Nawaunga Mkono Madaktari

Nawaunga Mkono Madaktari

Mchambuzi,
Naona unakwepa ukweli uliosimama wazi kabisa.. AFYA ni biashara hivyo yote uloandika hapo juu ni matokeo ya kunedesha biashara huduma muhimu kama AFYA wakati wananchi wake hawana uwezo. Kwa nini Kiogoma hakuna Madaktari au Hospital za kutosha?.. Kwa sababu hakuna biashara nzuri kuliko Moshi, Arusha na Dar..

Swala la AFYA kwa nchi kama yetu halikutakiwa kabisa kuwa ktk mfumo uliopo ambao una jenga maradhi zaidi ili wananchi waende kutibiwa Hospital. Mtu anaumwa malaria atafanyiwa vipimo vya kila aina ikiwa hakuomba yeye afanyiwe kipimo cha Malaria. Leo hii Tanzania unatakiwa kwenda Hospital unajua unaumwa nini, laa sivyo utatozwa maelfu na mwisho wa siku utaambiwa na Dakatari huyo huyo Jioni au kesho njoo katika zahanati yangu iko Buguruni.

This is reality mkuu wangu mnajaribu sana kuficha madhambi ya mchezo mzima wanaofanyiwa wananchi kwa kuilaumu serikali wakati UFISADI umekuwa sehemu ya maisha yetu. Kweli serikali imeshindwa tena sehemu zote za uongozi na ndio maana imefilisika.. au hamjaambiwa hilo?.

Hakuna daktari mwenye hali mbaya Dar au Tanzania naomba nionyesheni hata mmoja ambaye hana hata nyumba na gari la kifahari!..Na kama yupo basi huyo ndio kamaliza tu masomo na kaanza kazi lakini within next 5 yrs sii mwenzako tena.
Ni wizi mtupu toka mashuleni hadi Hospital tunafuga maradhi kama mbegu ya kuzaa wagonjwa.
 
Ikiwa serikali inatoa billioni 90 kila mwaka kwa kanisa mlitegemea itapata fedha wapi zaidi za kuboresha Hospital zake..

Nani alikwambia hizo fedha ni kwa ajili ya kujengea makanisa au kuendeshea mihadhara?
Dhumuni la pesa hizo ni kuboresha hospitali teule ambazo ni kimbilio la watz wengi!
 
Nani alikwambia hizo fedha ni kwa ajili ya kujengea makanisa au kuendeshea mihadhara?
Dhumuni la pesa hizo ni kuboresha hospitali teule ambazo ni kimbilio la watz wengi!
Wapi nimesema fedha zimejenga makanisa na mihadhara!... jamani huu ukumbi siku hizi vipi?..
Na kama ulivyosema ndivyo, sasa kwa nini madaktari wamegoma?.. kwa nini iwe jukumu la serikali ikiwa fedha hizo walipewa makanisa kuboresha huduma hizo..Wewe unajua hiyo kamati ya CSSC walizitumia vipi fedha hizo? na kwa nini usitake wakupe mahesabu lakini akisema Mkandara tayari ni Udini wakati hata wewe unaweza kuuliza?..
 
Mkandara hebu weka keyboard pembeni akili itulie.kama umebadilika hadi hulka (gadhabu) nitashangaa sana! Naomba nisi divert mjadala kujibu hoja zako! Kama umechange mkuu kama ulivyosema basi ni negative changes!
 
Wapi nimesema fedha zimejenga makanisa na mihadhara!... jamani huu ukumbi siku hizi vipi?..
Na kama ulivyosema ndivyo, sasa kwa nini madaktari wamegoma?.. kwa nini iwe jukumu la serikali ikiwa fedha hizo walipewa makanisa kuboresha huduma hizo..Wewe unajua hiyo kamati ya CSSC walizitumia vipi fedha hizo? na kwa nini usitake wakupe mahesabu lakini akisema Mkandara tayari ni Udini wakati hata wewe unaweza kuuliza?..

Bora umejijibu mwenyewe;nani ameongelea habari za udini hapa?
Madai ya madaktari ni juu ya ubora wa huduma za afya.Si kweli kwamba serikali imewekeza kidogo katika huduma za afya kwenye
hospitali zake ukilinganisha na hizo 90b ambazo kimsingi bado ni kwa dhumuni lilelile!
Serikali ilishindwa kujenga hospitali kubwa kila wilaya na mkoa na hivyo kulazimika kuingia mkataba na kanisa.
Bila kutoa hizo pesa;huduma zingekuwa aghali sana na hivyo watanzania wa kawaida kushindwa kumudu!
Mkuu Mkandara huyafahamu haya?
 
Nionyeshe nakala hata moja inayosema serikali ilishindwa kujenga Hospitali maana haya maneno nayasoma hapa hapa JF tu.. Ni lini na waziri au rais gani alitangaza uwezo mdogo wa serikali kujenga Hospital wilayani hivyo kulitaka kanisa lifanye hivyo..kumwona Daktari unalipa Ths 40,000 hadi 50 unaona sii ghali?
 
Nionyeshe nakala hata moja inayosema serikali ilishindwa kujenga Hoprital maana haya maneno nayasoma hapa hapa JF tu.. Ni lini na waziri au rais gani alitangaza uwezo mdogo wa serikali kujenga Hospital wilayani hivyo kulitaka kanisa lifanye hivyo..

Kwa hiyo unadhani serikali ingekuwa radhi kumwaga mabilioni hayo ya shilingi bure?
Mazingira yanaonesha ilizidiwa ndio maana ikafikia hapo!
 
[quote name="Ramadhan Y.Kengwa"]YAH;MAONi YANGU KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI Serikali tunaiomba iwe makini katika swala la madaktari kwani hii ndiyo inayofanya madaktari wengi kukimbilia nje ili kutafuta maslahi mazuri zaidi.Pia naiomba serikali isichanganye siasa na taaluma kwani hatari kwa maendeleo ya nchi, huu mgomo wanaoumia watu wa hali ya chini ambao ni walala hoi.Wakubwa wenyewe huenda nje kwa matibabu kwa sababu ya uwezo wao walionao, kufanya mchezo na madaktari ni sawa na kuchea maisha ya mtu au uhai wa mtu. Mwisho naiomba serikali iwalipe posho zao madaktari mbona wabunge wanadai posho na serikali inawatetemekea? NDIO MANAKE WANACHEZEA NDEVU ZA SIMBA?????????????????
 
huyu ni Mkandara kweli!!?? this is too low kwa level yako, hivi hapa tunaweza kukutofautisha na Maralia Sugu? kwa hiyo solution ya matatizo haya ni kuwa na Mahakama ya kadhi na tujiunge na OIC?
linapokuja suala la kanisa na huduma za jamii mkandara=malaria sugu=faizafoxy=topical=ritz=ally kombo=boko haram=mohamed said nk..nk! mtakesha.
 
Kwa hiyo unadhani serikali ingekuwa radhi kumwaga mabilioni hayo ya shilingi bure?
Mazingira yanaonesha ilizidiwa ndio maana ikafikia hapo!
Mazingira gani? Hivi kwani kabla ya mwkaa 1992 tulikuwa na shida gani ambayo wewe unaifahamu! Kwetu Ukerewe hadi leo Hospital ni moja binafsi sioni lolote jema ktk muafaka huo zaidi ya matatizo makubwa ktk Elimu na Afya. Mkuu wangu unachoshindwa kuelewa ni kwamba hawa waliokabidhiwa vyombo hivi ni binadamu kama wewe na wanataka maisha bora hivyo kutumia dini kama sehemu ya kuchumia tumbo.

Tuwaulize wao hizo fedha wamezifanyia nini hadi madaktari wanaandamana na kugoma kiasi sisi wananchi tunakosa huduma. Tuwaulize serikali walishindwa vipi kufanisi hizi Hospitali zenu na tuyapate majibu kutoka kwao sio sisi hapa JF kutunga majibu kwa niaba yao. Mimi natazama maisha yako wewe, mimi na Watanzania wote bila kujali dini zetu na kwamba tuna changia mtaji wa kuendesha hizi huduma kisha tunalipa tena gharama kubwa kwa magonjwa ambayo yalitakiwa kutolewa huduma baada ya sisi kuchagia mtaji.

Kama serikali imeweza kujenga shule za kata Tanzania nzima bado tunachangia ruzuku za kitu gani ktk elimu?.. mbona mnakwepa maswali.. Najua tuna tofauti ktk imani zetu na kwamba mimi naruhusiwa kumuuliza Sheikh sadaka yangu imetumika vipi lakini wewe huruhusiwi au pengine hampendi kuuliza, hivyo usinishangae sana kuuliza haya maana sielewi kwa nini iwe kosa kuwauliza viongozi wa CSSC wanavyozitumia ruzuku zetu ikiwa madaktari wamefikia kugoma na kuwaacha wagonjwa wakifa na watoto wengine wachanga wameachwa ktk maabara bila kuhudumiwa. Hata dini hairuhusu hivi na maamuzi kama haya.

