Nawaunga Mkono Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawaunga Mkono Madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 25, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Uamuzi wa madaktari kugoma haukuwa uamuzi rahisi; ni uamuzi ambao umekuja ukiwa na gharama kubwa kwao na kwa taifa vile vile. Lakini uamuzi ambao umekuja kwa sababu umelazimishwa. Sera ambazo zimekuwa zikisimamia sekta ya afya zimeonekana kushindwa na sasa haya ni mavuno yake. Upo mgogoro katika sekta hiyo na licha ya kuongezwa kwa vitu bado inaonekana watawala wameshindwa kabisa kujenga mfumo wa kisasa wa afya.

  Hivyo, naamini madai ya madaktari ni hatua ya mwanzo ya kudai huduma bora na mfumo wa kisasa. Siamini kama ni suala la mishahara na maslahi ya madaktari tu; binafsi naamini ni suala linalohusiana na a comprehensive healthcare reform.

  a. Hatuwezi kuendelea kuwa na serikali inaendesha mahospita mengi ambayo haina uwezo wa kuyahudumia - wakati umefika wa kufikiria serikali kuachia hospitali - ibakie na hospitali kama za jeshi n.k Tunaweza vipi kuzitoa hospitali kutoka kwenye mikono ya serikali na kuzileta kwenye sekta binafsi au ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma?

  b. Mfumo wa sasa wa centralized policy ya afya kwa taifa zima hata kwa mambo madogo umepitwa na wakati. Ipo haja katika kuangalia mfumo wetu wa afya kufikiria jinsi ya kufanya healthcare kuwa na a local outlook zaidi na hivyo kuwa ni ya sehemu ilipo.

  c. Kuboresha maslahi ya watendaji wa sekta ya afya kwa kuweka motisha zaidi, uhuru zaidi na vile vile kuinua elimu. Mojawapo ya matatizo ambayo ni wazi yapo ni jinsi gani madaktari na wauguzi wetu wanakuwa upgraded katika ujuzi na elimu yao.

  Ni kwa sababu hizi na nyingine naamini kuunga mkono mgomo wa madaktari ni jambo la kizalendo zaidi kuliko kuendelea kukaa kimya. Wao madaktari wanapodai maslahi zaidi na mafao zaidi wajue kabisa kuwa wananchi nao wanajiandaa kuwadai wao zaidi katika huduma na ubora wa huduma wanazotoa. Hivyo, wasikubali kuachilia kirahisi hadi wawe na uhakika kuwa madai yao ya msingi kabisa yameangaliwa na yanalenga katika kuboresha sekta ya afya nchini.

  Nawaunga mkono madaktari katika mgomo wao!


  Msingi wa kuelewa Maadili ya Mgomo wa Madaktari - SOMA KABLA HUJACHUKUA UPANDE!
   
 2. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja mkuu!kama ningekuwa daktari ningekuwa wa KWANZA!
   
 3. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena vyema. Vitendea kazi duni na visivyopatikana kwa wakati, hospitali ya mkoa yenye kuhudumia population ya 1.6 na huduma bure kwa wajawazito, wazee, watoto chini ya miaka 5, wenye magonjwa sugu na hapo wamesema pesa ni 300M kwa mwaka ubudget kununua dawa, vitendea kazi. Inawezekana? Wizara imeoza, matokeo ya serikali legelege.
   
 4. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa serikali yetu hawana uchungu hata kidogo na mahospitali yetu wala madoctor wetu.
  Siku ambayo wafanyakazi wa hospitali ya Apollo huko India wakija goma kama hapa Tanzania,ndipo viongozi
  wetu watakapoanza kuzithamini hospitali zetu....lakini kama Apollo ya India hawatakuja kugoma basi tusahau
  huduma bora kwenye vituo vyetu vya afya! kwani wao wataendelea kutibiwa huko India....Tafakari!
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  I strongly agree on {b}. Itaondoa ukwasi usio na lazima.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mie nawaunga mkono na kama kuna sapoti yoyote naweza kutoa wasisite kunitafuta!!

