Nawaunga Mkono Madaktari

Nawaunga Mkono Madaktari

Hivi Mkandara naye siku hizi ni mod? Maana ingekuwa ni mimi nasema anayosema ningekuwa nimefungiwa tayari. Au utovu wa nidhamu ni wanaposhambuliwa waislamu tu? Wanaposhambuliwa wakristo hizo ni facts?
 
Jokes aside, Mkandara unaamini kwa dhati sababu kubwa inayofanya wakubwa wapelekwe India kwa matibabu ni kwa sababu inatoa ruzuku kwa hospitali zinazoendeshwa na kanisa? Hebu angalia hiyo list ya madai ya madaktari kwa makini tena. Halafu unganisha na EPA, meremeta, na majinamizi mengine yanayofanana na hayo.
Mkuu wangu kwa nini mnanibandikia majibu wakati sijasema hivyo? ni wapi nimesema wakubwa wanapelekwa India kwa sababu ati serikali iinatoa ruzuku kwa Hospital za kanisa!..

Hoja zangu ni za msingi isipokuwa nyie ndio mnashindwa kutoka nje ya kabati la Udini. Swala la viongozi kupelekwa India nalipinga pale madaktari wanapolitumia kama sababu ya wao kufanya mgomo huu kusema kweli haihusiani kabisa na mgomo maana wangekataa kuwapokea viongozi Hospital zao kabla ya kuepelkwa India nasi tungeungana nao..

Mimi nimesema wazi kabisa kwamba serikali kuunda muafaka na kukabidhi kamati ya CSSC mamlaka ya Afya na Elimu ya wananchi wake nchini ni makosa. sasa iwe wewe unalitazama swala hil kwa jicho lolote lile hainihusu mimi maana nionacho mimi ni muafaka sawa na ule wa CUF na CCM ktk uongozi wa Zanzibar.. Je kuna makosa? ukimuuliza Mzanzibar atakwambia ni wivu wa watu wa bara lakini muulize wa bara atakubaliana nami vivyo hivyo ktk swala hili Musilaam, Budha au Pagan atakubaliana na mimi lakini sio Mkristu.

Nazungumzia maswala haya bila kutazama interest za dini na tofauti yangu kubwa na nyie wote ni kwamba kila hoja huitazama vizuri na kuisoma kisha natazama maslahi ya wahusika. Kwa mfano mnapopinga mahakama ya kadhi mbona mimi sisemi nyie ni Wadini? badala yake nimelichunguza swala hili kivyangu na kukubaliana nanyi kwamba mahakama ya kadhi haifai, ili hali mimi Muislaam japokuwa ninazo sababu tofauti kabisa na zetu. lakini nimekubali na kupingana na waislaam wenzangu ktk hili..Tena basi katiba inawapa mamlaka haya waislaam kisheria kuwa na chombo hicho maadam tunakubali Cultural law zitumike..Hee udini wangu uko wapi?

Madai ya Madaktari hayawezi kujengana EPA au Meremeta ili wao nao wapewe hii sio kuwatendea haki wananchi bali kama wanapinga haya waseme watu wote wasipewe ikiwa ni pamoja na wao. Mbona Zitto amekataa posho ili hali yeye mbunge na kusisitiza zifutwe? Hivi kweli tunakubaliana na hoja ya kina Shibuda ambao wanaikubali posho kwa sababu ya EPA na maswala mengineyo.. I'am consistant na argument zangu..

