Mimi ni mmoja ya watu nisiyeunga mkono MGOMO wa madaktari.
Labda useme kwamba, wewe Gwota, huungi mkono MGOMO wa aina yoyote ile na sio ule wa madaktari peke yao, hapo labda nitaweza kukuelewa.
Nakubaliana kwamba madai yao ni ya msingi sana na serikali ndio kiini cha yote na inatakiwa iyashughulie haraka sana.
Hii si kweli, ni unafiki. Huwezi kusema unaunga mkono madai yao halafu hapo hapo unapinga hatua yao ya kuchukua
the only option ambayo ina nafasi ya angalau kuwapatia ufumbuzi kwani ni the most effective.
watu wamekuwa wanaunga mkono kwa ushabiki tu na sio kwa kuangalia uhalisia na uzito wa jambo, hv utajisikia mama yako au baba yako akifa kisa mgomo wa madaktari?
Sasa hapa wewe ndiye unaleta ushabiki wa kipuuzi labda kwa kuwa wewe huyo mama yako hata unao uwezo wa kumfikisha hospitalini au nje ya nchi akatibiwe. Watanzania wangapi wanakufa kila siku bila hata hiyo huduma? Asilimia ngapi ya Watanzania hawataona tofauti yoyote madaktari wagome wasigome.
You cant make an omelette without breaking some eggs!
ushauri wangu:
Km kweli sisi wananchi tunaumizwa na madai ya madaktari inatakiwa sisi ambao ni wazima tufanye maandamano nchi nzima kushinikiza serikali iwatatulie madai yao huku wao wakiwa wanaendelea na matibabu.
Hapa ndipo unapoturudisha kule kule ulikoanzia, je unajua
ripple effect ya mgomo wowote ule. Hao madaktari watafanyaje kazi kama hawawezi kufika hospitalini kwa sababu wanaotoa huduma ya usafiri wamegoma, watatoaje huduma kwa wagonjwa kama watu wa utilities (maji, umeme n.k.) nao watagoma...
au wa kumkomoa kati ya serikali na madaktari tujue tunachekelea vifo vya wajawazito, vikongwe, wagonjwa wa moyo etc.
Anayechekelea hivyo vifo unavyovitaja ni serikali na si wananchi, serikali ambayo kiongozi wake mkuu anaenda kutalii huku wananchi wake wanakufa - hizo milioni 300 wanazochoma kila leo huko majuu zingeweza kabisa kuwapunguzia makali ya maisha madaktari na wakaendelea kutoa huduma japo kwa shida.
Tuache ubinafsi na ushabiki usio na maana juu ya swala muhimu la afya zetu. sidhani km muda huu ukipata ajali mbaya na ukapelekwa ICU utaendelea kuchekelea mgomo wa madaktari.
Hivi unajua waziri akipata ajali mbaya hapelekwi ICU Muhimbili, anakimbizwa India...! Anayekupeleka Muhimbili ama hajali sana hata ukipoteza maisha kwani kama wanavyodai madaktari, huko kuna ukosefu mkubwa wa vifaa na dawa. Ni asilimia ngapi ya wanaopata ajali hufa kama mbwa kwa sababu hata hiyo zahanati wanaisikia tu!
wengi mnachekelea kwa kuwa ni wazima wa afya.\
Hapa ndugu yangu umechemsha na kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, asante kwa ujasiri wako. Ukweli ni kuwa wananchi wengi kila wakiamka salama asubuhi wanamshukuru Mungu, kwani wanajua fika jinsi utoaji wa huduma mahospitalini ulivyo duni na hapa hakuna wa kulaumiwa bali serikali.