Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.


Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).


Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====
Screenshot 2023-06-16 232024.png

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.
 
Barabara wala si kitu kipya kuna wahanga walivunjiwa nyumba zao barabara ya tanga kwenda pangani hawajalipwa fidia!
Sio kitu kipya Ulaya au Tanzania? Kipya ni nini?

Malalamiko Yako peleka Kuna husika ila Hii ni game changer hakuna Kiongozi amewahi Jenga Kwa wingi huo Toka Nchi hii Imepata habari..

Ujue nyie midembwedo wa Dar Huwa mnaropoka tuu bila kujua adha ya watu Mikoani.
 
Poor journalism. WTF is EPC+F?? Lengo la habari ni ujumbe uwafikie walengwa (wananchi), kutumia manano na vifupisho visivyoeleweka na wengi ni ukanjanja na unapoteza ujumbe wote kwa ujumla.

Unless kama huo mradi ni porojo tu na propaganda kwahiyo hiyo ni mbinu ili next time wasiulizwe zile barabara zinaendelea vipi.
Engineering, Procurement Construction and Finance
 
Hao wadau wakandarasi wanaoonekana wakisaini mikataba kazi hiyo watalipwa kwa hela ya kitanzania au fedha adimu za kigeni kama US$ Dollars ?
 
Sio kitu kipya Ulaya au Tanzania? Kipya ni nini?

Malalamiko Yako peleka Kuna husika ila Hii ni game changer hakuna Kiongozi amewahi Jenga Kwa wingi huo Toka Nchi hii Imepata habari..

Ujue nyie midembwedo wa Dar Huwa mnaropoka tuu bila kujua adha ya watu Mikoani.

Tuna uzoefu na hizo ahadi hewa. Ahadi ya hizo barabara ni za miaka na miaka. Halafu kusaini hapo haimaanishi mradi ndio uhakika wa kuanza maana ni hadi hela ipatikane, na kwa sasa hela hakuna. Hivyo huo wa usanii wa kusaka kiki za kisiasa tunaujua vizuri.
 
Tuna uzoefu na hizo ahadi hewa. Ahadi ya hizo barabara ni za miaka na miaka. Halafu kusaini hapo haimaanishi mradi ndio uhakika wa kuanza maana ni hadi hela ipatikane, na kwa sasa hela hakuna. Hivyo huo wa usanii wa kusaka kiki za kisiasa tunaujua vizuri.
Ahadi hewa watu wamesaini mikataba 😆😆 we Jamaa Bure kabisa..

Kwanza tangu lini Samia amewahi kukupa ahadi hewa? Kwanza sio Barabara tuu Bali Hadi kwenye Afya amefanya mapinduzi, kwenye Elimu ndio kabisa Watoto wooote wanapata mkopo na Sasa kawaongeza wa diploma,Ajira ndio usiseme..

Samia ni kichwa kingine,anataka awasaidie huko kwenye bandari Wajamaa mbakaza Kwa kung'ang'ania umaskini na ujinga 😁😁😁
 
Sikuupenda ujamaa na wote waliouanzisha na walioendeleza
Ujamaa mbaya sana na ni umasikini

Yaani tukijipanga vizuri na kuanza kuwafunga majizi basi tutafika mbali
Ujamaa ni mfumo wa hovyo na umaskini wa kujitakia..

Ndio maana nawashangaa watu kwenye ishu ya Bandari kama Kuna vifungu haviko sawa wakosoe na kubainiaha ila sio kuondoa mwekezaji,utakuwa ni upumbavu ule ule wa miaka yote.
 
Tuna uzoefu na hizo ahadi hewa. Ahadi ya hizo barabara ni za miaka na miaka. Halafu kusaini hapo haimaanishi mradi ndio uhakika wa kuanza maana ni hadi hela ipatikane, na kwa sasa hela hakuna. Hivyo huo wa usanii wa kusaka kiki za kisiasa tunaujua vizuri.
Anataka kuonekana anaipenda Tanganyika.
 
Back
Top Bottom