Ukweli unabakia kwamba hawa madaktari wameweka madai yao kwa sababu Pinda katangaza kupitisha posho za Wabunge. hawa walitakiwa wajiunge na jumuiya nyinginezo za kitaifa kuweka madai ya kupinga posho hizi na sio kuomba wao pia wapewe wakati sisi wananchi tunaumia sana. Tunawalipa kuonana nao na tunawalipa kwa tiba na kadhalika mbali kabisa na ruzuku wanazopewa. Na nimewahi kuandika hapa kwamba kuna jamaa yangu alienda tibiwa India kutokana na gharama kubwa aloambiwa KCMC ya dollar za kimarekani 4,000 wakati tulipompeleka India imetugharimu only 2,500 Us flight included na katibiwa na kulala Hospital ya Appolo. Kwa hiyo madai ya watu kwamba bila ruzuku gharama zingekuwa kubwa zaidi ni uongo mtupu, haiwezekani mtu kwenda kumwona daktari unatozwa Tsh 40,000 kwa nusu saa halafu hawana hata vipimo vizuri halafu watu mnasema ati sio ghali... nyie mnaishi Tanzania gani?..

Sasa kama nyie mna uchungu sana na wananchi wengine bila kujali imani zao za dini hawa wote wanalipa kiwango kikubwa sana kwa tiba wakati wameisha changia mtaji wa kodi zao ktk ruzuku. Na tazama sehemu zote Subsidy ni kitu gani na inatolewa vipi tazama hata site za Marekani utaona lengo ni kumwezesha mwananchi asiyejiweza kukabiliana na gharama lakini Tanzania yetu haichagui mtu.. tunatozwa wote isipokuwa siku hizi wazee ndio wamewekwa tena kutokana na kwamba viongozi wenyewe wanazeeka na hivyo wanatazama maslahi yao wenyewe ama tiba kwa wazazi wao.

Hizo hospitali zinaweza kuendelea kupewa ruzuku kwa malengo ya kutibu wagonjwa na sio kuziendeleza hospital za binafsi. Mtu akienda Hospital ya kanisa anatozwa gharama na serikali itachangia gharama hizo sio kanisa kushiriki kupanga mipango ya maendeleo ya Afya na Elimu nchini wakisaidiana na serikali..Hii inalifanya kanisa kuwa part ya serikali mkubali msikubali ndio ukweli ulio wazi kabisa na ndio maana Udini umetokana na mambo kama haya..Tunaweza kabisa kuepuka mvurugano unaotokana na vitu kama hivi.

Na hakuna mahala nimepinga huduma za kanisa as a fact zimenikuza mimi sana tu maana nilipokulia kulikuwa khakuna shule isipokuwa za kanisa Namibu na Kagunguli na hospital moja tu ya kanisa Namibu. Ukija Ukerewe ni yale yale kwa hiyo ktk hilo nalipongeza kanisa lakini sii kuwapa wao mamlaka ya kuendesha AFYA na ELIMU jambo ambalo walikuwa wakifanya wakati wa mkoloni. Vyombo vya dini vibakie na maswala ya dini na kama wanataka kufanya biashara basi wawekeze ktk maswala hayo kama mashirika mengine au tulivyokuwa zamani bila serikali yetu kujiingiza ubia nao. Hili sikubaliani nalo iwe Kanisa au Bakwata kuweka muafaka na serikali kuunda ubia... Hii haikubaliki na naipinga kwa nguvu zote..
 
Mkandala uliwahi kulalamika kuhusu jukwaa la siasa,....

Leo katika mada tofauti kabisa,isiyo husisha mambo ya dini wala udini,ukiwa mchangiaji
wa kwanza katika thread hii ukaanza kwa kusema:-

Now,unabisha kwamba hujaongelea udini na wewe ndio ume chafua topic kabisa tofauti na
hoja uliyo itoa jukwaa la ulalamikaji kuhusu kuyumba kwa Jukwaa la siasa.

Kwanini tusiamini kwamba Una ID nyingi ambazo unatumia kueneza chuki za kidini humu
na ID nyingine una jidai mtakatifu?
Mkuu wangu kama unanisoma vizuri nachokipinga ni muafaka haina Udini wala shetani kama vile wewe unavyopinga muafaka wa CUF na CCM, haikufanyi wewe mbara sana kwa kupinga Muafaka huo isipokuwa umetazama malshai ya wananchi wa pande zote mbili.