Huu ni unyama toka pande zote na nina haki ya kuuliza mtu yeyote ninayefahamu ni mhusika wa janga hili..Siwaungi mkono Madaktari na wala siwaungi mkono serikali au kanisa wote hawa wanatakiwa kutoa maelezo ya kina ili tupate kujua tumefika hapa kwa sababu gani? Hawa madaktari mnaowatetea ni matajiri kati ya matajiri wa Kitanzania hawana maisha mabaya kama mnayojaribu kutudanganya. Na mifano yote nimeitoa huko nyuma.. Wee nambie ni kazi gani unaweza kutengeneza Tsh 40,000 kwa saa ama nusu saa kama kazi kumwona Daktari?..
 
Mchambuzi,
Naona unakwepa ukweli uliosimama wazi kabisa.. AFYA ni biashara hivyo yote uloandika hapo juu ni matokeo ya kunedesha biashara huduma muhimu kama AFYA wakati wananchi wake hawana uwezo. Kwa nini Kiogoma hakuna Madaktari au Hospital za kutosha?.. Kwa sababu hakuna biashara nzuri kuliko Moshi, Arusha na Dar..

Swala la AFYA kwa nchi kama yetu halikutakiwa kabisa kuwa ktk mfumo uliopo ambao una jenga maradhi zaidi ili wananchi waende kutibiwa Hospital. Mtu anaumwa malaria atafanyiwa vipimo vya kila aina ikiwa hakuomba yeye afanyiwe kipimo cha Malaria. Leo hii Tanzania unatakiwa kwenda Hospital unajua unaumwa nini, laa sivyo utatozwa maelfu na mwisho wa siku utaambiwa na Dakatari huyo huyo Jioni au kesho njoo katika zahanati yangu iko Buguruni.

This is reality mkuu wangu mnajaribu sana kuficha madhambi ya mchezo mzima wanaofanyiwa wananchi kwa kuilaumu serikali wakati UFISADI umekuwa sehemu ya maisha yetu. Kweli serikali imeshindwa tena sehemu zote za uongozi na ndio maana imefilisika.. au hamjaambiwa hilo?.

Hakuna daktari mwenye hali mbaya Dar au Tanzania naomba nionyesheni hata mmoja ambaye hana hata nyumba na gari la kifahari!..Na kama yupo basi huyo ndio kamaliza tu masomo na kaanza kazi lakini within next 5 yrs sii mwenzako tena.
Ni wizi mtupu toka mashuleni hadi Hospital tunafuga maradhi kama mbegu ya kuzaa wagonjwa.

Mkuu Mkandara,

Ukinisoma between the lines, utabaini kwamba mimi na wewe tunaongea kitu hicho hicho. Kwa mtazamo wangu, lugha zetu sawa, inawezekana tunachopishana ni 'lafudhi' tu. Vinginevyo, nia yangu ilikuwa sio zaidi ya ile iliyolenga to 'stimulate' a debate juu ya jambo hili, tuweze kuliangalia tatizo hili kwa undani zaidi. In that line, nikawasilisha takwimu za sekta ya afya kama zilivyo, ili kwa pamoja tusaidiane kubaini tatizo lipo wapi, na kupendekeza suluhisho la kudumu. Kwa kweli, sijawa as subjective katika maelezo yangu ya awali kwani - sijatetea sekta binafsi, sijatetea sekta ya umma, na wala sijatetea sekta ya NGO, zaidi ya kuelezea hali halisi kama ilivyo, na kumalizia kwa maswali.

Lakini kuna vitu viwili tu ambavyo ningependa kuvijadili, kama majibu yangu kwa hoja zako.

1. Kwanza ni kuhusu hoja yako kwamba "Afya ni Biashara." Nimeipenda hoja hii, kwani katika thread yangu nyingine, nilizungumzia kwa kirefu vacuum ya ideology inayolikabili taifa letu, especially in practicalities za vyama vyetu vya siasa ambavyo malengo yake ni kushinda chaguzi, kuunda serikali, na kuja na sera zenye lengo la kuboresha maisha ya watanzania, sera zitokanazo na itikadi, sio sera zitokanazo na leo waziri au katibu mkuu ameamkaje.Sasa, kuhusu Afya ni Biashara, hii ni itikadi ya kihafidhiana (Conservatism), unlike mtazamo kwamba Afya ni Huduma msingi katika Jamii ni itikadi ya mrengo wa kati kwa kiasi fulani, lakini zaidi mirengo ya kushoto. Kwahiyo iwapo wewe imani yako kuhusu Afya ndio hiyo, basi tofauti yangu na ewe ni ya ki-itikadi tu, na tofauti hii inajadilika, hakuna wa kukosea au wa kupatia, kama ulivyojaribu pendekeza. Ni suala la kujenga tu hoja.

Iwapo huo ndio mtazamo wako juu ya Afya i.e. kwamba ni biashara, ningependa tuendeleze mjadala huu, na naomba unielezee zaidi biashara hiyo itaendaje katika Tanzania ambapo suala la kuiachia sekta ya afya iendeshwe na nguvu za soko tayari ilishapelekea market failure, na ndio maana hao hao waliokuwa na mtazamo wa afya ni biashara (WorldBank na IMF), wakairudisha serikali katika kutoa huduma hiyo - again, kutokana na market failure in that sector.

Lakini Mkuu, katika mijadala mingi sana humu, kama vile nimekuwa nakuelewa wewe na mimi tupo katika mrengo mmoja ki-hoja yani, mrengo wa kushoto. Sikutegemea ungekuwa mrengo wa kihafidhiana juu ya suala hili la afya. Lakini inawezekana kwamba nilikuwa sikusomi vizuri awali, au sijakusoma vizuri katika hoja yako ya leo.

2. Kuna suala la pili ambalo ningependa pia kulizungumza. Linahusu kauli yako ifuatayo:

Kweli serikali imeshindwa tena sehemu zote za uongozi na ndio maana imefilisika.. au hamjaambiwa hilo?.

Mkuu Mkandara, Je, maana yako hapo ni kwamba Mimi Mchambuzi ni Sehemu ya Utawala wa Serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete? au nimekuelewa sivyo? Kama ulimaanisha hivyo, naomba tu uelewe kwamba, ingawa nimevaa shati la Chama Cha Mapinduzi, Mchambuzi ni mtu aliyejiajiri mwenyewe kujitafuita riziki yake ili mradi siku ziende, kwahiyo nipo kwenye sekta binafsi, sehemu ndogo ikiwa kwenye sekta isiyo rasmi, lakini kubwa zaidi kwenye sekta iliyo rasmi na inayolipa kodi. Mimi sina madaraka ya aina yoyote katika chama cha mapinduzi, kuanzia shina hadi taifa; Na pia sina madaraka yoyote katika Serikali ya CCM, kuanzia serikali ya kijiji, serikali ya mtaa, serikali kuu, na wala utumishi wowote wa umma. Mimi sina cha zaidi ya uanachama wa CCM niliyelipia ada zangu zote kama wanachama wengine wote huko mijini na vijijini.

Naomba Kuwasilisha Mkuu.
 
Well kuanzia sasa hivi Mkandara siye yule umjuaye tena. Mimi nalilia maslahi ya wananchi na sio ya Kanisa wala Msikiti. Tunalipa kodi zetu sasa wanagoma ili iweje kama sio tufe sisi, wakati wameshakatiwa fungu na serikali. nani anayepanga matumizi ya uendeshaji biashara zao kama sio kamati ya CSSC. Na hata wangekuwa Bakwata ningewashambulia kama navyofanya hapa maadam nachokitazama ni maslahi ya wananchi sio dini wala dhehebu.

Kama madaktari wanataka kugoma waanze na kwenda ktk menejimenti zao kujua kulikoni. Tena tunatakiwa kabisa kudai CSSC watupe matumizi ya ruzuku zetu maana mkuu wangu hata wewe Mkristu unalipia fedha hizi ktk kodi na bado unatozwa kumwona daktari. Hakuna nafuu kwako wewe wala mimi sote tunaumizwa, hivyo unapolifanya swala hili liwe la Udini ndipo napowashangaa wakati linakuumiza hata wewe. Hawa ni watu tu binadamu kama wewe mnawaogopa kitu gani?... kwa sababu viongozi wa dini!... Upuuzi mtupu ndio maana CCM itatawala milele kwa kuwagawa.
Mkandara wewe tuna maswali mengi kuliko majibu kwa hoja zako dhaifu. Ondoa kwanza udini ndani yako kisha ujadili hoja ya msingi. Sijajua nani amekuloga mwislamu wewe huna hata hoja zaidi ya malalamiko hasi. Kwa nini bakwata au chombo kingine kisipewe fedha hizo? Umeshawahi kujiuliza intellectually? Siyo religiously? Hebu jaribu kujifanya umeelimika kwenye jamii ya walioelimika ili kuficha wingi wa ujinga. Ni ushauri tu
 
Udini uko wapi jamani? Hivi kuuliza swala la AFYA ni la Udini kwa sababu tu CSSC wamekabidhiwa jukumu hilo..Sasa niwaulize nani maana umeme najua nitawaliza Tanesco, hili la afya niwataje nani au nipeni jina jingine basi nilitumie! hao Bakwata sitaki wapewe hata ndululu maana ni binadamu na wana matamanio wao wajishughulishe na dini tu. Swala la Afya ni la serikali na nataka kuilalamikia serikali lakini jukumu hilo wamewapa CSSC sasa mimi nifanyeje?
 
Kuna madaktari wengine wanasuasua kugoma utadhani hawana shida, maslahi yakiboreshwa ndo wa kwanza kucheki salio...
 
linapokuja suala la kanisa na huduma za jamii mkandara=malaria sugu=faizafoxy=topical=ritz=ally kombo=boko haram=mohamed said nk..nk! mtakesha.
Kweli aisee!! maana naona akili zake ameamuwa kuzifungia kabatini, hivi kwa nini muislamu hata awe msomi vipi lakini akiifuatilia hii dini lazima akili zake zipate mushkeli!! bado najiuliza sana hili swali.
 
Mazingira gani? Hivi kwani kabla ya mwkaa 1992 tulikuwa na shida gani ambayo wewe unaifahamu! Kwetu Ukerewe hadi leo Hospital ni moja binafsi sioni lolote jema ktk muafaka huo zaidi ya matatizo makubwa ktk Elimu na Afya. Mkuu wangu unachoshindwa kuelewa ni kwamba hawa waliokabidhiwa vyombo hivi ni binadamu kama wewe na wanataka maisha bora hivyo kutumia dini kama sehemu ya kuchumia tumbo.

Tuwaulize wao hizo fedha wamezifanyia nini hadi madaktari wanaandamana na kugoma kiasi sisi wananchi tunakosa huduma. Tuwaulize serikali walishindwa vipi kufanisi hizi Hospitali zenu na tuyapate majibu kutoka kwao sio sisi hapa JF kutunga majibu kwa niaba yao. Mimi natazama maisha yako wewe, mimi na Watanzania wote bila kujali dini zetu na kwamba tuna changia mtaji wa kuendesha hizi huduma kisha tunalipa tena gharama kubwa kwa magonjwa ambayo yalitakiwa kutolewa huduma baada ya sisi kuchagia mtaji.

Kama serikali imeweza kujenga shule za kata Tanzania nzima bado tunachangia ruzuku za kitu gani ktk elimu?.. mbona mnakwepa maswali.. Najua tuna tofauti ktk imani zetu na kwamba mimi naruhusiwa kumuuliza Sheikh sadaka yangu imetumika vipi lakini wewe huruhusiwi au pengine hampendi kuuliza, hivyo usinishangae sana kuuliza haya maana sielewi kwa nini iwe kosa kuwauliza viongozi wa CSSC wanavyozitumia ruzuku zetu ikiwa madaktari wamefikia kugoma na kuwaacha wagonjwa wakifa na watoto wengine wachanga wameachwa ktk maabara bila kuhudumiwa. Hata dini hairuhusu hivi na maamuzi kama haya.

Huu ni unyama toka pande zote na nina haki ya kuuliza mtu yeyote ninayefahamu ni mhusika wa janga hili..Siwaungi mkono Madaktari na wala siwaungi mkono serikali au kanisa wote hawa wanatakiwa kutoa maelezo ya kina ili tupate kujua tumefika hapa kwa sababu gani? Hawa madaktari mnaowatetea ni matajiri kati ya matajiri wa Kitanzania hawana maisha mabaya kama mnayojaribu kutudanganya. Na mifano yote nimeitoa huko nyuma.. Wee nambie ni kazi gani unaweza kutengeneza Tsh 40,000 kwa saa ama nusu saa kama kazi kumwona Daktari?..

Ni sababu tu umefunga akili yako isikubaliane na hili ndio maana utabaki ukibisha tu!
Kusini Peramiho Hospital ni kimbilio la watz wengi!
Nadhani unazifahamu hospitali kama Bugando,KCMC,Ifisi na zinginezo ambazo ni kimbilio la watanzania wengi.
Bila serikali kuchangia hapa hali ingekuwa mbaya!
Anyway;nilijua nabishana kwa hoja na wewe kumbe upo kidini zaidi mana umeanza kuingiza habari za mashehe na wachungaji...irrelevant na ishara kuwa umeishiwa hoja!
Uwe na usiku mwema!!!
 
Back
Top Bottom