  Juzi nilionea na mtu mkubwa huko wizarani anasema kuwa wamewaacha wogeme tu kwani hawawezi kushindana na dola....

  Kuhusu suala la kupeleka waginjwa India anadai hailiwezi kukoma kwa sababu baadhi ya wakubwa wanalazimisha wapelekwe!!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hizo ndizo zilikuwa fikra za Hosni Mubarak na Gaddafi! Wote waliamini kuwa dola iko juu ya wananchi. Ndio maana ni muhimu kwa wananchi kuonesha support. Watanzania tumekuwa tukigawanywa sana kiasi kwamba tunashindwa kusimamia hata vitu ambavyo tunajua vitatusaidia. kwa mfano, walim,u wanaweza wasiunge mkono madaktari kwa sababu madaktari watafanikiwa! wahandishi wanaweza wasiunge mkono walimu kwa sababu walimu watafanikiwa.

  Ni muhimu kwa wananchi kuwaunga mkono madaktari kwa sababu matokeo yake ni lazima yawe mabadiliko. Kwa mfano, wanafunzi wa vyuo vikuu wako wapi kuunga mkono madaktari?
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Unaonga mkono kwasababu wewe na wanao mnatibiwa US..ha ha ha
   
 9. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naunga mkono 100% kwa 100%
   
 10. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Well said mkuu
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hii ni siasa tu
  Tanzania haipo sawa na Egypt wala Libya

  kama wanasiasa wameshindwa kutoa shinikizo kwa watala
  madaktari wasitumike kufanya siasa huku 'watu wasiokuwa na hatia' wanakufa...

  serikali iliyopo ni kama viziwi

  walijaribu chama cha wafanyakazi na wakazimwa.....

  kilichopo sasa ni kujaribu kutoa maji kwenye jiwe while wasio husika ndo watakufa.....

  tunajidanganya mno na kuiga Misri na Egypt.....ukweli sisi bado saana.....

  wamefukuzwa wanafunzi chuo kikuu hakuna mwanasiasa aliekwenda kuwasaidia.....
  tusiwaponze hawa madaktari

  utawala huu unahitaji 'political interverntion...na sio madaktari'
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ​Napinga migomo ya madaktari lakini naunga mkono kama wangefanya maandamano baada ya kazi kwani mwisho wa siku katika mgomo wao watanzania wa kipato cha chini ndio wanaoteseka na si viongozi wa serikali kwani wao wataenda kutibiwa nje ya nchi na kuacha wanyonge wakifa
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  a) yako naipinga mpaka nakufa, Tafadhali hii sio USA hii ni Tanzania.
   
 14. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Hospitali zilizokuwa za missionary zirudishwe kwa wenyewe serikali imeshindwa kazi nukta. Hospitali za Mission zikirudi hata hizi clinic uchwara zitapungua kwani wengi wataona gharama nafuu kwa hospitali za mission. Huhuhuuuuuu! sirikali yetu imefulia mwanzo mwisho!!!!
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  I smell udini, missionary haijawahi kujenga hospitali zimjengwa naserikali ya kikoloni ambao walikuwa wakiongoza kikristo; walitumia kodi za wananchi wote wa Tanzania, "Hakuna hospitali ya missionary" kuna hospitali za zilizojengwa na serikali za wakoloni wakristo
   