Matatizo haya ya madaktari yanatokana na serikali kukosa kuwa na mipango madhubuti kuhusiana na Afya na CSSC inahusika. Sawa kabisa na Mbara annayepinga muafaka wa CCM na CUF kusema haikutakiwa. Tazama unavyoopenda lakini huu muafaka hata wangepewa Bakwata au AgaKhan ningeupinga kama alivyopinga Nyerere wakati wake..Mimi namfuata Nyerere na nilimwelewa kwa nini alifanya vile, nyie mnaogubikwa na Udini ndio mnashindwa kunielewa.
 
Pumba Express!!
 
Ikiwa serikali inatoa billioni 90 kila mwaka kwa kanisa mlitegemea itapata fedha wapi zaidi za kuboresha Hospital zake..

Shida ya akili za mnyama kupewa binadamu. Serikali haitoi fedha kwa kanisa. Kanisa kama kanisa halina uhaba wa fedha za kuendesha shughuli zake mpk lipewe na serikali. Mtu mzima anaposhindwa kutumia ubongo kufikiri ni shida kwa jamii. Serikali hutoa RUZUKU KWA HOSPITALI ZA KANISA na sio kulipa Kanisa. Hivi kwa akili yako ndogo, mgonjwa akipata legal case pale KCMC, inawajibika HOSPITALI au KANISA la Lutheran?

Kukosa shukrani ni tabia mbovu kuliko tabia nyingine za kijamii, na kukosa elimu ndio adhabu kubwa kuliko adhabu zote ktk jamii.
Kama unazungumzia serikali kuboresha hospitali zake, na wale ambao serikali ilishindwa kuwahudumia na sasa wanahudumiwa na hizi za kanisa nao wangefaidika na hayo maboresho wakiwa kilomita 600 kutoka zilipo hizo hospitali za serikali?

Watu wapo kwenye National Affairs, mwingine anaingiza ujinga wa dini yake; kwenda mkabake watoto kwa jina la sunna huko, manake ndio mnachojua zaidi. Mambo ya hospital na maendeleo ya hii nchi tuachie wenye utashi wa elimu na maendeleo.
 
Nadhani ipo haja ya kuangalia the morality ya mgomo wa madaktari; ni wakati gani kwa mfano madaktari wanakuwa na haki ya kugoma?
 
Shida ya akili za mnyama kupewa binadamu. Serikali haitoi fedha kwa kanisa. Kanisa kama kanisa halina uhaba wa fedha za kuendesha shughuli zake mpk lipewe na serikali. Mtu mzima anaposhindwa kutumia ubongo kufikiri ni shida kwa jamii. Serikali hutoa RUZUKU KWA HOSPITALI ZA KANISA na sio kulipa Kanisa. Hivi kwa akili yako ndogo, mgonjwa akipata legal case pale KCMC, inawajibika HOSPITALI au KANISA la Lutheran?

Kukosa shukrani ni tabia mbovu kuliko tabia nyingine za kijamii, na kukosa elimu ndio adhabu kubwa kuliko adhabu zote ktk jamii.
Kama unazungumzia serikali kuboresha hospitali zake, na wale ambao serikali ilishindwa kuwahudumia na sasa wanahudumiwa na hizi za kanisa nao wangefaidika na hayo maboresho wakiwa kilomita 600 kutoka zilipo hizo hospitali za serikali?

Watu wapo kwenye National Affairs, mwingine anaingiza ujinga wa dini yake; kwenda mkabake watoto kwa jina la sunna huko, manake ndio mnachojua zaidi. Mambo ya hospital na maendeleo ya hii nchi tuachie wenye utashi wa elimu na maendeleo.
Sasa kama halina shida ya fedha hizi mnachokililia hapa kitu gani.. Kina nani serikali ilisema imeshindwa kuwahudumia? nambieni nani alosema hivyo? hamtaki mnabakia kutunga maneno tu.. Lini serikali ilitangaza kushindwa kuwahudumia wananchi ktk Afya na ELimu kama sio kamba zenu..Nasema hivi ruzuku zifutwe na serikali ichukue jukumu hilo peke yake aiachane na maswala la kanisa yabakie kanisani..Nilitegemea wewe mwenye akili za binadamu utaelewa sawa kabisa na kujiunga nami maana kanisa linajiweza kabisa na hilo nalijua sana..

