Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Siku za mwanzo mwanzo zitakua ngumu sana, utakosa usingizi, utaota ndoto za ajabu ila pambana humo humo, mimi nina zaidi ya miaka kumi tangu niache ulevi.
Mkuu usemayo ni kweli hata mi nishajaribu kuacha wiki ya kwanza nilikuwa nakesha usiku kucha usingizi nakuja kuupata saa 11 alfajiri, na nikipata usingizi ni full nightmare mwanzo mwisho mindoto ya ajabu haiishi, sometimes naota nipo chimbo ambazo Huwa na kunywa na washkaji tunapiga vyombo mara naota nimelewa mpaka nashindwa kutembea, Lakini nikijaribu kusema siku hiyo nishtue vyombo nalala kama mtoto na Wala sioti, mwisho wa siku kwenye hiyo acha na kurudia pombe nikajikuta nimeimaster hiyo hali nikaamua Toka moyoni nisinywe mwezi mzima nikaweza na baada ya hapo hata Ile kiu au hamu ya pombe Sina washkaji wanakunywa mi nawaangalia tu
 
Dawa yake inabid utengenezewe wewe Bila kuona inatiwa kwenye pombe na inabid iyandaliwe na mtu ambaye Ana roho ngumu maana ukishakunywa tuu pombe iliyowekwa dawa utatapika nusu kufa kila ukihisi harufu ya pombe utatapika sasa Hali hiyo itafanya kila ukiona mtu au pombe au harufu lazima utapike mzee utakuwa unakimbia vijiwe vya watu walevi,, Nina ndugu yangu sasa hivi Ana wiki hagusi pombe kbsaaa alikuwa analewa mpaka kujisaidia sasa hv yupo safiiiii kbsaaaaa yaaan akiona mtu amebeba bia kinacho muokoa ni mbio!
 
Wakuu mko salama?
Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe.
Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe,kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.
Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.
Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.
Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
usikate tamaa kuna msaada ikiwa wewe mwenyewe una nia thabiti ya kuacha uraibu, tumepitia huko ila tunapambana na hatutaka tamaa msaada upo nitakushauri kama utapenda nitafute 0717551211 au 0767551211
 
Wakuu mko salama?
Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe.
Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe,kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.
Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.
Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.
Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
Huwezi kuacha pombe kirahisi hivyo kama tayari umeshakuwa addicted,hapo inahitajika uamue kwa hiyari yako kumgeukia Mungu na kuacha maisha ya dhambi,kumbuka hiyo ni roho kabisa ya kishetani inayokutesa kwahiyo huwezi kuiondoa kwa nguvu zako mwenyewe kwakua mpango wa shetani ni kuua,kuiba na kuharibu...
 
Ni maamuzi tu wala hakuna haja ya kukaa mbali na wanywaji. Mimi nimekua toka mdogo nimezungukwa na walevi, wanywaji, wapiga vyombo, na wavuta sigara na bangi, class yetu olevel ilikua ya wapiga maji muda wote na mimi ndio nilikua nawapeleka vilabuni kupiga vyombo.

Nimefika advance mambo yalikua hayo hayo, tunatoroka kwenda kwenye vilabu vya pombe na washkaji, wanapiga wanazima nawakokita hadi bwenini, kote huko sijawahi kuigusa. Chuo kikuu the same, nikamaliza nikafanya kazi ya whole sales ya pombe za aina yote kwa bar na migahawa, nilikua nakesha bar, sijawahi kugusa.

Kwenye shughuli zangu za kila siku nimezungukwa wa walevi na wanywaji kila kona ila sijawahi kugusa.

Kunywa pombe, kuacha yote ni maamuzi, haihusiani kabisa na kwamba washkaji zako ni walevi basi na wewe unakua mlevi.

Hajaamua kuacha, akiamuq anaacha, ukiona anashindwa kuacha ni hajaamua.
Umeongea vema. Nami ninarudia,"HAJAAMUA".
 
Wakuu mko salama?
Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe.
Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe,kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.
Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.
Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.
Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
Pole mkuu. Mimi nilikuwa na issue kama hiyo. Hebu Google 'how to quit alcohol timeline ' hii kitu kwangu binafsi ilinisaidia sana.
 
Bro labda unatumia Kvant, maana ile ni kifutio.

Anyway , pombe mbaya .

Ila mm kuacha bado aisee, ntapiga hivi vilite vyangu kadhaa huku napiga soga .
Kistaff kabisa.
Weekend ndio najiloweka. Weekdays bia zako 5-6 upate hamu ya kula usiku.
 
Mnakunywa vipi pombe mpaka hamjui ilikuaje? au kutapika ?

Tumieni kwa kiasi, maisha ni yako, mwili ni wako, fanya starehe kiasi.
Watu hawajua hata kunywa pombe vizuri unakuta mtu ndani ya dakika 10 kamaliza chupa ya bia , anaagiza nyungine 🤔 wengi tu hawajui kunywa pombe kwa kustarehe mtu anagida ila alewe haraka bila kujua madhara ya unywaji wa pombe kwa mtindo huo
 
Nina kaka yangu, blood brother akitoka yeye kuzaliwa nafata mimi, jamaa amekuwa mlevi hatari, mbaya zaidi anaishi na mwanamke wake ambaye wana watoto wawili, imefika hatua, mwanamke anataka kuondoka na watoto arudi kwao akaanze maisha upya,
Mind you "Huyu brother ninaye muongelea hapa kipindi tukiwa wadogo, yeye ndo alikua na tabia njema na darasani alikua bright mno,
Sisi ndugu zake wengine wakati mzee akituchapa fimbo, huyu brother wangu alitumika kama mfano wa tabia njema
muangalieni afya,....wengi hukata tamaa wakishajua ni positive,...
 
Dr am 4 real PhD

Castle_Lite

Evelyn Salt

Huyu mwenetu eti anataka kuacha pombe 🤣 si bora aseme tu ameishiwa 😂😂😂
Anakunywa Kvant huyu. Lazima pombe aione mbaya. Ule mzinga ukiishusha mwenyewe inafuta kumbukumbu😂😂😂😂

Utaweza kusema unasave hela kumbe ukikolea ndio unatumia hela zaid maana una stimu za kiwaki , unaweza nunulia wahudumu bia na chakula na watu wengne hata huwajui.
+ asubuh unaamka mchovu hata kazin/dili zingne unanisikia uvivu wa kufanya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom