo wa kati kwa kiasi fulani, lakini zaidi mirengo ya kushoto. Kwahiyo iwapo wewe imani yako kuhusu Afya ndio hiyo, basi tofauti yangu na ewe ni ya ki-itikadi tu, na tofauti hii inajadilika, hakuna wa kukosea au wa kupatia, kama ulivyojaribu pendekeza. Ni suala la kujenga tu hoja.
Iwapo huo ndio mtazamo wako juu ya Afya i.e. kwamba ni biashara, ningependa tuendeleze mjadala huu, na naomba unielezee zaidi biashara hiyo itaendaje katika Tanzania ambapo suala la kuiachia sekta ya afya iendeshwe na nguvu za soko tayari ilishapelekea market failure, na ndio maana hao hao waliokuwa na mtazamo wa afya ni biashara (WorldBank na IMF), wakairudisha serikali katika kutoa huduma hiyo - again, kutokana na market failure in that sector.
Lakini Mkuu, katika mijadala mingi sana humu, kama vile nimekuwa nakuelewa wewe na mimi tupo katika mrengo mmoja ki-hoja yani, mrengo wa kushoto. Sikutegemea ungekuwa mrengo wa kihafidhiana juu ya suala hili la afya. Lakini inawezekana kwamba nilikuwa sikusomi vizuri awali, au sijakusoma vizuri katika hoja yako ya leo.
2. Kuna suala la pili ambalo ningependa pia kulizungumza. Linahusu kauli yako ifuatayo:
[/COLOR]Mkuu Mkandara, Je, maana yako hapo ni kwamba Mimi Mchambuzi ni Sehemu ya Utawala wa Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete? au nimekuelewa sivyo? Kama ulimaanisha hivyo, naomba tu uelewe kwamba, ingawa nimevaa shati la Chama Cha Mapinduzi, Mchambuzi ni mtu aliyejiajiri mwenyewe kujitafuita riziki yake ili mradi siku ziende, kwahiyo nipo kwenye sekta binafsi, sehemu ndogo ikiwa kwenye sekta isiyo rasmi, lakini kubwa zaidi kwenye sekta iliyo rasmi na inayolipa kodi. Mimi sina madaraka ya aina yoyote katika chama cha mapinduzi, kuanzia shina hadi taifa; Na pia sina madaraka yoyote katika Serikali ya CCM, kuanzia serikali ya kijiji, serikali ya mtaa, serikali kuu, na wala utumishi wowote wa umma. Mimi sina cha zaidi ya uanachama wa CCM niliyelipia ada zangu zote kama wanachama wengine wote huko mijini na vijijini.
Naomba Kuwasilisha Mkuu.
Na hapana sii kweli kwamba AFYA kuwa biashara ni sera ya Kihafidhina sii kweli kabisa isipokuwa Uhafidhina unamlinda mwananchi na biashara inabakia mikononi mwa wananchi. Sio lazima Afya iwe biashara hata kidogo usitumie Uhafidhina wa Marekani maana mazingira tofauti. Canada, japan na nchi kibao AFYA ni bure na wahafidhina wapo isipokuwa matumizi yasiyokuwa na sabau ndio hatutaki. Marekani wanazo Hospital za bure lakini ia zipo Private tunachokataa wahafidhina ni kuona huduma hizi zinafanywa na serikali tu na kumfunga mwananchi ktk maamuzi ya afya yake.
Tatizo la Tanzania ni pale tulipoifanya AFYA kuwa biashara wakati huo huo serikali inaingiza mafedha kibao ktk subsidies ambazo hazitoi nafuu kwa mwananchi. Hivyo mimi kama Mhafidhina napinga matumizi mabaya ya fedha zetu na hivyo kutaka ruzuku zote zikatwe na tuunde mfumo mpya ambao Hospital binafsi zitapewa ruzuku tu ikiwa watatoa huduma hizo bure au karibu na bure laa sivyo wajitegemee na tutawajengea sera za kuwawezesha kuendesha biashara zao.
Serikali itaendelea kutoa huduma bure za Afya kulingana na mazingira yetu maana tuliupata Uhuru wetu kwa kupigania mambo haya. Na lazima tuya enzi ndio Uhafidhana wenyewe..
Hivyo kuna mambo mengi sana watu huchanganya baina ya UBEPARI na UHAFIDHINA ingawa kweli Uhafidhina unatetea zaidi kuboresha miundombinu inayozalisha kazi hivyo kuwapa nafuu wawekezaji wa ndani na sio Nje maana Uhafidhina tunapinga sana wageni.. Utajirisho wa wananchi ndio huzaa ajira na ajira ndio huboresha maisha ya wananchi na sio kutoka chini kwenda juu. Ukimwezesha mtu kujenga kiwanda kwa kodi nafuu unamhamasisha kujikuza na kutoa ajira zaidi hivyo ujenzi unaanza ktk uwekezaji.
Hakuna mahala popote panaposema Uhafidhina unapinga elimu na Afya bure kwa wananchi wake isipokuwa unatazama kwanza biashara inaweza vipi kuleta maendeleo dhidi ya serikali kujihusisha. Hivyo Mhafidhina yeyote hapa Canada ukimwambia US wanalipia Afya na shule tunacheka sana! kwa sababu kodi ya mwananchi inatumika pale inapohitajika zaidi na maswala yote ya biashara unawaachia wananchi serikali haiweki mguu isipokuwa kujenga policies zinazowawezesha hawa wawekezaji kukua kibiashara bila kuumiza wananchi.
Pili, swala la kutojua kama serikali imefilisika.
Mkuu wangu sina maana ya wewe isipokuwa hoja nzima mnashindwa kuelewa kwamba hapa tulipofikia serikali yetu IMEFILISIKA!...Ukweli ndio huo, serikali inatumia mabillioni ya fedha zake ktk vitu ambavyo havina mpango na matokeo yake tunakwama hapa tulipokwama isipokuwa wengi hawafahamu na nikadhani na wewe pia hufahamu hilo.
Sasa wewe nambie Madaktari wanagoma kwa sababu ya posho lakini wameweka na ati vifaa vya kutendea kazi havitoshi...hii kweli inaingia akilini?.. Miaka yote ya Udaktari wao wamefanya kazi hii ktk mazingira magumu zaidi enzi za mwalimu leo hii ubora wa Hospital wakati wewe mwajiriwa inakuwa sababu ya mgomo wako?. Sababu zote walizotoa hazina maana zaidi ya madai ya posho kwa sababu tu Pinda kapitisha ongezeko la posho za wabunge..peroid!.. Ni ujinga toka kwa serikali na ujinga toka kwa Madaktari maana wanatuumiza sisi wananchi.
Kweli serikali imefilisika na sii uongo na sababu kubwa ni hizi posho na matumizi yasiyokuwa ya msingi. Tunatumia fedha nyingi sana ktk recurrent expenditures badala ya kuboresha huduma zenyewe. Wabunge wana vikao mia kwa mwaka wote wakichota ruzuku lakini ufanisi ktk kazi hakuna. na kila tunapojiuliza kwa nini tumeshindwa zinaundwa tume nyingine kuchunguza na kuchukua posho zaidi. Sasa hivi ktk kufikiria Tanzania yenye mabadiliko wanaunda tume kuunda dira ya nchi wakati Katiba haijafikia muafaka.. Haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi na Ufafidhina tunajali sana kodi za wananchi zinatumika vipi.