Hii ndio sababu nasema serikali haina sababu ya kutoa ruzuku ikiwa wananchi tunatozwa gharama kubwa. Acha za kanisa ziwe private tutatia akili, na wengine tunajibanza humo humo ktk hospitali za kata kama zitajengwa. Maana sasa hivi hatujui jukumu ni la nani maana CSSC hupewa fedha na mahesabu yao hatutakiwi kujua wanazitumia vipi..wee tukana weee utachoka tu mimi nakuja na hoja!
 
Haaa! haaa! nimekugusa patamu..Sasa hivi ndio Mkandara utakaye deal naye. Hakuna cha CCM,CUF wala CDM - maslahi ya wananchi mbele..#changeTanzania..
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuna matatizo 10 ambayo yapo kwa binadamu hayakwepeki, lakini la 11 ni la kujitakia, sasa naanza kuamini alichoniambia.
 
Kanisa lina lawama kubwa kwakuwa wanapewa 90bil kila mwaka kuboresha hospitali za bugando, KCMC, etc lakini inavyoonekana hawakutumia kuboresha huduma hizi ..wamezifisadi..kama kawaida

Serikali ina lawama kubwa kwakuwa imeshindwa a. kuwafuatilia kanisa wasile hizo fedha za umma, b. kushindwa kubersha hospitali zake..

Utaona kuna tatizo letu ni a. Serikali kwa kushirikiana na kanisa katika kutunyonya na kutunyonga..wananchi wanatakiwa watambue hilo
 
Kwahiyo madai ya Madaktari kiini cha tatizo ni hayo uliyoyaandika? hivi humu misikitini huwa mnapewa mafundisho gani? kwa nini wote ujinga wenu unafanana.
 
Kwahiyo madai ya Madaktari kiini cha tatizo ni hayo uliyoyaandika? hivi humu misikitini huwa mnapewa mafundisho gani? kwa nini wote ujinga wenu unafanana.

Hata mimi nawashangaa sana huko kanisani mnapewa mafundisho (dogmatism)? kwasababu ujinga wenu unafanana kutetea mafisadi wa kanisa?? au ndio kuogopa kutofutiwa dhambi na maaskofu?
 
Nionyeshe nakala hata moja inayosema serikali ilishindwa kujenga Hospitali maana haya maneno nayasoma hapa hapa JF tu.. Ni lini na waziri au rais gani alitangaza uwezo mdogo wa serikali kujenga Hospital wilayani hivyo kulitaka kanisa lifanye hivyo..kumwona Daktari unalipa Ths 40,000 hadi 50 unaona sii ghali?

Huu ndio upumbavu ambao ukiwafikia baadhi ya watu huuchukua kama ndio ukweli na kukubali kuandamana. Wapi ndani ya nchi hii kuna hospitali (inayopokea ruzuku) inatoza 40,000 kumuona daktari?

Ujinga wa wapinga MoU ni kudhania kwamba, kila hospitali ya kanisa inapewa ruzuku. Jamani vichwa ngumu hebu eleweni hili: SI KILA ZAHANATI YA KANISA IMETAIFISHWA. Si kila utakapoona kanisa limejenga zahanati basi udhanie matibabu hapo yanagharamiwa na serikali. Hospitali zinazopokea ruzuku ya serikali zinafahamika na ukienda huko gharama za matibabu ni sawa na hospitali za serikali kwani hata namna ya uendeshaji na usimamizi huratibiwa na serikali. Sasa mtu usikurupuke huko ukaenda Kibangu Mission Hospital ukadhani wakatoliki walijenga kutoa huduma kwa niaba ya serikali.

