Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Natamani sana kuacha pombe ila nashindwa

Isenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
1,450
Reaction score
3,889
Wakuu mko salama?

Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe. Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe, kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.

Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.

Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.

Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
 
Nina kaka yangu, blood brother akitoka yeye kuzaliwa nafata mimi, jamaa amekuwa mlevi hatari, mbaya zaidi anaishi na mwanamke wake ambaye wana watoto wawili, imefika hatua, mwanamke anataka kuondoka na watoto arudi kwao akaanze maisha upya,
Mind you "Huyu brother ninaye muongelea hapa kipindi tukiwa wadogo, yeye ndo alikua na tabia njema na darasani alikua bright mno,
Sisi ndugu zake wengine wakati mzee akituchapa fimbo, huyu brother wangu alitumika kama mfano wa tabia njema
 
Go1AooyWkAAXLJB.jpeg

Mbona unafanya jaribio la ajabu hivo, uache ili iweje sasa yani......unatusikitisha wenzako.
 
Epuka ukaribu na watumiaji
Ni maamuzi tu wala hakuna haja ya kukaa mbali na wanywaji. Mimi nimekua toka mdogo nimezungukwa na walevi, wanywaji, wapiga vyombo, na wavuta sigara na bangi, class yetu olevel ilikua ya wapiga maji muda wote na mimi ndio nilikua nawapeleka vilabuni kupiga vyombo.

Nimefika advance mambo yalikua hayo hayo, tunatoroka kwenda kwenye vilabu vya pombe na washkaji, wanapiga wanazima nawakokita hadi bwenini, kote huko sijawahi kuigusa. Chuo kikuu the same, nikamaliza nikafanya kazi ya whole sales ya pombe za aina yote kwa bar na migahawa, nilikua nakesha bar, sijawahi kugusa.

Kwenye shughuli zangu za kila siku nimezungukwa wa walevi na wanywaji kila kona ila sijawahi kugusa.

Kunywa pombe, kuacha yote ni maamuzi, haihusiani kabisa na kwamba washkaji zako ni walevi basi na wewe unakua mlevi.

Hajaamua kuacha, akiamuq anaacha, ukiona anashindwa kuacha ni hajaamua.
 
Wakuu mko salama?
Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe.
Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe,kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.
Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.
Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.
Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
Acha pombe sasa
 
Mimi nilikuwa chapombe tena niliyekubuhu, ila niliacha, ukitaka kuacha pombe unaacha, huo uwezo unao, nguvu za kuacha pombe unazo, usitake kujipa vijisababu, wewe fanya maamuzi magumu acha pombe.
Siku za mwanzo mwanzo zitakua ngumu sana, utakosa usingizi, utaota ndoto za ajabu ila pambana humo humo, mimi nina zaidi ya miaka kumi tangu niache ulevi.
Nilikuwa nakunywa konyagi, gongo, beer na mataka taka yote ya ulevi tena nakesha kabisa kwenye ulevi na asubuhi bado napitia maeneo ya wauza gongo natia kitu ndani.
Leo hii ninaweza kwenda klabu nikacheza muziki na walevi na wala nisinywe pombe, na zaidi pia ninaweza hata nikanunulia watu pombe bila kuinywa, kwamba nimeshinda vita wala tatizo sio hela.
Zaidi ya yote pia muombe Yesu akupe nguvu.
 
Wakuu mko salama?
Wakuu kiukweli mpaka nimeanza kujichukia kuhusu unywaji wa pombe.
Mfano jana nimepiga maji hadi sijui nilirudije ghetto,sometimes kumbukumbu zinapotea sababu ya pombe,kiuchumi napo naathirika,yani naweza nikawa na ka laki moja kangu mfukoni,nikiingia bar tu hako kalaki kataisha na madeni juu.
Sasa asubuhi hii sijui ndo pombe jana nilizinywa nyingi au sijui ni nini nimeingia bafuni nimetapika sana.
Kwa kweli hii hali inanisononesha mno,natamani kuachana na huu unywaji lkn kila nikisema niache nitakaa siku mbili tu naanza tena.mfano leo nilipanga nisiguse pombe ila tayari kuna jamaa yangu ametoka kahama huko ana mpunga keshanambia jioni tukutane tupige vyombo.
Wakuu najinasuaje na unywaji huu wa tungi?
YESU aweza kukusaidia, njoo kwake. Mimi alinisaidia. nilitumikishwa na ULEVI kukuzidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom