MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,239
- 22,318
Wakuu bado ninasubiri kauli ya Mbowe kupinga "Wazanzibari" kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara huku bara. Kwa akili zake za kibaguzi nadhani hili pia lilitakiwa limuume na sio bandari tu. Siku nyingine mmiliki wa CHADEMA atafakari sana kabla ya kuropoka. Kauli yake ya kibaguzi ingekemewa sana na hayati Mwalimu Nyerere kama angekua hai. Au ni mbinu yake ya kuikosesha kura CHADEMA 2025? Hata kama kaamua kumuunga mkono Mama Samia ajitahidi kutumia mbinu salama.
Soma hapa chini taarifa ya wizara ya ujenzi na uchukuzi.
BARABARA ZA EPC+ F HAZITALIPIWA
Serikali imesema kuwa utekelezaji wa miradi saba ya ujenzi wa barabara kwa njia ya EPC+ F haitalipiwa na wananchi watakaotumia barabara hizo kama ambavyo baadhi ya wananchi wanavyodhani.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, wakati wa utiaji saini wa miradi hiyo ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika Kanda za Kaskazini na Kusini na kujengwa na makandarasi wanne (4).
“Tanzania haina barabara za kulipia mpaka sasa, hivyo upotoshaji unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kulipia kwenye barabara hizi si sahihi kwani barabara hizi ni za kawaida ‘high way’ kama zilivyo barabara nyingine” amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa mradi huu ni wa kwanza na mkubwa kutekelezwa nchini kwani utapita katika mikoa 13 na lengo likiwa ni kuboresha mtandao wa barabara nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea uzalishaji katika maeneo zinapopita barabara hizi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Barabara zitazojengwa zitapita katika mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Singida, Mbeya, Songwe, Lindi, Mtwara, Simiyu na Iringa na hivyo zitarahisisha usafiri wa wananchi na usafirishaji wa mazao ya misitu, biashara, chakula, uvuvi na ufugaji, malighafi za madini kama vile makaa ya mawe, grafaiti na Chuma”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa ametaja miradi itakayotekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara - Lupiro - Malinyi - Kilosa Mpepo - Londo - Lumecha/Songea (km 435.8) , Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42), Handeni - Kiberashi - Kijingu - Njoro - Olboroti Mrijo Chini - Dalai - Chambalo - Chemba - Kwa Mtoro – Singida (km 384.33), Igawa - Songwe – Tunduma (km 237.9), Masasi - Nachingwea - Liwale (km 175), Karatu - Mbulu - Hydom - Sibiti River - Lalago – Maswa (km 339) na barabara ya Mafinga - Mtwango – Mgololo (km 81).