Ama lah, kama unaweza kuthibitisha uanaume wako kwa kutoa mfano ulionyooka juu ya wapi umewahi kutozwa zaidi ya viwango vya serikali ktk designated hospital basi weka hapa ili serikali na wanaJF wengine wajue, lkn sio kuleta upotoshaji wa kijinga hapa.

Tumia akili yako kutofautisha gharama kati ya HOSPITALI ZA KANISA ZINAZOPOKEA RUZUKU NA KURATIBIWA NA SERIKALI NA HOSPITALI BINAFSI ZA KANISA. Mimi sio mantiki ya mtu kujivunia ujinga na kuwaambukiza wenzake kwa kisingizio cha kupigania imani. Kama kitu hujui uliza uelekezwe na sio kuongozwa na hisia. Siku moja moja mtokage huko buguruni mnakoishi muitembee Tanzania mjue mipaka yake na magumu ya wenzetu walio mbali na AMANA unakotibiwa wewe kabla hatujaanza kuropoka ujinga na kujazana roho za chuki kwa kisingizio cha dini.

Elimu kwanza!
 
hizo ndizo zilikuwa fikra za Hosni Mubarak na Gaddafi! Wote waliamini kuwa dola iko juu ya wananchi. Ndio maana ni muhimu kwa wananchi kuonesha support. Watanzania tumekuwa tukigawanywa sana kiasi kwamba tunashindwa kusimamia hata vitu ambavyo tunajua vitatusaidia. kwa mfano, walim,u wanaweza wasiunge mkono madaktari kwa sababu madaktari watafanikiwa! wahandishi wanaweza wasiunge mkono walimu kwa sababu walimu watafanikiwa.

Ni muhimu kwa wananchi kuwaunga mkono madaktari kwa sababu matokeo yake ni lazima yawe mabadiliko. Kwa mfano, wanafunzi wa vyuo vikuu wako wapi kuunga mkono madaktari?
Mzee wangu katika hili wala sintokuunga mkono wala hao madaktari kwa sababu wanachokifanya ni kuwatesa wagonjwa sio viongozi ambao wao huenda India. Sasa kama wangetaka kufanya mgomo wangesubiri JK au sijui waziri gani kaletwa kwao ana malaria wanamwacha alale word ya watu wote bila huduma na wagome kumhudumia wamwambie aiende India..Huwezi kumtumia mgonjwa kama mhanga wa kuomba posho zaidi hili mkuu wangu sikubaliani nalo kabisa...

Kama tungekuwa na ushirikiano wote kwa pamoja tungeingia barabarani na kuanza maandamano hata kama yangeanzishwa na hawa madaktari lakini kugoma kuwahudumia wananchi hii inaondoa Uzalendo wao kabisa.. Igomee serikali na sio huduma ambayo wananchi wanalipa tena kwa gharama kubwa sana kupata hata kidonge cha malaria..mkulima shamba bado anachemza Muarobaini kwa sababu hawezi kugharamia leo unataka posho zaidi wakati fedha hiyo itamgharimu mkulima na mfanyakazi.
 
Kwani wlaipojenga Hospitali hizi walitegemea ruzuku za serikali? mbona zilikuwa zikitoa huduma hata kabla.. mimi sielewi unakotaka kwenda haswa.. Nachosema maadam ni Hospital private serikali haitakiwi kuweka mguu wake. Wizara ya Afya inatakiwa kuwa na idara zake na CSSC haitakiwi kuwa moja ya idara hizo. kabish

Huu ni mtazamo wangu unaweza kutokubaliana lakini binafsi sikubaliani na sera za CCM wala CDM zinapohusisha kanisa ktk maswala ya kiutawala ktk wizara zake. Nimejieleza vya kutosha subsidies zinaweza kutoka tu pale chombo kinachotoa huduma kitawapa wananchi nafuu kubwa ya gharama lakini haya ya kumwona daktari kwa Tsh 50,000 wakati wamepewa ruzuku ni wizi sitojali nani anafanya hivo..Na madaktari leo ni mashahidi kuwa hata hizo huduma zeneywe ni mbaya kutokana na uwekezaji mbaya.. I think it's about time tuwawajibishe wahusika na kutambua kwamba mfumo huu haufai na umeharibu kabisa huduma za Afya nchini... Nimemaliza ukitaka nisome hutaki niache na mtazamo wangu...
- Sikubaliani na hotuba ya Dr.Slaa Kilombero!...