 16. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Acha ulevi wa kidini na kutumiwa na shetani kupotosha ukweli wewe. Hospitali, shule na asasi za kikristo zilizojengwa na wamisionari zilijengwa kwa misaada toka kwa wakristu wenzao waliokuwa ulaya ambao kwa wakati ule walikuwa wakereketwa haswa wa imani zao na kamwe serikali ya mkoloni haikuhusika. Kwa umakini waliokuwa nao wenzetu wazungu kila kumbukumbu ya wahusika katika kuzijenga asasi hizo zimetunzwa na zinaweza onyeshwa hadharani. Kwa bahati mbaya waarabu (Waasisi wa uislamu) walikuwa bize kutafuta watumwa wa kuwabebea pembe za ndovu na mbao toka Kongo na Kigoma na walitumia kiasi kidogo sana kujengea misikiti tena sehemu walizokuwa wamekaa. Waarabu hawakuwa na "Interest ya kujenga zahanati wala shule zaidi ya "madras". Nyerere ambaye kwa upofu wa baadhi yetu tunaomtazama kwa makengeza ya upotoshi na uzushi kama wako kwamba eti aliukandamiza uislamu ndiye aliyezitaifisha asasi hizo, si kwa ajili zilijengwa na "serikali ya mkoloni" bali ili kutoa fursa kwa wengi hata waliofuata imani za asili na waislamu wahudumiwe bila ya hofu ya kubadili imani zao.
  Sisi waislamu si wachangiaji wazuri wa maendeleo yetu, tazama hadi leo hii ambapo tuna maelfu ya mabilionea tunashindwa kujichangisha kuanzisha asasi za maana kiasi cha "kusaidiwa" na serikali hata katika upatikanaji wa Chuo Kikuu kule Morogoro!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi kabla ya mgomo wagonjwa walikuwa wanapata huduma nzuri na watu walikuwa hawafi kwa sababu walikuwa wanapewa huduma nzuri mahospitalini?
   
 18. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Naunga Mkono madai ya Madktari, naomba wasikilizwe wana point-nao ni watu wanahitaji kujikimu. Pesa ipo wanasiasa mnaichezea.
  Udaktari ni fani inayohitaji kupewa kipaumbele cha juu kama ambavyo walimu inawapasa.
  Hesabu za mwaka47, Kauli mbinu za kiprimitive!! Wanasiasa walio wengi ni wajanja wajanja/Matapeli huwa wanakuja na kauli mbiu kuwa Eti Fani hizo ni WITO. Lakini ukilinganisha na kauli mbiu ya inayowabeba wanasiasa angalia toka ngazi ya Diwani hadi Juu mtu anaanza kuitwa MHESHIMIWA hivyo wao kujikweza na kudidimiza taaluma za ukweli.
  Ukija ktk maslahi hali bado si shwari-Waheshimiwa hata kama yeye ni la Saba lakini anakuamulia nini ulipwe, inaboa sana.

  Inashangaza sana kuona watu hawa adimu pamoja na wahandisi wanabembelezwa sana kusoma na hata kupewa mikopo 100% na bodi ya mikopo. Wengi wa hawa wanalazimika kusoma masomo haya magumu ni watoto wa wakulima, watoto wa wanasiasa wao wanakuwa wanaandaliwa mazingira kuja kuwaongoza hawa.
  Mie sishangai kuona leo hii Bodi ya mikopo inaanza kuwatoza Riba hawa hawa waliohangaika. Wanaokusanya hiyo pesa ni wale wale watoto wa wakubwa.

  Ualimu na Udaktari ni WITO, Siasa ni Uheshimiwa
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kabla ya mgomo watu walikuwa wanapata hudumu kwa kiwango fulani, lakini kama mgomo ukiendelea basi huduma zitasimama kabinsa na vifo vitaongezeka mara dufu, na vifo vyenyewe vitakuwa vya watanzania masikini wasioweza kwenda hospitali za gharama kubwa. uwepo wa hospitali za umma unasaidia kwa kiwango kikubwa kuliko kutokuwepo kabisa
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,578
  Trophy Points: 280
  Wakati Wabunge wamejiongezea posho ya 200 kwa siku na kikao chao ambacho ni masaa 7, wanaanzia saa 3:00 mpaka saa 7:00 mchana na kurudi saa 11jini mpaka saa 2:00 usiku, huku wamekaa kwenye kiti cha luxury wengine wakisinzia tuu au bila kuchangia chochote, huku wengine wakishinda canteen au just kurandaranda viwanja vya bungeni kuamkua jamaa!. Madaktari wao 10,000! kwa shift ya 8 hours usiku mpaka asubuhi!.

  Hata vile vi little brown envelopes vya usafiri wa waandishi wa habari minimum ni 20,000! kwa press conference ya 30 min!

  Hii ni dharau kwa madakitari wetu!, Acha wagome!.
   
Loading...