Mkuu usipofushwe na msimamo wako wa kiimani hadi ushindwe kufikiria. Hospitali za tanzania zina milkiwa na makundi matatu
1. Serkali
2. Non profit organizations e.g msikiti, kanisa, NGO
3. Private eg Agakhan, Hindu mandal, buruani, TMJ, THI, etc

Serkali haina hospitali za kutosha kutibu wananchi wake wala kusomesha vijana wake wanaotaka kujiunga na taasisi za utibabu na uuguzi. Ili kuendeleza huduma hizo serkali ilitafuta alternative ambayo ni kutumia facilities za non profit organizations. Miaka ya nyuma serkali ilifanya ubabe ikazitaifisha na kujipachika illegal ownership.

Baada ya serkali kushindwa kuziendesha ilizirudisha kwa wamilki halali zikiwa katika hali mbaya. Kwa hali ya kawaida serkali ilitakiwa kulipa compensation au basi ijitegemee kwenye hii huduma ya afya lakini bahati mbaya serkali haikufanya chochote kati ya hayo na badala yake bado inawategemea walewale iliyowadhulumu.
Sasa serkali inawajibu wa kutoa huduma za afya kwa jamii lakini haina facilities za kutosha, je ni nani anaemtegemea mwenzake hapa? kanisa au serkali?

Mkandara nakushauri uonane na mbunge wako ili utoe malalamiko yako kwa serkali yako na uiulize ina mpango gani wa kujitegemea kwenye huduma za afya badala ya kutogemea facilities za kanisa
Hospitali za kanisa zitaendelea kufanya kazi za kutoa huduma kwa walengwa bila millioni 90 za serkali ya magamba kwa sababu wao ni non profit making organizations, tena serkali ikiacha kupeleka wagonjwa wake huko ndo huduma zitakuwa bora zaidi kwani wahudumiwa watapungua
 
Huu ndio upumbavu ambao ukiwafikia baadhi ya watu huuchukua kama ndio ukweli na kukubali kuandamana. Wapi ndani ya nchi hii kuna hospitali (inayopokea ruzuku) inatoza 40,000 kumuona daktari?

Ujinga wa wapinga MoU ni kudhania kwamba, kila hospitali ya kanisa inapewa ruzuku. Jamani vichwa ngumu hebu eleweni hili: SI KILA ZAHANATI YA KANISA IMETAIFISHWA. Si kila utakapoona kanisa limejenga zahanati basi udhanie matibabu hapo yanagharamiwa na serikali. Hospitali zinazopokea ruzuku ya serikali zinafahamika na ukienda huko gharama za matibabu ni sawa na hospitali za serikali kwani hata namna ya uendeshaji na usimamizi huratibiwa na serikali. Sasa mtu usikurupuke huko ukaenda Kibangu Mission Hospital ukadhani wakatoliki walijenga kutoa huduma kwa niaba ya serikali.

Ama lah, kama unaweza kuthibitisha uanaume wako kwa kutoa mfano ulionyooka juu ya wapi umewahi kutozwa zaidi ya viwango vya serikali ktk designated hospital basi weka hapa ili serikali na wanaJF wengine wajue, lkn sio kuleta upotoshaji wa kijinga hapa.

Tumia akili yako kutofautisha gharama kati ya HOSPITALI ZA KANISA ZINAZOPOKEA RUZUKU NA KURATIBIWA NA SERIKALI NA HOSPITALI BINAFSI ZA KANISA. Mimi sio mantiki ya mtu kujivunia ujinga na kuwaambukiza wenzake kwa kisingizio cha kupigania imani. Kama kitu hujui uliza uelekezwe na sio kuongozwa na hisia. Siku moja moja mtokage huko buguruni mnakoishi muitembee Tanzania mjue mipaka yake na magumu ya wenzetu walio mbali na AMANA unakotibiwa wewe kabla hatujaanza kuropoka ujinga na kujazana roho za chuki kwa kisingizio cha dini.

Elimu kwanza!

Acha kutoa mapofu na kutukana watu eti kisa kutetea uwizi unaofanywa na kanisa?? through MoU

Hospitali za Bugando na KCMC wako kwenye mkono hizo 90billion zimeshindwa kuboresha au wamekula viongozi wa kanisa??

Lawama zinaenda kwa a. Serikali na hospitali zake b. kanisa na hospitali zinazopokea ruzuku maana hakuna tofauti na za serikali wote wezi wa hela za umma..

Unatokana nini au umeshikwa pabaya au udini unakusumbua mkuu..oops
 
Huu ndio upumbavu ambao ukiwafikia baadhi ya watu huuchukua kama ndio ukweli na kukubali kuandamana. Wapi ndani ya nchi hii kuna hospitali (inayopokea ruzuku) inatoza 40,000 kumuona daktari?

Ujinga wa wapinga MoU ni kudhania kwamba, kila hospitali ya kanisa inapewa ruzuku. Jamani vichwa ngumu hebu eleweni hili: SI KILA ZAHANATI YA KANISA IMETAIFISHWA. Si kila utakapoona kanisa limejenga zahanati basi udhanie matibabu hapo yanagharamiwa na serikali. Hospitali zinazopokea ruzuku ya serikali zinafahamika na ukienda huko gharama za matibabu ni sawa na hospitali za serikali kwani hata namna ya uendeshaji na usimamizi huratibiwa na serikali. Sasa mtu usikurupuke huko ukaenda Kibangu Mission Hospital ukadhani wakatoliki walijenga kutoa huduma kwa niaba ya serikali.

Ama lah, kama unaweza kuthibitisha uanaume wako kwa kutoa mfano ulionyooka juu ya wapi umewahi kutozwa zaidi ya viwango vya serikali ktk designated hospital basi weka hapa ili serikali na wanaJF wengine wajue, lkn sio kuleta upotoshaji wa kijinga hapa.

Tumia akili yako kutofautisha gharama kati ya HOSPITALI ZA KANISA ZINAZOPOKEA RUZUKU NA KURATIBIWA NA SERIKALI NA HOSPITALI BINAFSI ZA KANISA. Mimi sio mantiki ya mtu kujivunia ujinga na kuwaambukiza wenzake kwa kisingizio cha kupigania imani. Kama kitu hujui uliza uelekezwe na sio kuongozwa na hisia. Siku moja moja mtokage huko buguruni mnakoishi muitembee Tanzania mjue mipaka yake na magumu ya wenzetu walio mbali na AMANA unakotibiwa wewe kabla hatujaanza kuropoka ujinga na kujazana roho za chuki kwa kisingizio cha dini.

Elimu kwanza!
Mkuu huna haja kabisa ya kuja na matusi wewe jenga hoja nitakuelewa vizuri tu.. Ruzuku inayopewa kanisa hutumiwa vipi? wee nipe matumizi yake utanisaidia zaidi ya kusema sio kila zahanati inapewa. Linatolewa fungu na kupewa CSSC ambao wanapanga matumizi ya fungu hilo, sasa tupe Tax return za CSSC tutaweza kujadili kwa mapana na sio matusi, hunijui sikujui pengine naweza kuwa hata babako..
Madaktari ndio wamegoma na hatujui fedha tunazolipa zinatumika vipi, kuuliza hili limekuwa kosa?. Mbona mna panic kirahisi namna hii kuna maslahi gani ambayo sisi wengine hatuyafahamu kaisi kwamba mnachukulia personal.
 
Back
Top Bottom